Nina Tsh. milioni 200, niweke benki gani yenye 'Fixed Interest' nzuri?

Weka benki robo ya pesa , nyingine zungusha kwenye biashara , ama vipi wekeza kwenye ardhi . Ardhi ni benki inayozalisha sana ili mradi ardhi isiwe na mgogoro . Nilinunua kiwanja miaka 5 iliyopita kwa 4m leo nauza 8m na mteja yupo !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu safi sana, hujakumbatia ujuzi na maarifa yako. Hongera!!!
 
Amepewa alternative tu, uamuzi ni wake. Pamoja na kuwa yeye ni mwoga wa biashara au hajawahi kufanya biashara yoyote, ni vizuri kuangalia options zote maana kuweka hela bank kwa kisingizio cha security ya 100% ni kujinyima fursa ambazo kwa maoni yangu yeye(mleta mada) tayari anazo.

As long as kiasi fulani ana-fix bank, say 50% ya pesa zake, hizo 50% aingie nazo mtaani afanye investments aamgalie vitu kama hati fungani, shares kwenye makampuni makubwa hazitamtupa hasa kama atakuwa anatafuta elimu na kujua zaidi, sasa iliyobaki ndio awekeze kwenye eneo la interest yake.

Hawezi kuanguka kote huko mkuu. Tusiwe waoga.
 
interest rate ya fixed deposit sasa hivi inacheza kuanzia 6% kwa mwaka kwa mabenki mengi. kwa hiyo pesa yako unaweza kunegotiate ikapanda panda mpaka 7-8%, kwa mwaka.
 
nyie watu embu eleweni uzi! mtu ameuliza bank yenye fixed interest nzuri... nyie mnajitia ujuaji mwingi na washauri wakuu kwenye mipango na matumizi

kama ujaelewa swali tulia! sio kumwaga upupu usio msaidia mtoa mada
 
ok, utawekalini na wapi?
Nafikiri naweza hata kukutafuta moja kwa moja. Nilitazamia ndani ya siku 20 nione timu ninayoitafuta itakuwa imepatikana, all in all naweza kukupa move ilivyo.
 
Mkuu katika biashara ya kukopa fedha karibu watu wote wanaokwenda kukopa ni waaminifu sana na wanakuwa wameshapiga mahesabu ya biashara zao na kujua namna watakalivyolipa deni. Hilo ondoa mashaka nalo. Tatizo kubwa lipo kwenye maendeleo ya biashara inayomfanya akope.... je itaenda kama alivyopanga? Mara nyingi kabisa plan za biashara haziendi sawa na matarajio! eg: Kama ulivyosema anaweza akatokea huyo mama mwaminifu sana akakopa fedha, laki tano, akitegemea kufungua Mpesa na kurudisha kila wiki.Biashara ikanza vizuri sana lakini baada ya mwezi akaja tapeli akakomba msingi wake wote... au kama ni mama ntilie, ikaja corona virus karantiini na mtaji wote ukapotea... Kwa kifupi nataka kukumbusha kuwa kinachofanya watu wasilipe madeni mara nyingi siyo kukosa uaminifu!
 
Acha kabisa ndugu uko sahihi.
 
Dah kwel.maisha kitendawili nahangaika kupata laki 5 mwez wa 3 huu kwa ajil ya mtaji wa mafuta tu nianze biashara...mtu ana 200m[emoji1487][emoji1487][emoji1487][emoji1487]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau, nina 200 million TZS, je niweke fixed account benk ipi yenye interest nzuri ya mwaka?
Asante

Michango

==========



================

Tafadhali Kimla soma Ushauri kwa wastaafu na wanaopata hela nyingi kwa mkupuo - JamiiForums
Nilikuwa nafuatilia suala kama lako miezi miwili imepita yaani kabla huu ugonjwa ( corona ) haujashika kasi duniani niliambiwa kuwa rate zinatofautiana kutoka na muda utaoweka mfano ikiwa ni miaka miwili rate ni tofauti na mwaka mmoja, niliambiwa postal bank wanatoa 7% kwa mwaka na 9% kwa miaka miwili ukianzia 100m na bank nyingine niliambiwa BankABC wanatoa asililimia 10 % kwa mwaka mpaka 11% kwa sasa sjui hali ikoje maana corona imevuruga kila kitu.

Wadau walinishauri pia bank mpya zina risk ikifilisika inachukua mda kupata pesa yako na inaweza kupotea kabisa ila wakashauri bank kongwe kama NMB, CRDB na Postal bank
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…