Nina wasiwasi na mke wangu...

Nina wasiwasi na mke wangu...

Habar wana JF,
Naimani mko wazima.

Kiukweli nimekuwa na wasiwasi na safari ya wife, sijui kwanini lakini ni safari ambayo siielewi kabsa wakuu. Nina mashaka nayo coz naona mapicha picha tu.

Ni kwamba wife kasafiri juzi ijumaa kuelekea Singida lakini safari yake sielewi elewi kabisa, kwasabubu kwanza ni safari ya kushtukiza lakini pia mpaka now sielewi aim ya safari ni nini mpaka now.

Alhamisi amerudi kutoka kazini usiku tunalala ndiyo ananipa taarifa ya kuwa kesho Ijumaa anasafiri, nikamuuliza unaenda wap? Akaniambia kapigiwa simu na dada zake wamemuita ambao wanakaa Singida. Nikamuuliza kunatatizo akasema hapana, ila sijui wanashida gani na mimi ndiyo wamenipigia simu niende.

Kiukweli nilikuwa nimechoka nahitaji kupumzika, sikutaka ku complicate kitu, nikamjibu sawa nikalala. Then asubuhi nikajiandaa nikaenda kazini vizur. Niko job ananipigia simu kuwa ndiyo anatoka home anaelekea stendi kupanda bus. Iikuwa almost kama saa 7 hivi mchana nikamjibu haya na nikamuuliza kama kunakitu chochote anahtaji akasema hapana yuko powa.

Basi nikakata simu lakini kiukweli ghafla akili yangu ilishikwa na wasiwasi juu ya safari yake but sikutaka ku doubt anything nikapotezea. Baadaya kupita kama lisaa akanitumia message kuwa amepata basi but akifika Dodoma atashuka kuna ndugu yake anamchuka then wanaenda wote.

Daah, sikutaka pia ku doubt wala mambo mengi nikamjibu sawa, nikaachana naye nikaendelea na kazi zangu, but bado sikuona sababu ya yeye kushuka Dodoma. By saa 2 ndiyo ananiambia ndiyo wanaondoka Dodoma nikamjibu sawa safari njema tukaacha hivyo. Basi mi nikarud home usiku kwakuwa nilishapita somewhere nikapata chakula nikafika home niko good, nikaoga nikaingia kwa bed nikampigia ananiambia kashafika ila kachoka na safari nikamuacha nikapumzika.

Sasa leo Jpili tumeongea asubuh vizur tu na tukaagana baadae by saa 7 mchana ananiambia ndiyo anataka kurudi leo. Nikamuuliza mbona hukuniambia asubuhi na kwanini usingeondoka asubuhi? Sijaona cha maana anachonijibu, basi nikamwambia haya kama unarudi leo. Tuakaacha baada ya kama nusu saa ananipigia simu ananiambia kuwa yupo stendi, mara gari sijui hakuna, mara zimejaa, mara nimechoka nasikia usingizi, nikamwambia sasa siungebaki ili uondoke kesho asubuhi akasema sawa tukaacha.

Baadae ananitumia message eti amepata gari ila linaishia Dodoma kwaiyo atashuka Dodoma. Aloo nikasema kimoyomoyo hapo Dodoma hapo siyo bure, coz kwenda kashuka Dodoma kurudi baada arud kesho kama kweli kakosa usafiri na tumekubalina anarudi kesho mapema na sidhani kama kweli alikosa usafiri by that time ananiambia kuwa kapata usafiri.

Ila unaishia Dodoma so ataenda kulala Dom, sikutaka ku complicate nikamjibu sawa basi nikaachana nae. Ila cha ajabu baada ya hapo akawa kimya hakusema kama kafika au laa. Yaani ndo ananitumia text saa hii, saa 5 usiku kuwa alifika salama ila alishindwa kuniambia coz vidonda vya tumbo vilimshika akafikia kupumzika. Heheheh nacheka ila najua mwenyewe wakuu but sijamjibu na sitamjibu lakini namsubiri arudi kesho nikitoka kazini anieleze vizuri kuhusu hii safar yake.

Japokuwa mimi siyo mtu wa kumchunguza mwanamke na sipendi kabisa kuchunguza mtu sababu naelewa what’s gonna happen.

Wakuu kama kuna la kuniongezea karibuni sana, uwanja ni wenu.
Ushauri wangu bro achana nae usimuulize kitu mwache yete ndio awe anababaika kuleta narrative za safari zake
 
Mnyaturu kuliwa nje ni jambo la kawaida sana na hakuna namna yyt unaweza kumzuia kwahiyo huna budi kuzoea.

NB; Kwa kawaida taarifa yyt toka ukweni inayomhusu mke huanzia kwa mume ( mashemeji / wakwe hutoa taarifa kwa mume) kwamba kuna A B C na "wanaomba" mke asafiri halafu jibu wanalipata baada ya majadiliano baina ya mume na mke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nilimruhusu sababu yakusema ameitwa na dadazake but haijulikani nini shida kwakuwa ni familia yake nikamruhu aende ili tujue nini shida huko
Wewe hao Dada zake hauna mawasiliano nao?
Umejiridhisha kuwa kweli kulikuwa na huo wito?
Kwanini aitwe yeye direct bila kukujulisha wewe?
Maana ingekuwa family issue walitakiwa wakupigie wewe simu, wewe ndo uiratibu hiyo safari ya mkeo

Otherwise ni mtu mnaishi tu ila sio mkeo...
 
Hapana mkuu huwa naamua lakini hii sikutaka ku doubt coz nikimkataliga safar analalamika na kuona namuonea lakini pia nikwasababu tu kaeleza kuwa kaitwa na hajui nini shida kwa heshima tu za mashemeji nikamuacha aende ili akirud anieleze vizur hicho kilichomfanya akaitwa huko
Sio haraka kiasi hiko,ngoja aje akupe hiyo sababu uone kama inamashiko

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Hapana mkuu huwa naamua lakini hii sikutaka ku doubt coz nikimkataliga safar analalamika na kuona namuonea lakini pia nikwasababu tu kaeleza kuwa kaitwa na hajui nini shida kwa heshima tu za mashemeji nikamuacha aende ili akirud anieleze vizur hicho kilichomfanya akaitwa huko
Kwa kuwa katoa taarifa ghafla na usiku na amesema hakuna shida yoyote anakoenda. Jibu lilikuwa rahisi tu , "utaenda keshokutwa au wiki ijayo ". Hapo hawezi kukulaumu kwa kuwa hujamkatalia. Kuna wakati binadamu anatakiwa aongozwe kama ng'ombe ukimruhusu ajiongoze atakula mahindi ya watu
 
Sawa sawa mkuu nimekuelewa sana shukrani sana ntafanya hivyo najua atajaa tu wacha nijifanye niko good hakuna tatizo lolote kama ulivosema
Akijaa umepanga kumfanya nini? Assume umekosea na limepita unachotaka kukijua kinaweza ghalimu maisha ya mmoja wenu. Umeshasema una hasira na hasira iko karibu sana na ukichaa.
 
Nikweli mkuu ndo mchakato unaofuata shukrani sana mkuu kwa ushauri
Nakushauri acha lipite usifuate ushauri unaopewa ila next time kuwa makini na ufanye mambo kama mwanaume na mume
 
Mkuu nilimruhusu sababu yakusema ameitwa na dadazake but haijulikani nini shida kwakuwa ni familia yake nikamruhu aende ili tujue nini shida huko
Je uliwasaliana na hao mashemeji zako Kama kweli wamemwita mkeo!!? Au uliaamua kumuaamini tu mkeo!!??

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom