Nina uhusiano na mke wa mtu. Natamani kumuacha lakini inakuwa ngumu

Mkuu mimi sijakuhukumu
Nimetoa mawazo yangu hasa kwenye dhana nzima ya heshima ya ndoa na kuchepuka
Mchepuko wako ameolewa halafu ukimchunia anahamia kwa mamake huoni ni tatizo??

Unajua una muda gani kabla hiyo ndoa yako unayoilinda haijaharibika huku ushaharibu ya mwenzako??
Fanya maamuzi sahihi mapema kabla hujaharibu kotekote.
 
Samahani naomba nikuulize jambo, huyo binti ni kabila gani maana tunaweza kutafuta mchawi kumbe pia na kabila nalo huwa ni culture yao hiyo na mama yake ni kabila gni ,maana kuna kabila ambazo wao ndoa nikutoa mkosi lakini mapenzi ni jadi kwao ,
 
Mkeo sisi ndo tunamla
 

Ushauri mzuri sana, kutamka neno muache ni rahisi, lakini kama ulishakua kwenye situation hiyo utaelewa ugumu wake. Wanawake wengi hawana furaha kwenye ndoa zao, wanalazimika kutafuta hizo furaha kwa watu wanaowapenda zaidi.
Labda cha kusahihisha hapo kwenye ushauri wako, hahitaji KUMFOSI, mke wa mtu akikupenda anakusikiliza na kukutii zaidi ya mtu mwingine yeyote, hapo amwambie tu kistaarabu kuwa anahitaji kumfanyia hayo Mumewe ili yeye aendelee kuwa nae. Kama mwanamke akizingatia haya, ipo siku mmewe atamtafuta jamaa kumshukuru kwa kurejesha furaha kwenye ndoa yao.
 
Haya makabila hapana aisee...
 
Naona kila anayekwambia usichotaka kukisikia unamuona anajifanya mtakatifu. Sasa sijui ulitegemea ukileta uzi wako tukupongeze?. Unachokifanya ni upumbavu; utakuja ufe kiboya umuache mkeo analia kwa aibu. We are not judging you; ila tunakusaidia. Hakuna mtakatifu humu; ila kila mmoja akikosea ataaambiwa na sio kutiwa moyo afanye anachokitaka kisa tu hakuna msafi kati yetu. Muheshimu Mungu, muheshimu mkeo na watoto wenu.
Sitakuwa wa kwanza kugongewa na hili mm halinisumbui. Kwa sababu kuna siri nyingi kwenye ndoa,ndo maana watu wote hapa kwa sababu mm nimesema wamegeuka watakatifu.
 
Yaani unaleta hii dhambi yako humu siku hii ya Ijumaa kuu badala ya kwenda kutubu kanisani. N way inaonyesha wewe na huyo kijana aliyomuoa huyo binti wote mmerogwa. Mpaka ulete hapa hili inaonyesha hutaki na huna mpango Wa kumuacha na badala yake umetaka tu kutujulisha unavyopendwa na mke Wa mtu. Ila jisaidie sana ujinasue ikiwezekana shirikisha na ndugu yako hata mmoja Wa karibu na mnayeheshimiana na unayeamini ana busara sana ili muwe karibu ktk hili na omba sana Mungu akupe ujasiri Wa kujinasua manake kuna hatari kubwa yaja kwako na familia yako. Mana naamini huyo kijana ana ndugu,jamaa na marafiki na kama ni kweli anajua basi jua atachukua ushauri huko kwote juu ya nn cha kufanya,sasa atachukua ushauri gani ndio hujui,sijui.
NB: BINADAMU NI KIUMBE CHENYE ROHO NGUMU NA HATARI KULIKO WANYAMA WENGINE WOTE!
 
Pole sana aisee, mke wa mtu ni sumu... siku wa kwako akiibwa na akamegwa utajua uchungu wake....

ANZA VISA VIDOGO VIDOGO...PUNGUZA NAE MAWASILIANO HUENDA IKASAIDIA...MDANGANYE SIKU MOJA MOJA ASIWE ANAKUFUATILIA SANA
Unajisumbua tu jamaa hatofanya hivyo mana keshasema amejaribu kumuacha anashindwa,sasa hivyo visa ataanzia wapi huyu muhuni?
 
Mkuu nadhani kinachokufanya unione wa ajabu ni tofauti zetu za namna ya kufikiri na kuamua. Kwanza sijachukia kuambiwa ukweli,lkn kunishambulia kunisaidia nn!?? Kinachokupa nguvu ya kunisema ni kwa sababu mimi ndo nimeweka wazi kosa langu. Sasa kuna haja gani ya kuniambia tena kuhusu kosa lilelile ambalo mm ndo nalijutia!?? Kwa nn usinipe suluhisho tu la moja kwa moja!?? Mm nimeleta hapa kupata mawazo mapya siyo!?? Sasa kuanza kuni-attack kwa kitu ambacho me ndo nimekitengeneza kunanisaidia nn!?? Me nataka msaada wa kutoka siyo kunielezea kuhusu ubaya wa hilo tukio. Hicho ndo nakataa,na nna kataa kwa sababu naamini hakuna mtakatifu. Hakuna ushauri niliopingana nao,na ntachukua hatua. Hv nnavyoandika hapa,yy mwenyewe nimemtumia link asome na anapiga simu hapa sipokei kwa sababu me bado nipo nyumbani. Ntaongea naye nikifika kwao. Yupo kwao kwa mama yake tangu jana,ndo nataka nikaongee nao pamoja na mama...!! Nna member wa hapa na ni jinsia ya kike namsubiri anakuja tunaenda naye huko. Huyu member tunafahamiana na tunaheshimiana sana nje ya keyboard. Alijua labda nimeleta chai,lkn ameona umuhimu na kaniambia atakuja leo aongee na huyo dada,now yupo njiani namsubiri afike tupate chai twende huko. Ndo hivyo mkuu sichukii ushauri,lkn kuniambia kuhusu huo ubaya ni kupoteza muda kwa sababu me pia najua nafanya vibaya na athari zake nazifahamu ndo maana nataka msaada wa kutoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…