Nina mtaji wa milioni kumi; nifanye biashara ipi kati ya hizi nilizochagua?

FANYA BIASHARA ILIYOKUPA HIZO MILIONI KUMI.
Case closed!!!
 
daycare unyama sanaaa.
 
Huo ndio ukweli biashara inaendena na waganga mimi nakuambia hivyo kwa uzoefu nimezaliwa katika familia ya wafanyabiashara na mimi nafanya biashara
Naunga mkono hoja hata mimi biashara yangu ya majeneza kuna kipindi iligoma kabisa mpaka nikawaza nifunge tu nirudie kazi yangu ya zamani (wizi wa mafuta ya transformers)
Lakini kuna mganga nilimpata kipindi hicho alikuwaga ameletwa hapa Dom na kigogo mmoja wa serikali nikatonywa na chawa mmoja wa kigogo huyo nikamtafuta huyo mtaalam tukaelewana akaja kufanya setting hapa ofisini yaani biashara ilikubali mpaka nikaona sasa naelekea kuwa bilionea!
Baadae hali ile ilipungua tena nahisi nilitakiwa kurenew setting ila tatizo nilipotezaga namba za yule mganga halafu yule kigogo naye alishahama hayupo huku ila natamani sana ningepata tena mganga kama yule ningekuwa mbali
 
[emoji23]biashara ilikubali kwahyo watu walikufa sanaaa daaahh[emoji119]
 
Hakuna mganga anayeweza kukupa dawa ya biashara,yeye na familia yake masikini halafu akupe dawa ya biashara!kama anayo si angewapa watoto wake au ndugu zake.
Mnajiongopea tu,ingekuwa hivyo Afrika ingeongoza kwa kuwa na matajiri wengi Duniani.
Tushakwambia we bado chalii sana katka maswala haya, kaa kimya.
 
Hii 10M umeipata kwenye biashara gani? Kwann usiendelee nayo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…