Oppomall
JF-Expert Member
- Feb 8, 2017
- 3,683
- 3,966
FANYA BIASHARA ILIYOKUPA HIZO MILIONI KUMI.Habari ya muda huu wakuu,, Poleni na majukumu ya kila siku. Mimi kama kijana nimeamua rasmi kujikita kwenye kufanya Biashara maana ndiyo ndoto yangu ya siku nyingi sana.
Binafsi nimepambana hapa na pale nmebahatika kupata mtaji wa Tsh Milioni 10 hivyo nmeamua kujikita rasmi kwny Biashara na kwa kufikilia nmepata mawazo ya Biashara 4 ambazo binafsi ninazipenda na kuzimudu..
1. BIASHARA YA KUUZA VYOMBO VYA MAJUMBANI
-Hapa nitahusisha uuzaji wa vyombo mbalimbali ambavyo vinatumika kwny majukumu ya kila siku majumbani kama (Masufuria, Hotpots, Vijiko, Visu, Madeli, Ndoo za maji,Mabeseni,Chupa za Chai, Viti & Meza za plastic, Majaba etc)
2. BIASHARA YA NGUO NA PRODUCTS MBALIMBALI ZA WATOTO(0-3YEARS)
-Hapa itahusisha kuuza products mbalimbali za watoto wachanga hadi miaka mitatu(3) kama vile (Nguo, Nepi, Viatu, Kofia, Neti, Beseni za kuogea, Toys km Vigari & Midoli, Poda & Sabuni za watoto etc)
3. BIASHARA YA BIDHAA MBALIMBALI ZA UREMBO NA VIPODOZI VYA WANAWAKE
-Hapa nitahusisha bidhaa kama(Perfumes, Rasta, Lotions, Poda, Hereni, Lipstics, Cheni, Nguo za ndani,Madela etc)
4. BIASHARA YA VIFAA MBALIMBALI VYA UJENZI WA NYUMBA NA VIFAA VYA ELECTRONICS
Wakuu naombeni USHAURI kwa uzoefu wenu ni Biashara ipi hapo yenye return kubwa na bidhaa zake ni more Liquid (Rahisi kuuzika kwa haraka) na ni sehemu gani naweza kupata hzo bidhaa kwa urahisi na Bei nafuu kwa DAR ES SALAAM na changamoto pia za hyo biashara husika na kama itapendeza Location nzuri ya kufanya hyo biashara kwa DAR.
NINAWASILISHA KWENU WADAU KWA USHAURI.[emoji123][emoji120]
Case closed!!!