Wadau, nina 200 million TZS, je niweke fixed account benk ipi yenye interest nzuri ya mwaka?
Asante
Michango
==========
================
Tafadhali Kimla soma Ushauri kwa wastaafu na wanaopata hela nyingi kwa mkupuo - JamiiForums
Asante
Michango
==========
Mkuu salute!
Seriously fanya haya kwa pamoja baada ya miaka 5 utakuja kunishukuru hapa.
1.Nunua hisa za millioni kumi tu uweke malengo ya miaka 5, mfano hisa za CRDB bado ziko chini na zinaweza kupanda sana tu hata mara tano baada ya miaka hiyo mitano.
2.Chagua kuwekeza kwenye UTT au hatifungani za serikali. Napo unaweza kuwekeza hata million 40.(utt +hatifungani)
3.millioni 100, weka fixed account..tafuta benk hizi ambazo ni global.banclays kwa sasa inaitwa Absa,fnb,bankABC interest zake ni kubwa kuliko hizi local banks.
4.millioni 25 weka kwenye biashara ya nafaka...mfano mpunga ,au ndegu,au choroko...hutajuta wala usiogope.(niulize nitakuogonza)
5.Millioni 25 njoo tufanye biashara ya pamoja,Mimi Nina wazo.very productive wewe una pesa,...Mimi ndo nitalisimamia na biashara itaenda vizur kwa sababu ujuzi na uzoefu wa hiyo biashara.(makubaliano ya kisheria tutaweka ili kulindana na kuaminiana)
Kamwe usikubali kuweka fixed accouts hiyo pesa yote mkuu, itakuwa ni uoga na ufinyu wa maarifa sana hata kama unazo nyingi hizo million 200 ila bado kuna namna ya kuzizalisha zaidi. Usibweteke ukasema unazo nyingi ukaanza kufanya biashara ya mwendo wa kinyonga, hakuna tajiri duniani ametajirika kwa kwa savings accounts au hizo fixed accounts, matajiri wote wanafanya investments.
Hizo million 100 utakazoweka fixed accounts ni kwa tahadhari tu kuwa biashara ikishashika mizizi unaongeza mtaji kwemye biashara kutoka fixed accounts ndo watu wenye jicho la tatu wanavyofanya.
Bahati nzuri biashara zote hizo juu nilizo kuorodheshea nina ujuzi nazo na zingine nazifanya...ukiacha hati fungani ndo sijawahi kufanya, kwa hiyo wewe kama uko tayari fanya hayo niliyokushauri, ingawa ushauri sio lazima ufatwe.
Najua watu wana pesa ila hawana mawazo ya biashara au wanaogopa kufanya biashara. Wenye pesa za mitaji msiogope kufanya biashara frankly speaking mimi nipo nitakushauri, mwanzo hadi mwisho kwenye biashara yako kama ukinikaribisha niwe mshauri wako usitishwe na watu waoga wa kuthubutu.
Dunia ya sasa inataka taarifa sahihi ndo muhimu sio uoga na hadithi za kukatisha watu tamaa.
Ni hayo tu Mkuu wa million 200/= karibu sana kwa ushauri na vitu kama hivyo.
dylm.mashauri@gmail.com 0762742349
Sent using Jamii Forums mobile app
================
Tafadhali Kimla soma Ushauri kwa wastaafu na wanaopata hela nyingi kwa mkupuo - JamiiForums