Nina Tshs 150,000/= nifanye kitu gani ili niizalishe?

Nina Tshs 150,000/= nifanye kitu gani ili niizalishe?

Anza na kuchoma maandazi na tangawizi...baada ya miaka 50 utakuwa kama Bakhresa....
 
Hivi hapa leo ni JamiiForums kweli?
Mbona jukwaa limejaa dhihaka sana, mtu ana shida watu wanamdhihaki?

Nakushauri kama uko DSM nunua nguo peleka sehemu za ndani ndani huko kama wilaya ya Kisarawe, pia viatu vinauzika hasa vya wanawake kama sendo
 
Usikatishwe tamaa na hizi kejeli za humu jf, hao matajili hawakuanza na milioni kama wewe kuna walio anzia chini ya hiyo ela uliyo nayo na wakafanikiwa, tatizo tulio wengi tunataka mafanikio ya mda mfupi na tunataka kuanzia juu, ukianzia chini unapanda juu ndo biashara yako itadumu mda mrefu.ukiamua kuwa mjasiliamali mambo ya statas weka pembeni,statas itajileta yenyewe kadri unavopata mafanikio
 
Nunua chenji chenji bank uende kuuza kwenye vituo vya daladala,katika hiyo 150k ukiuza zote kwa siku unaingiza faida ya elfu 30.
 
Nunua mkokoteni, nenda kwenye mitaa ambayo kuna tatizo la uzoaji taka, fanya kazi ya kuzoa taka mara moja kwa wiki kwa kila nyumba wakulipe 2,000 utapiga hesabu mwenyewe. Baada ya muda utaongeza mikokoteni na kuajiri watu, baadae hata kufungua kampuni.
 
hiyo hela bado unayo au umeenda kujiuliza viti virefu?
 
Usikatishwe tamaa na hizi kejeli za humu jf, hao matajili hawakuanza na milioni kama wewe kuna walio anzia chini ya hiyo ela uliyo nayo na wakafanikiwa, tatizo tulio wengi tunataka mafanikio ya mda mfupi na tunataka kuanzia juu, ukianzia chini unapanda juu ndo biashara yako itadumu mda mrefu.ukiamua kuwa mjasiliamali mambo ya statas weka pembeni,statas itajileta yenyewe kadri unavopata
mafanikio

Bado hujampa ushauri anaoutaka,acha porojo.
 
Mkuu ngoja nikupe ushauri mdogo na mzuri ambao utakuza pesa yako kwa mda mfupi:
Mimi ni mfugaji wa kwale njoo nikuuzie tray 10 for 15,000 each itakuwa 150,000/ then utaenda kuuza kwenye super market for 20,000/ per tray au direct kwa watu for 30,000/ per tray then hera yako itakuwa imerudi + faida
 
Back
Top Bottom