Alikuwa anatafuta support ila kaambulia spana za utosi! Mwanamke wa kuoa ni A huyo B ni wa kuendelea kumchakata kwa siri kama hataki ampige chini tu 😂😂😂 ila mke ni AWewe unaacha msichana wa maana kwa sababu za kipuuzi
Nitarajia useme huyo A unamuoa lini?
Kwa jinsi navyoona mimi wewe unaruka mkojo unakaja kinyesi.
Kwenye uzi wako unajaribu kuonyesha huyo B ndo sahihi lakini ukweli upo pale pale mwanamke wa kuoa ni huyo A sasa wewe mchukulie poa tu kisa umedumu nae mda mrefu basi unamuona fara sio sahihi
Jichanganye kwa hiyo B utaleta mrejesho soon humu.
Unamponza dogo wehOa huyo mdogo huyo mnayelingana umri akizaa Mara mbili utamchukia bure atazeeka ghafla loh.
Huyu jamaa mwehu kweli yani wanaume wanakataaga pepo wenyewe wanakimbilia moto wa duniani 😂😂😂Yan umedumu na mtoto wa watu kwa miaka mitano mkasomana tabia na ukamuona anakufaa,leo hii unaona bora huyo mwanachuo ambae hata nyendo zake huzijui?
Na kama tokea awali ulikua na malengo ya kuoa mtu wa kabila lako hukujua A sio kabila lako?
Kuhusu changamoto ya maumbile ya miguu nadhani uliijua mwanzon kabisa wa mahusiano yenu,sijui ulikua wapi kukosoa Leo hii umepata mwanachuo ndo unaanza kuyaona hayo.
Pia suala la umri wako na A haukuujua mapema?Kua makini unaeza jikuta unawapoteza wote.Hadi sasa A akipata mwingne anaeeleweka na mwenye mtizamo chanya atamkubalia mana ameshakata tamaa na wewe kwa vitendo vyako.
Then umekiri A alikuvumilia tokea enzi huna kazi ad leo.Huoni huyo ni mwanamke mvumilivu?Pia hakutegemei ni mpaka wewe uamue kumpa mwenyewe.Napo mkipata tegemezi mnanungunika.sasa uko upande gan yan hueleweki
Eeh yani kiwanja cha mazoezi ndio anataka aporomoshee ghorofa ajiwekeze mazima😅 kuna fuse haiko sawa mahali!Jamaa mwanamke wakugegedanyeye anataka amfanye mke🤣🤣🤣🤣
Makurubembe yanakutia spana hadi unarudisha majeshi nyuma😅 ukipata mwanamke anayekupenda unakitulizaDaaa Aiseee Kwa akili hizo broo hutoboi et umwache A Kwa sababu za kipuuzi tu aaaaa weee
Mimi Nina N wangu tupo kwenye relationship for 6 years since old school anauvumilivu sana she deserves to be my queen nimekutana na makuru membe kibao ndani ya mwezi tu nikaona mbele kiama Bora nirejeshe majeshi now nimetulia tu namsubiria N wangu awe future wife
Amini nakwambia mwana kuli find mwana kuli get!
Atalia na kusaga meno,, anatupa dhahabu kwa vipande vya chupaWe jamaa unakwenda kwenye uzee lakini bado unajiona kama uko kwenye 17. Bado hisia na matamanio vinakuendesha. Huna upendo wowote kwa B. Ila nguvu ya tamaa ñdiyo inayokusukuma kumuona A hafai. Wanaume wenzako uwa wanatambua kutofautisha upendo na tamaa. Ukiruhusu A kuondoka, utajuta maisha yako yoooooooote. Wale wanaosimuliaga wamepoteza dhahabu na kuchukua jiwe ndio wewe.
Umeyumba tena umeyumba vibaya mno. Unalo litafuta utalipata muda si mrefu.Habari zenu ndugu zangu.
Nakuja kwenu na Id mpya ili niweze kuwa muwazi kwenu nipate msaada. Naona karma inaninyemelea na sielewi nifanye nini ndugu zangu.
Mimi ni kijana wa miaka 31. Sijaoa lakini nimekuwa na girflriend wengi kwa wakati mmoja bila wao kujuana.
Shida yangu ni hii: Katika wasichana wote niliowahi kuwa nao, kuna huyu msichana A. Kwa kweli tumekaa naye kwenye mahusiano zaidi ya miaka 5. Tangu nikiwa chuo. Msichana huyu sijapishana naye umri sana. Nimemzidi kwa miezi kadhaa. Ila amekuwa akiniheshimu kwa muda mrefu, akinijali tangu sina kazi hadi sasa.
Ila niseme ukweli ndugu zangu. Huyu msichana kwanza mguu wake mmoja ni mfupi mwingine ni mrefu, hivyo anakuwa kama anachechemea fulani. Licha ya hayo mapungufu ya kimaumbile, ni mtu mwenye elimu yake, mzuri sana (kwa macho yangu), hanitegemei kwa chochote hadi pale mimi ninapoamua kumnunulia kitu au kumtoa out. Otherwise hata mimi muda mwingine ananipiga tafu.
Shida ni kwamba sasa nimepata mtu mwingine ambaye nahisi tunaweza kuendana zaidi ya A. Ingawa simjui vema msichana huyu maana ni mwanafunzi wa chuo ambaye nimemzidi miaka zaidi ya 7. Tupo mikoa tofauti. Yeye ni tegemezi kwangu kwa kila kitu. Na kiukweli mara nyingi tunagombana sana na tumeshaachana mara kwa mara sababu ya huyu msichana A ambaye naye imefikia hatua kuwa sasa nichague jambo moja. Kumuacha ama kuendelea naye pasipo mimi kuwa na wasichana wengine. Jambo ambalo kwangu ni gumu sana.
Nimejaribu mara kadhaa kuongea na A na at the same time nakuwa na B kwa simu. Jambo ambalo A amekuwa mkali na sasa ninashindwa kuwa huru hata kuongea na B.
Kiukweli B naona ni msichana mdogo na pia kabila letu ni moja hivyo ninapata amani sana kuwa nitaweza kuwa na huyu binti kuliko kuwa na A. B anamaliza masomo mwaka huu na tunategemea mwakani tuanze safari ya kukaa karibu ili kujuana na hàtimaye tufunge ndoa.
Migogoro hii kwangu imekuwa kero na nimemtamkia maneno mabaya sana A ambaye amekata tamaa nami kabisa. Hanipigii tena simu na kiukweli najihisi kama nipo mwenyewe inspotokea ninapata changamoto fulani.
Naombeni ushauri wenu wadau. Je nipo sawa ama nimeyumba?
Ila mademu wa Chuo si wakuwawekee plan kabisaaaaNimekoma kusoma hapo kwa mschana wa pili uliposema tuu, ni Mwanachuo.
Mwanachuo sio mtu wa kumuamini, uwezekano wa kubadirika huko mbele ni mkubwa. Usikute umri wake bado ni under 25.
Oa huyo mdada unaemzidi miezi tuu.
Halafu usikute huyo denti, una msomesha kwa namna moja au nyingine.
Ule mswaki wameutumia sana eehh? Unaweka mswaki mmoja kila MTU akija anautumia halafu inajenga confidence kwao sanaSijaoa lakini nimekuwa na girflriend wengi kwa wakati mmoja bila wao kujuana.
Wakilingana umri mke stawahi kuzeeka akizaa bana. At least kuwe na age differenceUnamponza dogo weh
Hahahahahah mke akizeeka haina shida hamna ambaye hataazeeka hio tabia ya age difference ndio mnakuja kutesa wazee na michepuko yenu viben 10 bora wote damu zipoe pamoja sio mmoja damu baridi mwengine bado ana joto!Wakilingana umri mke stawahi kuzeeka akizaa bana. At least kuwe na age difference
kweli mkuu yaani nimepata bahati ya kua na msichana mtulivu sana sana Katika kizazi hiki ni wachache sana Kuna muda hua najaribu kutest mizinga ya nyuki hua naambulia manundu natoka ndukiMakurubembe yanakutia spana hadi unarudisha majeshi nyuma😅 ukipata mwanamke anayekupenda unakituliza
Habari zenu ndugu zangu.