Kuna mbinu nyingi za hii biashara kutegemea na aina ya miti
Kama ni miwati
Unanunua miti ikiwa mikubwa unakua unauza rejereja kwa watu wanaojengea kama milunda
Unakua unawauzia wanaochoma mkaa kama wapo katika hilo eneo
Unauza maganda ya miwati bila miti wanachuna huku miti imesimama wanakuachia miti hio miti utauza kama kuni za vigogo vya kupasua na nguzo za fence
Kama ni pines(mipaina)
Nunua miti iliyo midogo alafu kaa kama mwaka au miezi michache nenda mjini unakoishi (najua unaishi mjini ndiyo mana unaipata jf) tafuta mtu mwambie nina miti kijijini naiuza lazima akija nunua utamuuzia kwa bei ya juu
Nunua miti na subiri ikue alafu unapasua mwenyewe na kuuza mbao
Nunua miti mikubwa ipasue weka mbao stoo ikauke ikikauka vizuri bei huwa juu
Nunua miti mikubwa bila eneo ambalo ipo miti usipasue tafuta mtu mjini mpeleke kwenye miti yako muuzie
Tafuta mteja wa miti kabla ya kununua miti akikuambia bei nenda katafute miti kama aliokuambia nunua kwa bei ya chini alafu unamuuzia
Kama ni milingoti
Nunua milefu kama nguzo nenda kwa wanao nunua nguzo wauzie hii huhitaji kupelekewa
Nunua miti mikubwa pasulisha mbao na uza mbao
Nunua miti pasua mbao na uzipeleke mikoa yenye bei nzuri na uziuze(hii usipokua makini faida inaweza isionekane ila ukitulia huleta faida kubwa)