Nina shida na mkopo wa 6M kwa marejesho ya miezi 10

Nina shida na mkopo wa 6M kwa marejesho ya miezi 10

Annonymous

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2013
Posts
688
Reaction score
1,126
Habarini wakuu

Ni mfanyabiashara na mwajiriwa wa kampuni moja ya mawasiliano Tanzania.

Nina shida na million 6 kwa marejesho ya kuanzia miezi 10.

Naamini baadhi yetu ni wazoefu wa mikopo. Wapi naweza kupata mkopo huu.
 
Siku hizi kuna mikopo kausha damu, mkopo wa miezi 6 inapatikana kwenye taasisi za kifedha, hiyo riba Sasa.

Bongo ukiwa na shida mkombozi ni asset tu, unauza asset unafanya mambo yako.

Wabongo tujitahidi tunapokuwa na nafuu za kiuchumi tuweke asset, hata dhahabu nunua weka ndani huwa haishuki thamani, hapa nazungumzia dhahabu halisi ama cheni genuine ya dhahabu au Pete genuine ya dhahabu siongelei matakataka yaliyookotwa migodini.
 
Habarini wakuu
Ni mfanyabiashara na mwajiliwa wa kampuni moja ya mawasiliano Tz.
Nna shida na million 6 kwa marejesho ya kuanzia miezi 10.
Naamini baadhi yetu ni wazoefu wa mikopo. Waapi naweza kupata mkopo huu.
Nenda bank au taasisi nyingine zilizosajiliwa kutoa mikopo.
 
Kweli ndugu assets ni kitu cha muhimu sana hasaaa hiyo dhahabu.....kuliko kukaa na maburungutu ya pesa nunua tu madini weka ndani
Hii nilistukaga kitambo nilikuwa na brother wangu mmoja kwa Sasa ni marehemu, tulikuwa mjini kati halafu mfukoni hatuna kitu.

Basi akaniambia twende kwa wahindi Indira ghandi tukachukuwe pesa nikawa na mashaka, tulivyofika kwa wadosi sonara wakatufungulia milango yao ya umeme bro straight akavuwa Pete akaweka mezani, mdosi akaichukuwa akaweka juu ya mzani akachukuwa calculator nikashangaa mdosi anatowa laki nane.

Sikuwahi kuwa mpenzi wa dhahabu na nilikuwa naamini bro ile mipete yake ni mifanfa tu kumbe alikuwa akinunuwa kwa sonata gramu za ukweli na ukikwama unarudi kwao unaawachia dhahabu zao wanapiga calculation wana angalia faida wanayopata unapewa cash bila mbambambaa, hapo ndio nilipata somo la kununuwa asset za jewels, siyo lazima cheni au Pete uzivae unaweza kuhifadhi ndani tu na ukiwa unazivaa siku za matukio muhimu tu lakini lengo lako siyo urembo Bali ni asset.
 
Ukipata huo mkopo ndo kufilisika kwako kunakuwa kumefika. Ni bora kuendeleza biashara kidogo kidogo..bila kukopa. Mikopo ya bongo ni pasua kichwa.

Yaani unakopa pesa riba kubwa, bado unatakiwa umkatie afisa mikopo, halafu ile pesa inaingia tu..unaanza kupeleka marejesho.
 
Hii nilistukaga kitambo nilikuwa na brother wangu mmoja kwa Sasa ni marehemu, tulikuwa mjini kati halafu mfukoni hatuna kitu.

Basi akaniambia twende kwa wahindi Indira ghandi tukachukuwe pesa nikawa na mashaka, tulivyofika kwa wadosi sonara wakatufungulia milango yao ya umeme bro straight akavuwa Pete akaweka mezani, mdosi akaichukuwa akaweka juu ya mzani akachukuwa calculator nikashangaa mdosi anatowa laki nane.

Sikuwahi kuwa mpenzi wa dhahabu na nilikuwa naamini bro ile mipete yake ni mifanfa tu kumbe alikuwa akinunuwa kwa sonata gramu za ukweli na ukikwama unarudi kwao unaawachia dhahabu zao wanapiga calculation wana angalia faida wanayopata unapewa cash bila mbambambaa, hapo ndio nilipata somo la kununuwa asset za jewels, siyo lazima chini au Pete uzivae unaweza kuhifadhi ndani tu na ukiwa unazivaa siku za matukio muhimu tu lakini lengo lako siyo urembo Bali ni asset.
Jewelry ni assets nzuri sana wahindi na waarabu huwa hawakai na maburungutu ya fedha ndani......wananunua dhahabu wanaweka ndani unaweza kushangaa mtu ananunua saa milioni mia mbili au cheni ya milioni 80 ukajua ni urembo kumbe mwenzako amewekeza waTanzania Bado hatujaamka na kuufahamu ulimwengu. Bado wengi hawajui sayansi ya fedha inavyofanya kazi.
 
Jewelry ni assets nzuri sana.....wahindi na waarabu huwa hawakai na maburungutu ya fedha ndani......wananunua dhahabu wanaweka ndani.......... unaweza kushangaa mtu ananunua saa milioni mia mbili au cheni ya milioni 80 ukajua ni urembo kumbe mwenzako amewekeza....... waTanzania Bado hatujaamka na kuufahamu ulimwengu......Bado wengi hawajui sayansi ya fedha inavyofanya kazi.....
Jewelry na land ni asset zisizohitaji rocket science kuwekeza, hazikutupi hata siku moja.

Mimi hii January kila nikiichungulia bill za shule bado zinanichanganya sizielewi, nakunywa kiwanja kimoja million 10, niliwekeza millioni 4 tu.
 
Siku hizi kuna mikopo kausha damu, mkopo wa miezi 6 inapatikana kwenye taasisi za kifedha, hiyo riba Sasa.

Bongo ukiwa na shida mkombozi ni asset tu, unauza asset unafanya mambo yako.

Wabongo tujitahidi tunapokuwa na nafuu za kiuchumi tuweke asset, hata dhahabu nunuwa weka ndani huwa haishuki thamani, hapa nazungumzia dhahabu halisi ama cheni genuine ya dhahabu au Pete genuine ya dhahabu siongelei matakataka yaliyookotwa migodini.
Asset hata nyapu nazo hazishuki thamani!
 
Jewelry na land ni asset zisizohitaji rocket science kuwekeza, hazikutupi hata siku moja.

Mimi hii January kila nikiichungulia bill za shule bado zinanichanganya sizielewi, nakunywa kiwanja kimoja million 10, niliwekeza millioni 4 tu.
Good move.....watu wengi Bado wana imani za kizamani kuwa utajiri ni kuwa na keshi..... kunahitajika elimu kubwa sana ya fedha kuwatoa watu gizani.....Mimi nilipopata elimu hiyo nimejikuta naichukia keshi......
 
Wanaosema dhahabu haishuki bei hawajawahi enda uza.

Bei yake inacheza sana

Pia unapoenda uza anayenunua hununua chini ya bei ya soko ili naye apate faida
 
Habarini wakuu

Ni mfanyabiashara na mwajiriwa wa kampuni moja ya mawasiliano Tanzania.

Nina shida na million 6 kwa marejesho ya kuanzia miezi 10.

Naamini baadhi yetu ni wazoefu wa mikopo. Wapi naweza kupata mkopo huu.
Uko wapi milioni sita utanirudishia 10m upo tayari uje na hati ya nyumba au kadi ya gari na mashaihidi 3
 
Jewelry ni assets nzuri sana.....wahindi na waarabu huwa hawakai na maburungutu ya fedha ndani......wananunua dhahabu wanaweka ndani.......... unaweza kushangaa mtu ananunua saa milioni mia mbili au cheni ya milioni 80 ukajua ni urembo kumbe mwenzako amewekeza....... waTanzania Bado hatujaamka na kuufahamu ulimwengu......Bado wengi hawajui sayansi ya fedha inavyofanya kazi.....
Asee unaona kabinti fulani kametia kikuku mguuni unakadharau na kukaita mwajuma n'chokonoe kumbe kametunza malaki ya pesa hapo.. Nimeipenda hii kanuni.

Utatumia mbinu gani sasa ili usiuziwe famba hata na hao masonara wanao aminika?
Cc Matola
 
Kwenye maduka ya jewelry kwa wahindi hakuna mbambambaa, dhahabu inauzwa kwa gramu, unatajiwa bei ya gramu kama ni pete au cheni, mzani digital uko pale inawekwa unasoma gramu mwenyewe, unanunuwa cheni au Pete kutokana na uwezo wako.

Kama sikosei bei ya gram moja kwa Sasa inaweza kuwa around tsh laki tatu au pungufu.

Sasa kazi ni kwako unataka kuhifadhi gram ngapi shingoni au kidoleni.

Ila nakuhakikishia hakuna duka la jewelry wanalouza dhahabu fake, huo ni uhuni wa huko migodini ndio wanauziana matakataka.
 
Back
Top Bottom