Nina Shida kubwa sana, naomba msaada wa haraka

chatu mkubwa

Member
Joined
Aug 1, 2017
Posts
6
Reaction score
7
Mm n mwalimu wa shule ya msingi nilianza kaz 2014 mwaka huo huo nikafanikiwa kukopa mkopo ambao unanitesa kwel mpaka sasa mshahara wangu n mdogo Nina madeni kila kona mpaka kazi naiona gunia LA misumari,,,,

shida zaid kuna taasisi ya mtaani nilikopa 758000 nimelipa 350000 baada ya hapo nlipata matatizo yaliyopelekea nishindwe kurejesha PESA iliyobaki deni ilitakiwa liishe januali jamaa wamenifuata juzi wakanipigia mahesabu kwa riba natakiwa nilipe milioni moja na laki saba 1700000

Mshahara wangu in laki moja na arobain 140000 Nina mke na mtoto mmoja naambiwa niwe nawapa laki moja kila mwezi wamedai nkienda tofauti wananipeleka kwenye vyombo vya sheria ntaishije Mimi kwa 40000 inayobaki

Naomba MSAADA wa mawazo hasa kisheria maana sina amani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama mda wa mkopo ulishaa wao wameshika mpini itakula kwako.dah na ukiendelea kuwalipa kidogo kidogo uo mkopo autakuacha maana kiasi kinaongezeka kadri mda unavyoenda
 
Pole kwa matatizo... wadau wanakupa msaada ila na mi lazima nikuchane kiume.


Next time ukikopa... lazima utambue haya.

-pesa ya mkopo si ya kujengea wala kununulia kitu ambacho hakirudishi pesa kiwepesi ,,,
Yaani ununue kiwannja na haujengi... it means umezika pesa unakula nyaasi.

Sent from "La -Vista"
 
Samahani mkuu kama nitakukwaza kuquote text yako

Huyu mtu hahitaji ushauri ila anachotaka ni ushauri nasaha kwa sababu huwezi ukamwambia ivo mtu ambaye tayari kashaathirika na tatizo ebu jitahidi mpe mawazo yako japo kidogo afanye nini ili ajikwamue ushauri wangu utakuja!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa upande wangu mkuu nakupa pole sana for all which happened!
Ila kwa hio fedha arobaini ni fedha ya housegirl na huwezi ukaishi kwa hio hela mtu na familia cha kwanza kabisa chunguza mali zinazokuzunguka nyumbani kama zipo either miti,ng'ombe,au rasilimali yoyote ile na uiuze ili ulipe deni
Kama hauna kabisa jitoe ufahamu siku za wikendi panga semina za ujasiriamali ukafundishe huko na utalipwa kuhusu hili njoo nikupe uzoefu bure kabisa lakini second washirikishe ndugu jamaa na marafiki wa karibu wakusaidie lau fedha kidogo kama mchango au hata mkopo bila riba ili kuzuia riba isiendelee huko ulikokopa,third fanya kazi ya udalali ambayo haina mtaji wowote ili kukuongezea kipato unaweza ukawa darali wa mifugo,nyumba,vifaa vya ujenzi,vuombo vya usafiri n.k,ukishindwa kabisa kabisa kabisa acha kazi ya ualimu maana hio laki nne na 19 sio hela kabisa maana hautafika dar hata siku moja utafia mikoani

Usiku mwema ndugu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ok.wewe na mkeo mpangane biashara ndogondogo muongeze kipato.lakini jisalimishe kwenye sheria kaeleze ulipokwamia kama binadamu nadhani kwakuwa unauhakika wa kupokea mshahara utapangiwa marejesho kila mwezi na zile riba zitasamehewa.salini mkiomba kwani madeni ni mkosi ndani yaani ukizidiwa madeni utampa sababu mke kuliwa nje huko.fikirini kabla ya kutenda kujengea wazazi si kwa mikopo ya riba tumia mshahara kwani nyumba mbovu ndo uliyokulia pale.taratibu pangeni mambo yenu.Mbarikiwe sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
samahani wote nitakaowakwaza, hivi kweli mwanaume umetoka tu chuo hali ya nyumbani kwenu unaijua halafu unakomaa kuoa haitoshi unakopa ili ujenge kwa mshahara wa laki tano na hauna shughuli myingine ya kufanya hata kufundisha tution, jiongeze
 
Pole sana mkuu, jaribu kuongea na marafiki wa karibu au ndugu waweze kukusaidia au kukukopesha mkopo usio na riba, au hata mwajiri wako ili umalizane nao..mkuu watu hukopa pesa kwa ajiri ya biashara ...pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…