Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umekosea sana wewe ndo kichwa cha familia iweje mke akurupuliwe kama ngedere na wewe ukubali au huyo mke kakuoa wewe.Hapana mkuu huwa naamua lakini hii sikutaka ku doubt coz nikimkataliga safar analalamika na kuona namuonea lakini pia nikwasababu tu kaeleza kuwa kaitwa na hajui nini shida kwa heshima tu za mashemeji nikamuacha aende ili akirud anieleze vizur hicho kilichomfanya akaitwa huko
Mi naamini hakuna kibaya coz angetaka kuliwa angeliwa bila hata kukupa hizo sababu ambazo hata mtoto anashtuka ila jiwekee negative thinking coz itakufanya ukubaliane na ukweli hata kama unauma when things changes, if Possible Mwambie akuelezee shida iliyompeleka coz wewe ni mumewe why usijue..akipata kigugumizi itabidi ukubali mojaxmoja pia jitahid ujue Why Dodoma?Sawa mkuu lakini nitajua tu coz najua pakumkamatia shukrani mkuu
Ila uache uzwazwa, wana shida na mkeo wwakupigie wewe kumuombea ruhusa,safari ya kindezi kama hizo kwako full stop.Shukrani mkuu
Umekosea sana wewe ndo kichwa cha familia iweje mke akurupuliwe kama ngedere na wewe ukubali au huyo mke kakuoa wewe.
Simama kama mwanaume mzee usichukulie mambo kama mvulana safari yoyote mwanamke inatakiwa akuombe ruksa mwezi au week mbili kabla,usichukulie vitu kama hivyo kirahisi.
Kama kuna tatizo kwao inatakiwa wazazi wake wakuombe wewe umruhusu wewe maana yupo chini ya himaya yako.
Mwisho nasikitika kwa kutosimamia ndoa yako vizuri kwa kuwa na misimamo dhaifu.
Stress gani tenaMkuu huu ushauri wakibabe usingetoa utatuongezea stress.
Mi naamini hakuna kibaya coz angetaka kuliwa angeliwa bila hata kukupa hizo sababu ambazo hata mtoto anashtuka ila jiwekee negative thinking coz itakufanya ukubaliane na ukweli hata kama unauma when things changes, if Possible Mwambie akuelezee shida iliyompeleka coz wewe ni mumewe why usijue..akipata kigugumizi itabidi ukubali mojaxmoja pia jitahid ujue Why Dodoma?
Dodoma inasingiziwa sana siku hizi... Pole mkuu... Pambana tu na hali. Kumbuka huyo ni mkeo na wewe ndo kichwa wa nyumba, wewe ndo wa kutoa miongozo.Habar wana JF
Naimani mko wazima
Kiukweli nimekuwa na wasiwasi na safari ya wife sjui Kwanini lakini nisafar ambayo siielew kabsa wakuu nina mashaka nayo coz naona mapicha picha tu.
Nikwamba wife kasafiri juzi ijumaa kuelekea Singida lakini safari yake sielewi elewi kabsa kwasabubu kwanza nisafari ya kushtukiza lakini pia mbaka now sielew aimed ya safari ni nini mbaka now.
Alhamisi nimelud kutoka kazini usiku tunalala ndo ananipa taarifa ya kuwa kesho ijumaa anasafiri nikamuuliza unaenda wap? akaniambia kapigiwa Sim na dadazake wamemuita ambao wanakaa singida nikamuuliza kunatatizo akasema hapana ila sijui wanashidagani na mimi ndo wamenipigia cm niende Kiukweli nilikuwa nimechoka nahtaji kupumzika sikutaka ku complicate kitu nikamjibu sawa nikalala then asubuh nikajiandaa nikaenda kazini vizur.
Niko Job ananipigia Cm kuwa ndo anatoka home anaelekea stend kupanda Bus ilikuwa almost kama saa 7 hivi mchana nikamjibu hayaa na nikamuuliza kama kunakitu chochote anahtaji akasema hapana yuko powa bas nikakata Cm lakini kiukweli ghafra akiliyangu ilishikwa na wasiwasi juu ya safari yake but sikutaka ku doubt anything nikapotezea.
Baadaya kupita kama lisaa akantumia message kuwa amepata bus but akifika Dodoma atashuka kuna ndugu yake anamchuka then wanaenda wote daah sikutaka pia ku doubt wala mambomengi nikamjibu sawa nikaachana nae nikaendelea na kazi zangu but bado sikuona sababu ya yeye kushuka Dodoma By saa 2 ndo ananiambia ndo wanaondoka Dodoma nikamjibu sawa safari njema tukaacha hivyo.
Bas mi nikarud home usiku kwakuwa nilishapita somewhere nikapata chakula nikafika home niko good nikaoga nikaingia kwa bed nikampigia ananiambia kashafika ila kachoka na safari nikamuacha nikapumzika.
Sasa leo Jpili tumeongea asubuh vizur tu na tukaagana badae by saa 7 mchana ananiambia ndo anataka kurud leo nikamuuliza mbona hukuniambia asubuh na kwanini usingeondoka asubh sijaona cha maana anachonijibu bas nikamwambia hayaa kama unarud leo tuakaacha baada ya kama nusu saa ananipigia cm ananiambia kuwa yupo stend mala gari sjui hakuna mala zimejaa mala nimechoka naskia usingizi nikamwambia sasa siungebaki ili uondoke kesho asubuh akasema sawa tukaacha.
Baadae ananitumia message et amepata gari ila linaishia Dodoma kwaiyo atashuka Dodoma aloo nikasema kimoyomoyo hapo Dodoma hapo siobule coz kwenda kashuka Dodoma kurud baada alud kesho kama kweli kakosa usafiri na tumekubalina anarud kesho mapema na sizan kama kweli alikosa usafiri by dat time ananiambia kuwa kapata usafiri ila unaishia Dodoma so ataenda kulala dom sikutaka ku complicate nika mjibu sawa bhas nikaachana nae.
Ila chaajabu baada ya hapo akawa kimya hakusema kama kafika au laa yaan ndo anantumia text sahii saa 5 usiku kuwa alifika salama ila alishindwa kuniambia coz vidonda vya tumbo vilimshika akafikia kupumzika heheheh nacheka ila najua mwenyew wakuu but sijamjibu na sitamjibu lakini namsubiri arudi kesho nikitoka kazini anieleze vizur kuhusu hii safar yake japokuwa mimi sio mtu wa kumchunguza mwanamke na sipendi kabsa kuchunguza mtu sababu naelewa what’s gonne happen wakuu kama kuna la kuniongezea karibuni sana uwanja ni wenu
Nakumbuka askari mmoja wa kike aliwahi kusema "hamna mwanamke wa peke yako siku hizi, ukimfuatilia mke au mpenzi wakojiandae tu, kujiletea msongo wa mawazo"