Nina tabia ya kupenda kucheka sana. Je, ni tatizo?

toplemon

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2017
Posts
4,612
Reaction score
4,721
Wakuu mimi nina tabia ya kupenda kucheka sana yaani napenda kutaniana na watu yaani nitacheka sana.

Ila ni kwa watu tuliozeana tu ila kwa mtu ambaye sina mazoea nae ni ngumu kuelewa kama mimi ni mcheshi au muongeaji kiasi kwamba hadi mtu akinikuta ambaye hajanizoea huishia kusema "kumbe anaongeaga hivi? Kumbe anachekaga huyu"..

Ila kwa watu tuliozoeana basi tutataniana nitacheka sana yaani nitacheka sana hadi sazingine nitacheka hadi nitakaa chini kama ni jambo la kuchekesha sana.

Jee hili ni tatizo?Jee haina tafsiri au mtazamo mbaya?Nataka nijuwe ili niache maramoja kama sio jambo zuri.
 
Usiache, cheka zako kwa raha zako.
Watu wana matatizo chungu zima wanalazimisha hata kucheka cheko linagoma.
Kuna nyakati za kufurahi na kucheka, na nyakati za kulia. Tumia huu muda kufurahi haujui kesho ina nini.
 
Kama bado una marinda basi yatakuwa yapo njia panda.
 
Nikija kupata mwanamke mcheshi hivyo sikuachi lazima niweke ndani niwe nafurahi kwa kweli.
 
Wa jinsia gani mwenzetu?

Comments zinategemea jinsia yako. Uchekaji chekaji wa mwanaume ni tofauti na kucheka cheka kwa mwanamke
 
Unge share picha yako ukiwa unacheka labda tungeweza kukusaidia.
 
Usiache, cheka zako kwa raha zako.
Watu wana matatizo chungu zima wanalazimisha hata kucheka cheko linagoma.
Kuna nyakati za kufurahi na kucheka, na nyakati za kulia. Tumia huu muda kufurahi haujui kesho ina nini.
Upo sahihi kabisa
 
Sio shidaaa
Mimi nacheka, naongea. Siku nikiwa kimya naulizwa una matatizo gani maana sio kawaida.
Tuendelee kucheka tu [emoji1635]
You are absolutely right
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…