Nina-solve vipi huu msala?

Chura

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2009
Posts
1,385
Reaction score
2,402
Wajuvi naomba msaada wa Kitaalamu, Unatoka zako Job mwanao wa damu anakupigia simu uende mahali mkale vyombo, unamsisitiza wewe umepumzika anakwambia hata maji tu na msosi basi unaamua kwenda.

Umeenda kujiunga nao kupiga Vyombo ila ww ukawa hunywi, mwana na manzi yake wakawa wanaagiza sana yani shusha vitu weka vitu na misosi ya kuzidi, wakati huo wewe mzee mkubwa umeagiza maji tu, sasa wakati mnapiga vitu nwana anaanza ongea na simu afu anajikataa kiaina.

Yani unabaki ww na shemeji afu bonge la bili linakuja na ww mtaalamu una yako tu ile ya maji.

Gafla muhudumu anakuja anaomba bili, shift yake imeisha anataka kukabidhi, unamwambia nipe dk 5 unamuuliza shem vipi unakava? Unashangaa shem jasho linamtoka, mnampigia mwamba hapokei simu.

Hapo unajitoaje wajuvi unamuita waiter unamuambia kila mtu alipe? alichokunywa na kuagiza au unafanyaje maana shem anakuangalia kwa jicho la huruma yan ukilipa unamla bure bure, ila sasa huna noti unafanyaje wakubwa?
 
Hivi unafahamu katika medani za ajira, wanadamu huitwa "Rasilimali watu",kwa hio hapo ulipo na huyo binti nyie ni rasilimali, ni haki ya meneja wa hio sehem,kuwatumia anavyoona inafaa na itampendeza, Nitamlaumu mmiliki akiamua ya kwamba "mafuta" ndio solutions.
 
hakuna mwana wa damu anakiwa na mambo ya kinduza namna hiyo.
lakini huwezijua labda kapata ajali.
 
Kula jicho la shemeji mkuu.. kopa hata kwa mtu. Clear bills. Shemeji ana utamu wake.
 
Wewe uli solve vip?

I guess hii ni chai

Kama serious upo kwenye dilemma nitumie number na pic ya huyo demu nijifanye ndo jamaa aliyetokomea nije kuokoa msala[emoji848]
 
Sasa si mumpigie mshikaji awatumie hela?
 
Lipia maji yako alafu mwambie shemeji kila mtu ashinde mechi zake za nyumbani imeisha iyoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…