Nina tatizo la ngozi , yapata mwezi wa 5

Nina tatizo la ngozi , yapata mwezi wa 5

JELA

Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
14
Reaction score
4
habari jf doctor!

Nina tatizo langozi yapata mwezi wa tano tokea lianze, nimekwenda hospitali, nimepima mpaka damu kwa ajili ya HIV nikapewa majibu, nikaambiwa sina HIV, isipokuwa nimeliweka tatizo muda mrefu bila tiba.

Ni kweli tatizo lilianza muda mrefu kuanzia mapajani , kwani kulikuwa kunabadilika rangi na kuwasha , nilikuwa natumia dawa za kawaida za kupaka kama whitefield, na vidonge kama ketoconazole lakini bado. Baadae nikarudi nikaambiwa nifanye dematology kama sikosei ndipo jibu likaja kuwa tatizo limeingia kwenye damu.

Kwa sasa nawashwa mikononi, mapajani, miguuni na mgongoni pia sehemu zinazowasha ZIMEBADILIKA RANGI KUWA NYEUSI. msaada tafadhali jf doctor
 
Ukipata untifungal creams na steroid cream pamoja na oral tablets for two weeks
 
habari jf doctor, nina tatizo langozi yapata mwezi wa tano tokea lianze, nimekwenda hospitali, nimepima mpaka damu kwa ajili ya HIV nikapewa majibu, nikaambiwa sina HIV, isipokuwa nimeliweka tatizo muda mrefu bila tiba. Ni kweli tatizo lilianza muda mrefu kuanzia mapajani , kwani kulikuwa kunabadilika rangi na kuwasha , nilikuwa natumia dawa za kawaida za kupaka kama whitefield, na vidonge kama ketoconazole lakini bado. Baadae nikarudi nikaambiwa nifanye dematology kama sikosei ndipo jibu likaja kuwa tatizo limeingia kwenye damu. Kwa sasa nawashwa mikononi, mapajani, miguuni na mgongoni pia sehemu zinazowasha ZIMEBADILIKA RANGI KUWA NYEUSI. msaada tafadhali jf doctor
Tafuta vitunguu swaumu, utwange halafu upake Yale Maji yake baada ya kuoga kutwa Mara tatu, siku saba. Utapona kabisa na ngozi yako itarudi natural.
 
asante, sky eclat pia asante kideko
 
ntajaribu vitunguu swaumu pia sky eclat ni majina gani ya antfungal cream na steroid cream na tablets zipi ili niende dukani nikiwa najua naenda kununua dawa ipi?
 
Back
Top Bottom