Nina wasiwasi na hii Gari, ushauri wenu

Nina wasiwasi na hii Gari, ushauri wenu

INSIDER MAN

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2018
Posts
2,005
Reaction score
19,579
Habari za usiku wataalam

Jaman mimi nasema ukweli kwenye magari bado ni mshamba nilijichanga changa nikanunua gari ya kunisadia mishe za hapa na pale ni Toyota IST, gari naweza sema bado ni mbichi ina kama miezi 3.

Hili jukwaa limekua na msaada sana kwangu napata elimu sana kuhusu magari. Ndugu zangu nina week nimefanya service ya gari hii service ya2 baada ya kuagza gari. Service ya kwanza nilitumia oil ya total quartz.

Service ya pili niliamua kubadili oil na kutumia Lique Molly baada ya kuona watu wanaisifia sana, wakati tunabadili filter tuligundua wale jamaa wa mwanzo hawakubadili filter so walinipiga hela ya filter.

Kwenye service ya2 mafundi walishauri nisafishe engine kwa kutumia engine flush ili kutoa uchafu, na nikafanya service ya oil ya gear box ambapo tulitumia T-IV fundi alikagua akasema gari haijafanyiwa service kwenye gearbox hivo nibadli oil.

Tuje kwa mada, baada ya service kuna kitu naona hakipo sawa kwa kawaida gari ikiwashwa lazma itoe moshi fulani hivi wa mbali ila sahivi sioni kingine wakati fundi kafanya service aliitest gari kuna maji meupe matone yalikua yana dondoka kwenye bomba la moshi nilivomuuliza fundi akasema hapo engine ipo sawa nisiwe na wasiwasi ila sahvi sion kabisa yakidondoka.

Gari ile rpm haivuki mbili hta wakati inatoka japan ilikua hivohvo ikifika3 inarud mpaka2 au chini ya 2, kingine ukiwasha rpm haizid moja au inakua nusu.

Kutokutoa moshi na maji ndo kunanichanganya kwasababu najua moshi ni matokeo ya kuwa mafuta yamechomwa na ni ule ni uchafu, nisaidieni wataalamu wa magari.
 
Hilo la kutokutoa moshi ni dalili nzuri kuwa engine iko vizuri.

Moshi huwa unaashiria engine ina matatizo sometimes baadhi ya engine parts zinakuwa zimechoka.

Gari inayotoa moshi sana na mngurumo usio wa kawaida mara nyingi inahitaji engine overhaul
 
Habari za usiku wataalam

Jaman mimi nasema ukweli kwenye magari bado ni mshamba nilijichanga changa nikanunua gari ya kunisadia mishe za hapa na pale ni Toyota ist, gari naweza sema bado ni mbichi ina kama miezi 3.

Hili jukwaa limekua na msaada sana kwangu napata elimu sana kuhusu magari. Ndugu zangu nina week nimefanya service ya gari hii service ya2 baada ya kuagza gari. Service ya kwanza nilitumia oil ya total quartz.

Service ya pili niliamua kubadili oil na kutumia lique molly baada ya kuona watu wanaisifia sana, wkt tunabadili filter tuligundua wale jamaa wa mwanzo hawakubadili filter so walinipiga hela ya filter.

Kwenye service ya2 mafundi walishauri nisafishe engine kwa kutumia engine flush ili kutoa uchafu, na nikafanya service ya oil ya gear box ambapo tulitumia T-IV fundi alikagua akasema gari haijafanyiwa service kwenye gearbox hivo nibadli oil.

Tuje kwa mada, baada ya service kuna kitu naona hakipo sawa kwa kawaida gari ikiwashwa lazma itoe moshi flan hivi wa mbali ila sahivi sioni kingine wakati fundi kafanya service aliitest gari kuna maji meupe matone yalikua yana dondoka kwenye bomba la moshi nilivomuuliza fundi akasema hapo engine ipo sawa nisiwe na wasiwasi ila sahvi sion kabisa yakidondoka.

Gari ile rpm haivuki mbili hta wakati inatoka japan ilikua hivohvo ikifika3 inarud mpaka2 au chini ya 2, kingine ukiwasha rpm haizid moja au inakua nusu.

Kutokutoa moshi na maji ndo kunanichanganya kwasababu najua moshi ni matokeo ya kuwa mafuta yamechomwa na ni ule ni uchafu, nisaidieni wataalamu wa magari.

Gari ikiwa kwenye parking ukakanyaga accelerator bado Rpm haivuki 3?
 
Naomba kukuuliza swali kabla ya kujua nicomment nn hasa ulipokuwa watumia oil ya kwanza kitu gan uliona changamoto hadi uhamie ktk oil ya pili?

swali langu jingne kpi kilikupelekea badiri gearbox oil kulikuwa na changamoto gan hadi uchange gear box oil?

ulifrush engine sawa haina shida je aliweza funga components zote ktk standard ile ile? nikupata muongozo hapo naweza pata cha kuongea zaidi
 
Wakuu Nina 5M ila nataka niongezee zifike walau 6M or 7M hapa naweza pata gari ya aina gani?
kwa ushauri tu fanya kwanza research wahitaji gari kwa matumizi gani na gari gani waweza afford kulingana na kipato chako kuanzia operations hadi maintainance swala la kuwa na bughet lisiwe kigezo cha kuchagua gari itaweza kucost mbeleni ktk matunzo
 
Naomba kukuuliza swali kabla ya kujua nicomment nn hasa ulipokuwa watumia oil ya kwanza kitu gan uliona changamoto hadi uhamie ktk oil ya pili?

swali langu jingne kpi kilikupelekea badiri gearbox oil kulikuwa na changamoto gan hadi uchange gear box oil?

ulifrush engine sawa haina shida je aliweza funga components zote ktk standard ile ile? nikupata muongozo hapo naweza pata cha kuongea zaidi
Umeuliza maswali konk sana.
 
Kuflush engine sio lazma engine ifunguliwe, anayosemea jamaa itakua ipo kwenye kopo kabla hujamwaga oil anamimina so ni kama mvuke inasafisha engine uchafu wote kama kuna oil iligandia gandia inasafisha hii ni kitu nzuri sana hakuna oil inayobaki, baada ya dk15 ndo anamwaga oil utaona uchafu unavotoka.

Gari nyingi ukinunua below 70,000 km nyingi hazijafanyiwa service ya gearbox hasa kwa kubadili oil ni vema kama hujanunuq gari fatilia service ya gari ilifanyiwa upande gani na kipi hakufanya, wengi sana hili hatufatiliii gari ikifika unawaza kuendesha.

Lique molly ni oil nzuri sana hata mm natumia hii oil yangu ya kwanza niliweka castrol ila nilivoingia huku naona gari ipo poa sana.

Nimesoma vzr maelezo ya jamaa amesema ni mshamba kwenye magari amesema ukweli, ila jamaa gari yake inaonesha ni nzima haina shida ana wasiwasi au wenge tuseme .
 
Wakuu Nina 5M ila nataka niongezee zifike walau 6M or 7M hapa naweza pata gari ya aina gani?
Mkuu kama unaweza kusubiri mpka upate hela ya kutosha kuagiza bora ufanye hivyo, gari za mkononi nyingi majanga na kama ndo gari ya kwanza kumiliki kushikishwa kimeo ni rahisi sana.
 
Sasa gearbox ilikuwa na tatizo gani?

Yaani Mechanics wetu kama wauguzi tu tofauti mmoja anatumia visu na mikasi na mwingine nyundo na [emoji373]
Sijawahi kubadili oil ya gearbox hapo ndio utata umeanza
Yaani unasema gari bado nzuri halafu makanjanja wa kwanza wakakupiga filter na hawa wanaojifanya waungwana ndio kabisa
 
Back
Top Bottom