Nina Tatizo la kugairisha mambo/mipango (Procrastination)

Bodhichitta

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2015
Posts
315
Reaction score
762
Nimegundua nina Hili tatizo la kugairisha mipango yangu ninayopanga baada ya mda flani.

Yaani naweza nikawa na mipango thabiti kabisa juu ya jambo flani ambalo ukiangalia Kwa mda huo nikilifanya linaweza kuniletea faida kubwa saana au kupiga hatua kubwa saana katika maisha ila Kwa bahati mbaya baada ya siku najikuta nafikiria saana na hatimae nagairisha Hilo jambo.

Mfano, nimeshawahi kupanga mipango ya biashara ambayo Kwa wakati huo ilikuwa inahitaji mtaji kama 4,500,000. Nilikuwa sina hata mia mda huo ila nikaweka mipango namna ya kufanya saving ili niipate hiyo ela.

Bahati mzuri baada ya kam miezi 9 nikapata hiyo ela, Cha ajabu akili ikabadilika na kuwaza vitu vya ajabu kwenye hiyo biashara hapohapo nikagairi.

Nikawaza biashara nyingine ambayo inahitaji 5,000,000. Nikasema haina shida ngoja niongezee ikifika nianze.

Baada ya miezi miwili nikapata 5M, Cha ajabu nikagairi kuifanyia kazi hilo wazo.

Nikaacha ela kwenye akaunti, nikaanza kuomba ushauri Kwa watu baadae nikapata wazo la kufanya ila Hilo lilihitaji 7,000,000. Ikanibidi niongeze hiyo ela mpaka ikafika 7M. Cha ajabu akili inaleta vitu vya ajabu kwenye hiyo biashara.

Mpaka baadae nikagairisha tena. Ikabidi niwaze kuwa huenda Nina shida sio Bure.

Nikaanza kusoma vitabu mbalimbali nikaja kugundua Hilo tatizo lipo na linawakumba baadhi ya watu.

Nikaamua nichukue zile mbinu nilizosoma kwenye vitabu mbalimbali ili kutatua tatizo langu ila Cha ajabu hakuna kinachobadilika.

Kuna wakati nikijaribu kuwaeleza watu juu ya mipango yangu wanasema ni mizuri na wananipa matumain yakuendelea nayo ila Cha ajabu siwezi kuianza.

Kama Kuna mtu analifahamu vyema hili tatizo naomba aniambie kinagaubaga namna gani naweza kuondokana na hili tatizo??

Naona kwangu ni mtahani mkubwa saana, na linaweza kunirudisha nyuma Kwa kiasi kikubwa.

Asante, naombeni msaada wenu tafadhali.

Nahitaji msaada wa haraka niweze kuifanyia kazi malengo yangu.
 
Nasubiri watalaamu waje
 
Kubwa zaidi kuomba ushauri kuhusu masuala ya mipango Yako ya maisha kama afya,elimu na biashara ni jambo zuri,lakini ni Bora zaidi ukaifanya mipango Yako bila kumwambia mtu mwingine yeyote,Kwa sababu unapoaaambia watu wengine wao watakupa ushauri kutokana na wao wanavyoelewa,hivyo utaanza kuyaona mapungufu kwenye mipango Yako,na mwisho utahairisha, hivyo kuwa na maamuzi binafsi ni vizuri zaidi.
 
Soma hiki kitabu hapa chini. Kina mapendekezo 21 practical ambayo ukiyazingatia yanaweza kukusaidia. Hata hivyo ni lazima utambue kwamba hili ni tatizo la kisaikolojia na itabidi uwe na dhamira ya kweli, kujikana na nidhamu binafsi ili kupambana nalo. Ni sawa tu na vita vya kuacha punyeto.

Nakutafutia na tafsiri ya Kiswahili na nikiipata nitakuwekea. Kama wewe mwenyewe hauko tayari kuamua hakuna atakayeweza kukusaidia. I am rooting for you 🙏🏿

➡️➡️➡️ Na kama una tabia ya kuangalia porn, kupiga nyeto, kujidharau; na kuzunguka mitandaoni humu bila cha maana anza kupunguza maana tabia hizo na procrastination zinakwenda pamoja.
 
Attachments

Angalia watu wako au jamii inayokuzunguka ikawa mfanani mitazamo.

Pili unapopanga unakuwa mkimya au na wewe ni wale nape kalewa rubisi kagera kaanza kuongea kihaya kwa kiswahili
 
Kikubwa ni huna uthubutu, una uoga wa kupoteza pesa,
Wengi tuna hilo tatizo, ila sometimes inahitaji tu akili ya kujilipua na kutenda
Sio tu kwenye pesa mkuu, hata kwenye suala lisilohitaji pesa.
 
Soma hiki kitabu hapa chini. Kina mapendekezo 21 practical ambayo ukiyazingatia yanaweza kukusaidia. Hata hivyo ni lazima utambue kwamba hili ni tatizo la kisaikolojia na itabidi uwe na dhamira ya kweli, kujikana na nidhamu binafsi ili kupambana nalo. Ni sawa tu na vita vya kuacha punyeto.

Nakutafutia na tafsiri ya Kiswahili na nikiipata nitakuwekea. I am rooting for you 🙏🏿
Asante, kiongozi ngoja nisome na hiki
 
Nishawahi kuisoma hii kwenye kitabu kimoja kinaitwa power of concentration ndo nilikutana na hii uliyoitaja wewe nimejaribu lakin wapi
Fanya dopamine detox utakua sawa.

Ondoa vitu vyote vinakupa distraction, mfn tv, social media n.k
 
Nimegundua nina Hili tatizo la kugairisha mipango yangu ninayopanga baada ya mda flani.

Yaani naweza nikawa na mipango thabiti kabisa juu ya jambo flani ambalo ukiangalia Kwa mda huo nikilifanya linaweza kuniletea faida kubwa...
kughairisha ni kuwacha kabisa kufanya.
Kuahirisha ni kuchelewesha kufanya.

Ulikusudia kuandika lipi kati ya hayo?
 
The desire of winning must be greater than the fear of loosing.

Mimi huwa natumia sheria ya 5S. Ndani ya sekunde tank Natalia kuanzia jambo. Unafanya kwanza alafu ntajifunza baada ya kufanya.
 
Back
Top Bottom