Nina tatizo la nyonga kuvuta (kucheza)

Nina tatizo la nyonga kuvuta (kucheza)

Samireal

Member
Joined
Aug 16, 2015
Posts
88
Reaction score
22
Kuna wakati nilikuwa napata maumivu makali kwenye nyonga za ndani au naweza kusema nyonga za mbele wakati nikiwa nafanya mazoezi ya kukimbia na nilikuwa nahisi kama vile kitu kinavuta (kinacheza/kudunda) upande wa kushoto chini ya tumbo kwenye maungio ya mguu sometimes nilikuwa nahisi maumivu hadi kwenye korodani.

Ilinibidi niache mazoezi nikaanza kutumia dawa ya kuchuwa na maumivu yalipotea lakini kuanzia juzi nahisi kitu tena maeneo yale yale japo hakuna maumivu, je linaweza likawa ni tatizo gani na hospital linaweza kucost kama sh.ngapi?

Na je bawasiri inaweza ikawa inahusika na hili tatizo?
 
Back
Top Bottom