Duh! Mkuu utakuwa ushawahi kutapeliwa kwa njia hii ndo maana umekuja kunituhumu moja kwa moja? Au ni zile story za kijiwe cha kahawa?
Nimetoa email na namba za simu zangu tena ambazo ni mawasiliano ninayoyatumia kila siku zaidi ya miaka kumi sasa,hapo kweli tapeli anaweza kufanya hivyo?
OK,nimetoa ushauri wangu kwa mdau,na baadae nami nikatoe namna ambavyo ninaweza kutoa mchango wa utaalamu na maarifa nilionao kwenye ujasiriamali na biashara kwa ujumla.sasa namtapeli vipi?
Mkuu,sio watu wote ni matapeli,..na tujifunze kuwa kila mtu ana kitu ambacho mwingine hana, mtu unaweza ukawa na wazo la biashara ila ukawa huna fedha,ukawa na wazo pamoja na pesa ukawa huna muda ikabidi utafute Watu,ndo concept ya ajira ilianzia hapo,..ukawa na wazo,fedha,muda ila utahitaji Watu wa kufanya nao kazi...ili kufanikisha lengo lako.
Unaweza ukaona chain hyo inavyoenda,..huwezi kufanya biashara na ikafanikiwa kwa kiwango KIKUBWA kwa kutegemea ndugu wa damu pekee,.utahitaji tu watu usiowajua kabisa watakuja kukusaidia kwenye biashara au Kazi zako ili usonge mbele zaidi.
Mo angeamini ndugu zake wa damu tu ndo wawe washauri wake kwenye biashara sidhan kama angefika hapo alipo the same applied kwa Bakheresa,Patel,kusaga,manji,rostam na wengine wengi.
Watanzania kama kweli tunataka kusonga mbele kiuchumi hasa financial freedom,hatuna budi kutafuta maarifa kupitia kujifunza kwa watu,kusoma vitabu,na kuwa na mtandao wa watu wenye maarifa kuhusu hiyo Kazi,biashara au ujasiriamali wako.hao watu asilimia kubwa hawatakuwa ndugu zako wa damu.(lazima hilo ulikubali).
Hapa jukwaani kuna watu wamenufaika sana kupitia maarifa yanayotolewa humu,..watu wamenufaika kwa kushirikiana kufanya biashara,kupeana ujuzi na maarifa mbalimbali kwa kuonana mubashara,,watu wameanzisha kampuni za pamoja,urafiki wa kweli n.k kupitia hapa jamiiforum.
Sasa imefika wakati lazima hizo negative mentality tuziondoke kichwani mwetu,tuwe wadadisi zaidi,tuwe na big opened mind,tukubali kushirikishana wenye pesa zao,washirikiane na wenye mawazo,wenye muda nao pia watafute wenye pesa na mawazo ili waweze kufanya kitu kwa pamoja hatimaye kushinda huu adui umasikini ambazo chanzo chake ni ujinga,(yaani kukosa maarifa sahihi kwa wakati sahihi na kwa jambo sahihi).
MKUU NAKUSAMEHE BURE KWA KUNITUHUMU NA KUNIDHANIA KUWA NI TAPELI,NIMEKUSAMEHE KWA HIZO TUHUMA ZAKO.
email na namba zangu nilishatoa,mwenye kiu na uamuzi wa dhati kushirikiana hasa kupata ushauri
wa biashara, ujasiriamali na maarifa mbalimbali kuhusu financial freedom.
karibu.
It seems impossible until it's done.(nelson mandela)