Nina Shida kubwa sana, naomba msaada wa haraka

Kukopa harusi, kulipa matanga

Ongea na huyu mtu uliyemkopa apunguze deni. Mwambie income yako hauwezi kumlipa 100,000 kila mwezi. Lakini unaweza kumlipa 50,000 kwa mwezi. Mwambie kama hutakuwa hata na hauna nauli ya kwenda kazini kwa sababu pesa yote anachukua yeye hautaweza kumlipa. Mwambie awe reasonable.

Pia kama mambo yote yanashindikana waite ndugu wote fanya kikao. Kuona kila ndugu anaweza kusaidia kiasi gani. Utawalipa kidogo kidogo ndugu zako.
 
Lipa tu Mkuu dawa ya deni ni kulipa hakuna namna walipe tu laki moja mikoani kwa elfu 40 unaishi tu mke mrudishe kwao na mtoto mkopo ukiisha atarudi kwani nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaa nao chini, lkn kama hawajasajiliwa subiri mwende mahakamani, mahakama itaamua kwa haki ukifika eleza hali halisi ya mshahara wako
 
Ndugu kama haitambuliki li sheria usikubali,kubali waende kwenye vyombo vya sheria Maana hawatofanya Hivyo since wao sio taasisi rasmi ya kukopesha, hawalipi kodi na Wala hawaitumikii serekali. So kubali kulipa palipobaki tu pengine Acha na waambie wakupelekea kwenye vyombo vya sheria
 
pole mkuu ila kama ulivyoshauriwa hapo juu,omba msaada wa kisheria ili hayo mahesabu unayodaiwa pamoja na riba yaangaliwe upya,then hiyom taasisi je ipo kisheria na inaruhusiwa kisheria kukupesha watu?na riba yao imewekwa kisheria?,nasikitika nchi yetu haina taasisi inayothibiti haya masuala haya ya credit,ila the only way please pata msaada wa kisheria kutoka kwa watu wanaoelewa masuala haya.
 
Riba na marejesho ya mkopo lazima yalingane na kipato, kama kipato chako kweli ni 140, 000 wewe fikishana nao mahakamani tu, utapangiwa rejesho linalolingana na kipato chako.

Lkn hiyo habari ya nyumba usiitaje huko maana unaweza kupigwa mnada kulipia deni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah...lazima achanwe bana siku nyingine atie akili....
. Awauzie deni benki. Riba za mtaani ni kubwa sana na ni za muda mfupi tofauti na benki...

Sent from my beretta ARX 160 using JamiiForums Mobile App
 
Pole sana Mkuu; matatizo ni sehemu ya maisha kwa wanadamu.Ushauri wangu;
1.tumia changamoto hii kuwa fursa ya kukuvusha kwenda mbele zaidi.
2.jisalimishe kwa jamaa ukimshirikisha mwajiri na mwanasheria wa halmashauri ili wakusaidie kulisuluhisha hili na mengine yaweze kwenda.
3.kama unaweza kuendesha pikipiki au bajaj, omba day worker/ deiwaka ili ukitoka kazini uwe unapiga kazi za bodaboda.
4.mwambie mkeo ukweli ili mutumie kidogo kichopo kuanzisha mradi mdogo hata wa maandazi au ice cream ambapo awe anauza mwenyewe shuleni au nyumbani.
5.mshirikishe mwajiri ili akusaidie mikopo ya vijana na akina mama kupitia 10% ya mapato ya halmashauri.
Pole sana; usikate tamaa,yana mwisho na utavuka.

The Great Gatsby
 
Kama haitambuliki kisheria hapo unaweza unaweza kuacha kulipa riba iliyosalia maana ni taasisi za fedha tu ndio kisheria zinaruhusiwa kutoza riba. Jambo la msingi lazima ukusanye ushahidi vizuri kuonesha kuwa ulishalipa mkopo halisi plus riba nyingi tu lakini deni haliishi. Tafuta bush lawyer akusaidie kuwaandikia barua ili wasikusumbue

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…