You men! unasema huna mtaji, ungejiajiri, hivi unafikiri mtaji wa kujiajiri ni kiasi gani? ngoja nikuambie, Tafuta kama mradi walau wa 50,000/= andaa vizuri, angali na faida yake, design marketing strategy alafu uanze. Kuna wife wa my friend alikuwa anagombana na mume wake kwa sababu anataka mtaji wa 20,000/=, mume wake akaona hakuna biashara ya aina hiyo. Nikamwambia wewe mpe, mbona hapa jioni tushakausha more than fifty. basi jamaa akampa, wife wake akanunua materials ya kufumia mikufu, bangili na hereni akakaa chini kwa siku mbili, 20000 imeisha. bahati nzuri akapata mteja mmoja akanunua mikufu mitatu kwa 15,000/= akabakiwa na mikufu 4 na hereni 4 sawa na 21,000. Nakuambia huyo shem sasa ana 4 weeks amepata order ya mikufu 500 yenye thamani ya 2,500,000/=. Embu jitose, ni rahisi kufanya kazi ngumu kabla hujapata kuajiriwa.