Nina mtaji wa sh million 6 ambayo mpaka sasa sijajua exactly ni biashara gani nifanye

Joined
Sep 10, 2014
Posts
84
Reaction score
26
Habari ya muda huu wakuu.
Mimi ni msichana wa miaka 24, nimeajiriwa katika kampuni ambayo masaa 8 nakuwa kazini na ninaishi dar-es-salaam nina mtaji wa sh million 6 ambayo mpaka sasa sijajua exactly ni biashara gani nifanye ili kuizalisha pesa hiyo na bila kuingilia ratiba yangu ya kazini maana nafahamu biashara nyingi zinahitaji usimamizi wa karibu sana ili kuepusha vitu kama kutapeliwa pesa.
Nilishawahi kufanya biashara ndogo ndogo nikiwa chuo kama kuuza nguo na viatu kwa wanachuo wenzangu wa jinsia ya kike.
Kwa kuileta mada hii kwenu nina imani nitapata msaada mzuri wa mawazo ya biashara kutokana na hali yangu halisi ilivyo.
Ahsanteni.
 
Una 2900$ dollars, only 29 a hundred dollar bill!? Biashara zipo nyingi mno mtaji wake hauzidi laki mbili kilichopo ni ubunifu

Hata hizi hizi wanazofanya watu kila.Siku Ukizitwist kidogo tu ukaimplement idea yako ni bonge la biashara
 
fungua mpesa na bank wakala ..ni rahisi kusimamia coz transaction zote zinakuwa na statement.Au fungua salun ya kiume unaweka mtu mnaelewana kiasi atakachokupa kwa wiki afu gharama zingine zote zinakua zake(kama wanavyofanya daladala)
 
Una 2900$ dollars, only 29 a hundred dollar bill!? Biashara zipo nyingi mno mtaji wake hauzidi laki mbili kilichopo ni ubunifu

Hata hizi hizi wanazofanya watu kila.Siku Ukizitwist kidogo tu ukaimplement idea yako ni bonge la biashara
Binafsi naposikuaga maneno km yako hapo ndo kichwa hukatika breki na kuongeza mwendo wkt mteremko ni mkali sana.

Hapo kwenye ku twist mkuu hebu tutwistie IDEA moja km kweli unamaanisha kiuhalisia au kimaandishi.
 
Habari ya muda huu wakuu.
Mimi ni msichana wa miaka 24, nimeajiriwa katika kampuni ambayo masaa 8 nakuwa kazini na ninaishi dar-es-salaam nina mtaji wa sh million 6 ambayo mpaka sasa sijajua exactly ni biashara gani nifanye ili kuizalisha pesa hiyo na bila kuingilia ratiba yangu ya kazini maana nafahamu biashara nyingi zinahitaji usimamizi wa karibu sana ili kuepusha vitu kama kutapeliwa pesa.
Nilishawahi kufanya biashara ndogo ndogo nikiwa chuo kama kuuza nguo na viatu kwa wanachuo wenzangu wa jinsia ya kike.
Kwa kuileta mada hii kwenu nina imani nitapata msaada mzuri wa mawazo ya biashara kutokana na hali yangu halisi ilivyo.
Ahsanteni.
Nashauri endelea na biashara hizohizo ndogondogo zinalipa sana.Cha msingi panga ratiba nzuri ya muda wa kusimamia baada ya kazi.Mf. unaweza tafuta vijana wakakufanyia biashara wewe ukaweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha unawasimamia.Mfano wa biashara hizo ni kama vile kuchoma mahindi,kuuza vitafunwa na uji.Ukiangalia kwa haraka haraka unaweza kudharau lakini kadri unavyokuwa na vijana wengi ndivyo unavyopiga pesa.Kama huna muda wa kusimamia ninaweza kufanya hivyo kwa makubaliano maalum.
 
Hii ni changamoto inayotukumba wengi sana kutokujua fursa ya namna na wapi pa kuwekeza mitaji yetu.

Ngoja na mm nijibanze hapa pembeni niibie nondo.
Mi pia nataka nijiingize kwenye biashara walau jmosi na jpili nishindege huko. Kitu chenye tija ndio changamoto sometimes nawaza nifanye car wash ila sijui pa kuanzia
 
Tumia M3 kuvuta boda mbili. Au bajaji Moja.

Tumia M1 kusoge karibu na maeneo ya vyuoni tafuta frem, vuta mtumba (viatu au nguo au vyote) flani stereo (wa wadada) panga

Tumia M 2 kununua nafaka. Uza reja reja.
 
Mi pia nataka nijiingize kwenye biashara walau jmosi na jpili nishindege huko. Kitu chenye tija ndio changamoto sometimes nawaza nifanye car wash ila sijui pa kuanzia
Kama unafikiria kufanya biashara hiyo basi jiongeze.Kuna sehemu nimeiona fursa hiyo .Nenda pale nyuma ya jengo la GEPF kwa nyuma kuna parking kubwa ya magari hakuna huduma hiyo japo Luna vijana wachache huwa nawaona na baadhi ya walinzi wakiosha baadhi ya magari lakini hawako rasmi na hawana cage zile za kupandisha gari kidogo iwe juu ili ioshwe vizuri na hawana mipira ile maalum yenye pressure kwa ajili ya kusafisha uchafu sugu nk.Nenda serikali ya mtaa kaombe kibali cha kuweka car wash, na kitambulisho chako cha mjasiriamali uanze kazi.Nafikiri mpaka hapo utakuwa umepata pa kuanzia.All the best.
 
Asante mkuu wacha kesho nitembelee maeneo hayo. Nipate kujionea
 
Habari ya muda huu wakuu.
Mimi ni msichana wa miaka 24, nimeajiriwa katika kampuni ambayo masaa 8 nakuwa kazini na ninaishi dar-es-salaam nina mtaji wa sh million 6 ambayo mpaka sasa sijajua exactly ni biashara gani nifanye ili kuizalisha pesa hiyo na bila kuingilia ratiba yangu ya kazini maana nafahamu biashara nyingi zinahitaji usimamizi wa karibu sana ili kuepusha vitu kama kutapeliwa pesa.
Nilishawahi kufanya biashara ndogo ndogo nikiwa chuo kama kuuza nguo na viatu kwa wanachuo wenzangu wa jinsia ya kike.
Kwa kuileta mada hii kwenu nina imani nitapata msaada mzuri wa mawazo ya biashara kutokana na hali yangu halisi ilivyo.
Ahsanteni.
Fanya Forex and Allience in global motion.
 
Please note the following.

1.Mafanikio hayaji kwa sababu umefanya kitu kipya kabisa tu bali hata kile wengine wanachofanya ila unaamua kufanya kwa njia tofauti .( tafuta uniqueness)

2.Unapofanya kitu usichokipenda toka moyoni utatumia nguvu kubwa sana kufanikiwa tofauti na mtu ambaye anafanya kitu akipendacho kutoka moyoni. UNAPENDA NINI?

3.MONEY NEVER STARTS AN IDEA, IT IS THE IDEA THAT STARTS THE MONEY.

to be continued
 
Kama umeweza kujiwekea mpaka kufikisha hapo natumaini hata mara 4 yake unaweza pia.
Kama unapenda kazi yako na inakulipa kiasi cha kupata na akiba basi nakushauri uendelee kuzikusanya tu kwa nguvu zote
Bado mdogo piga kazi kwanza na zikusanye haswa baadae utakuja kujua nini cha maana kufanya bila kuitegemea tena hiyo kazi
 
Huu uzi wamengolea vitu vingi

angalia changamoto wanazokutananazo ili uziepuke

hiki kitabu nikizuri kitakusaidia kufikiri nje ya box
Nitakipitia
 
Back
Top Bottom