Nina tatizo la kuumwa kiuno,naomba msaada

alovera

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
220
Reaction score
173
Nina tatizo la kuumwa sana kiuno,wakati mwingine kinauma kinakuwa kama kinawaka moto hasa wakati wa usiku,nimetibiwa hospitali kadhaa kwa muda mrefu sasa (zaidi ya miaka miwili) ila sipati nafuu,naomba msaada kwenu wana Jf kwa yeyote anayejua dawa either za hospital au Tiba mbadala,ila za hospitali nimetumia sana ila sipati nafuu ya muda mrefu,napataga nafuu ya muda tu.
 
1.Acha kula pilipili 2.kunywa maji maji ya uvuguvugu litamoja asbh mchana na jioni 3. punguza chumvi katika chakula chako.chai yako tumia asali na tangawizi unapolala tumia mafuta ya habba soda kijiko 1 na asali kijiko kimoja kunywa.inaelekea wewe unauzito mkubwa dhibiti uzito usiongezeke ila upungue
 
Dawa ya Maradhi ya Kiuno

1.Uwatu kijiko kimoja kikubwa Kwa Kiingereza (Fenugreek)

2.Zaatari vijiko vitatu vikubwa Kwa kiingereza ( thyme)


3.Ubani (Dhukr)Mweupe Punje saba.


4.Maji chupa moja.


Unachemsha pamoja .


Matumizi: Unakunywa Robo Glasi kutwa mara tatu kila siku kwa muda wa siku 7 utapona inshallah.


Ngoja nimwite Dr MziziMkavu unahitajika huku!
Mkuu Baba Kelvin hujambo lakini?
 
Mkuu MziziMkavu hiko kijiko ni cha kulia ama kikubwa cha kupakulia?
 
Mzizi mkavu hebu nisaidie kuna rafiki yangu mara nyingine anavimba tumbo bila sababu linajaa upepo kamaliza hospital zote hakuna majibu je ni mapepo mabaya hebu msaidie jamani atumie nini
 
Asante Ndugu kwa ushauri wako, ninaufanyia kazi mara 1
 
Mzizi mkavu hebu nisaidie kuna rafiki yangu mara nyingine anavimba tumbo bila sababu linajaa upepo kamaliza hospital zote hakuna majibu je ni mapepo mabaya hebu msaidie jamani atumie nini
Mwambie anitafute kwa wakati wake ninaweza kumtibiana akapona. Anaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
pepo ilo! nenda ukaombewe kanisani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…