Nina Shida kubwa sana, naomba msaada wa haraka

Niongezee kidogo hapo pia mkuu.

"Pesa ya mkopo pia siyo ya kusomeshea mchumba"
 
Kwa mtu mwenye familia huo sio mshahara wa kuutegemea hata kama hudaiwi na yeyote!

Mkuu,

Kakodi mashamba ya mpunga Morogoro, kilimo cha umwagiliaji.

Ama kodi vijana wakukatie mkaa uuze kwa bei ya jumla, utaweza rejesha huo mkopo.



Steve Jobs - Giant Of Technology.
 
Chatu mkubwa! Hii hali ya madeni hasa kwa sisi walimu imepindukia. Katika shule niliyopo tupo walimu wanne wenye madeni mengi! Mimi nadaiwa na taasisi 5. Nilitegemea ahadi ya mheshimiwa kuhusu kupandishwa daraja au mshahara mpya lakini imekuwa hola. Yaani hapa shuleni kwetu tunafanya kazi kama panya. Yaani tumedanga mpaka uongo umeisha. wapo wanaolipwa, wengine tunawasubirisha kwa kuwapiga chenga. Mshahara wa mwezi wa saba uliisha tarehe 4/8. usidhani kwamba kumefanyika manunuzi ya mwezi mzima! La hasha! Hakuna kitu kama hicho. Hivyo ni kukopa tu, hakuna namna.
Ndugu mji unakuwa mkubwa kama una amani. Kwa jinsi madeni madeni yalivyo mengi nahisi kama vile mji unanibana, yaani naona mji ni mdogo maana kuna mitaa si salama kwa mimi kupita, nadaiwa.
Natamani ningefanya kazi za ziada baada ya kazi lakini muda unabana. Shule haina nyumba hivyo naamka mapema kati ya 11 hadi 12. Saa 1:30 niwe shuleni. Kutoka saa 10:30. Hadi kufika nyumbani ni kati 11:30 hadi 12:00. na ninakuwa nimechoka.
Kwa kifupi naishi kama mtu ambaye hajui aendako.
TUPO WENGI!

Sent using Jamii Forums mobile app
 


mkuu taratibu kias na hicho kilimo!hana uzoefu nacho kitamkata! na ni gharama pia!labda anunue mpunga! naujua mpunga!
 
Pole sana mkuu I understand your situation, kwanza mkopo haujawahi acha mtu salama. Mkopo ni shida tu najua wengi watanipinga kwamba huwezi endelea bila mikopo lakini mi sikubali hata wale tunawaona kama mfano bado ukiongea nao wana matatizo makubwa sana na mikopo ndiyo maana unaona mtu anakuwa na mikopo hata 10 akijaribu kukopa sehemu moja kulipa nyingine.
Juzi nimeangalia tarifa kenya kampuni ya nakumatt karbia wanafilisiwa sababu madeni na mikopo mikubwa, je hawa nao si wanawatalamu wa fedha inakuwaje wanafilisiwa?
Nikirudi kwenye issue yako ningekushauri tu uende mahakamani hamna jinsi hapo upo kwenye kumi na nane, kama hao jamaa sio registered na hawalipi tax riba yao itafutiliwa mbali. Pole sana ikiwezekana achana na mikopo ni stress tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulijaza mkataba kuwa wamekukopesha pesa? Na je wanalipa code serikalin kwa biashara yao hyo ya kukopesha pesa je ni halali na inajulikana serkalin? Ka ni hapana bas kubali wakupeleke vyombo vya sheria, vichukuwe mkondo kama vp ni pm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu taratibu kias na hicho kilimo!hana uzoefu nacho kitamkata! na ni gharama pia!labda anunue mpunga! naujua mpunga!
Sawa mkuu, ni katika kutizama shughuli ambazo zitarejesha faida kwa muda mfupi ili aweze kuwalipa wanaomdai na yeye mwenyewe kuwa huru kifedha.

Steve Jobs - Giant Of Technology.
 
hiyo sehemu uliyoenda kukopa inatambulika na serikali?
kama walikupa kienyeji tafuta msaada wa kisheria
nadhani alipokuwa anakopa alikuwa na akili timamu (alielewa anachokifanya) mtaani wengi wanaopeshana kienyeji ile kusaidiana why akimbilie sheria kwa sababu kashindwa kulipa.
 
Defaulter.Ulikopa kwa malengo gani?,tuanzie hapo.alafu inaonekana una matatizo katika kumanage pesa.Jitahidi kuishi below your means na uepuke kukopa kusiko na tija.
Chamsingi ni kupambana,changamsha akili yako,tafuta kazi za part time kundisha tuisheni ama kuwa home tutor.tumia mazingira uliyonayo
 



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pengine wana hasira na wewe kwasababu ya ID yako Ya JF, unakopa hela ya watu halafu unajiita chatu mkubwa unategemea nini sasa unakoelekea utamezwa na mnyoo japo wewe ni chatu
 
Wakati unaingia MKATABA ,Huyo aliyekukopesha IWE ni taasisi Kampuni,MTU Binafsi alikuwa IMESAJIRIWA kwa kazi hiyo ya kutoa mikopo? JIRIDHISHE HILO KWANZA, Ukikuta hakuwa amesajiriwa kwa kazi hiyo, TAFUTA WAKILI HARAKA MFAILI KESI MAHAKAMANI ILI HATA ZILE PESA ULIZOWALIPA WAKURUDISHIE HARAKA.NA WAO WAPIGWE ADHABU KALI.Taasisi zote,awe MTU. Binafsi sheria inawataka wasajiriwe kwanza kabla ya kuanza kukopesha watu. HIVYO MKATABA ULIOINGIA NAO ULIKUWA BATILI KISHERIA,
 
Fanya hima uchunguze usajiri wa hiyo taasisi , Hata kama itakuwa imepata usajili hivi karibuni Lakini KIPINDI kile ulichokuwa umeingia nao MKATABA hawakuwa wamasajiriwa bado MKATABA huo ULIKUWA BATILI, Hivyo muone mwanasheria ALIYEKARIBU NAWE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…