Nina Shamba Sijajua nipande nini,Ushauri Wadau

ikigijo

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2017
Posts
1,839
Reaction score
1,902
Habari Wadau Jf,
Nina Shamba La Ekari 10 lipo Bagamoyo Pwani Karibu na Kidomole.

Bado ninatafakari nilime nini,ambacho naweza kuitumia Ardhi vema.Nipo Naishi Dar.Angalau Mazao yasio ya Msimu itapendeza Zaidi.

Kulingana na Kazi yangu angalau bagamoyo nimeona ni Karibu kuwa na shamba.
 
Panda mihogo au korosho
Niliwahi fikiria wazo hilo ila nikakutana na maswali kichwani haya;
Korosho sasa hivi ni nzuri na zina bei nzuri sana ukianza kuvuna

Tatizo watu wanaiba sana sana,sasa hivi nimekuja huku lindi kuna kazi nafanya yaani wenyeji wanachofanya ni kushinda shambani muda mwingi...sasa kwa Mgeni kama una shamba unaweza lia.

2.Kuhusu mihogo sijajua Ardhi ya maeneo hayo kama inakubali,ingawa nilitaka kitu ambacho sio cha msimu yaani ni vema nikatumia gharama nikipanda tuu nakuwa kazi ayngu ni kuvuna tuu,
 
Unashamba afu haujui nini cha kupanda!Huna tofauti na mtu ambaye ameoa afu hajui kazi ya mke,kwa ushauri wangu panda mawe yakikua vuna ponda kokoto, fungasha kwenye vifuko sambaza kwenye masupermarket.
 
Panda mirungi mkuu hutajutia nakuambia!
 
Unashamba afu haujui nini cha kupanda!Huna tofauti na mtu ambaye ameoa afu hajui kazi ya mke,kwa ushauri wangu panda mawe yakikua vuna ponda kokoto, fungasha kwenye vifuko sambaza kwenye masupermarket.
Kwani ni lazima uoneshe kuww wewe ni mvuta bhange!?
 
panda (ganja) pesa yake chapchap
 
Mkuu kwa uhakika wa kuelewa mazao gani yanatakiwa kupandwa kwenye shamba lako nakushauri uwasiliane na Kituo cha utafiti wa kilimo Mlingano, Tanga. Wao watakushauri vizuri sana baada ya kuchukua sampuli za udongo na kuzichambua kwenye maabara yao. Jamaa wapo vizuri sana tuwatumie, hutajutia watakuandikia ripoti safi ya ushauri.
 
Mkuu tafuta mtaalamu wa udongo apime kwanza udongo atakushauri nini uweke na hali ya hewa ya huko. Kubuni zao hakutakusaidia sana. Lakini mtaalamu anaweza kujua nini kitafanya vizuri na nini hakitafanya vizuri.
 
Safi sana. Hao wako vizuri ndio nilikuwa nawafikiria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…