Nina wasiwasi na mke wangu...

Nina wasiwasi na mke wangu...

Kwanza jambo łakwanza huyo dada yake(Shemeji yako) ilipaswa pia akupe taarifa ya kumuhitaji mkeo.
Pili mwanamke anaomba ruhusa ya safari na sio kutoa taarifa ya safari hai make sense kabisa.
But yote umeyalea mwenyewe hapo MBUSUSU IMEPIGWA
 
Mimi mke wangu kuchukuliwa na mama tu kwenda kokote ni mpaka mama aniambie wiki moja before.. huyo ni mama yngu yani. Imagine mtu tu apige simu.. haahahah ila hizi ndoa za wakuu wa kaya wanawake zina shida sana
 
Nlitaka niseme maneno magumu nkaona hapa modi hawashindwi kunipiga ban af nkakosa uhondo.
Mpka sasa hv 1st half away team wanaongoza kwa goli 3.
Blaza, usisahau kunitag kwenye mrejesho
 
Hao mama wakwe ndio nuksi kabisa ,

Usiwe na jaziba sana ,Kuna mke wa mtu alinisumbua sana nimle mbusu mbusu nikagoma Tena mwenzake akawa anasema wapi imendikwa me mke wa mtu huku akigeuza kalio

Daah nihatari sana mkuu
 
Habar wana JF,
Naimani mko wazima.

Kiukweli nimekuwa na wasiwasi na safari ya wife, sijui kwanini lakini ni safari ambayo siielewi kabsa wakuu. Nina mashaka nayo coz naona mapicha picha tu.

Ni kwamba wife kasafiri juzi ijumaa kuelekea Singida lakini safari yake sielewi elewi kabisa, kwasabubu kwanza ni safari ya kushtukiza lakini pia mpaka now sielewi aim ya safari ni nini mpaka now.

Alhamisi amerudi kutoka kazini usiku tunalala ndiyo ananipa taarifa ya kuwa kesho Ijumaa anasafiri, nikamuuliza unaenda wap? Akaniambia kapigiwa simu na dada zake wamemuita ambao wanakaa Singida. Nikamuuliza kunatatizo akasema hapana, ila sijui wanashida gani na mimi ndiyo wamenipigia simu niende.

Kiukweli nilikuwa nimechoka nahitaji kupumzika, sikutaka ku complicate kitu, nikamjibu sawa nikalala. Then asubuhi nikajiandaa nikaenda kazini vizur. Niko job ananipigia simu kuwa ndiyo anatoka home anaelekea stendi kupanda bus. Iikuwa almost kama saa 7 hivi mchana nikamjibu haya na nikamuuliza kama kunakitu chochote anahtaji akasema hapana yuko powa.

Basi nikakata simu lakini kiukweli ghafla akili yangu ilishikwa na wasiwasi juu ya safari yake but sikutaka ku doubt anything nikapotezea. Baadaya kupita kama lisaa akanitumia message kuwa amepata basi but akifika Dodoma atashuka kuna ndugu yake anamchuka then wanaenda wote.

Daah, sikutaka pia ku doubt wala mambo mengi nikamjibu sawa, nikaachana naye nikaendelea na kazi zangu, but bado sikuona sababu ya yeye kushuka Dodoma. By saa 2 ndiyo ananiambia ndiyo wanaondoka Dodoma nikamjibu sawa safari njema tukaacha hivyo. Basi mi nikarud home usiku kwakuwa nilishapita somewhere nikapata chakula nikafika home niko good, nikaoga nikaingia kwa bed nikampigia ananiambia kashafika ila kachoka na safari nikamuacha nikapumzika.

Sasa leo Jpili tumeongea asubuh vizur tu na tukaagana baadae by saa 7 mchana ananiambia ndiyo anataka kurudi leo. Nikamuuliza mbona hukuniambia asubuhi na kwanini usingeondoka asubuhi? Sijaona cha maana anachonijibu, basi nikamwambia haya kama unarudi leo. Tuakaacha baada ya kama nusu saa ananipigia simu ananiambia kuwa yupo stendi, mara gari sijui hakuna, mara zimejaa, mara nimechoka nasikia usingizi, nikamwambia sasa siungebaki ili uondoke kesho asubuhi akasema sawa tukaacha.

Baadae ananitumia message eti amepata gari ila linaishia Dodoma kwaiyo atashuka Dodoma. Aloo nikasema kimoyomoyo hapo Dodoma hapo siyo bure, coz kwenda kashuka Dodoma kurudi baada arud kesho kama kweli kakosa usafiri na tumekubalina anarudi kesho mapema na sidhani kama kweli alikosa usafiri by that time ananiambia kuwa kapata usafiri.

Ila unaishia Dodoma so ataenda kulala Dom, sikutaka ku complicate nikamjibu sawa basi nikaachana nae. Ila cha ajabu baada ya hapo akawa kimya hakusema kama kafika au laa. Yaani ndo ananitumia text saa hii, saa 5 usiku kuwa alifika salama ila alishindwa kuniambia coz vidonda vya tumbo vilimshika akafikia kupumzika. Heheheh nacheka ila najua mwenyewe wakuu but sijamjibu na sitamjibu lakini namsubiri arudi kesho nikitoka kazini anieleze vizuri kuhusu hii safar yake.

Japokuwa mimi siyo mtu wa kumchunguza mwanamke na sipendi kabisa kuchunguza mtu sababu naelewa what’s gonna happen.

Wakuu kama kuna la kuniongezea karibuni sana, uwanja ni wenu.
Kwa hiyo unataka sisi tukuulizie kwa dada yakr kuhusu kumuita mkeo ghafla?

Kama ulimruhusu mkeo asafiri basi peleka machozi yako kwa mtoni.
 
Hao mama wakwe ndio nuksi kabisa ,

Usiwe na jaziba sana ,Kuna mke wa mtu alinisumbua sana nimle mbusu mbusu nikagoma Tena mwenzake akawa anasema wapi imendikwa me mke wa mtu huku akigeuza kalio

Sawa mkuu nimekuelewa
 
Akifika mwambie hivi safari yako niliamua kuifuatilia kwa ukaribu Sana kupitia simu yako hebu nielezekeze ulivyotembea nilinganishe na nilichofuatilia kupitia simu inavyoonyesha ulikopita na ulikokuwa

Yeah sawa mkuu nimekuelewa sana nitafanya hivyo
 
Mkuu vp kama mkeo, yupo jamii forum na ameona uzi wako the whole thread??

Fata ushauri huu kama una nia na mkeo
Mm huwa sina masihara huwa nachukua namba ambayo ni recent mara nyingi kwenye
Call logs then hapo sura mbuzi sicheki
Na kima mimi ni miyeyusho sana
Lazma aichanganue safari yake vzuri
Ndo awe huru...!! Tunasubiri mrejesho

Sawa mkuu nitaleta mrejesho
 
Chochote atachoomba kati ya hivyo atarajie ugomvi mkubwa [emoji28][emoji28][emoji28]! Hio ni benchmark tu. Likitokea gomvi ajue tu mkewe ameliwa taari.

Mkuu bola ugomvi kuliko upuuzi huu siwez mkuu kitaeleweka tu
 
Hapo ndo ninapogundua kuna shida katika jamii. Wanawake nyuzi zikianzishwa kuwaponda huwa mnajimaliza humu kujitetea au kucomment ili mjisawazishe na kuonekana sawa machoni pa watu. Leo kuna mwanamke amebugi lakini wanawake wako kimya. Penye makosa yenu hamuongei..au mnajipanga kuja na utetezi. Penye makosa mmekaa kimya...
Very absurd

Turudi kwenye mada. Huyu dada ni kweli kuna red flags na mkuu umeshashtuka. Akija utafanya kutokana na utakavyoamua. Ila humu kama una binti, mtoto, ndugu wa kike aliyeolewa embu muwe waelewa. Kuna kitu kinaitwa mamlaka. Mke yuko chini ya mamlaka ya mume. Na Yesu aliagiza utii kama kanisa linavyomtii yeye. Safari ya ghafla kirahisi tu..bila hata kutoa taarifa.

Wewe baba, mama unamuita binti na husemi kwa mume wake. Hii sio heshima. Ukitaka mkwe akupende na wewe heshimu mamlaka kama mume wa bintiyo. Misingi mnaiharibu. Baadae huyu kijana akiwa nongwa kwa binti yako mnaanza kusema. Kumbe hamkumuheshimu mwanzo. We are africans...lets live like african. Wewe mama uko na baba. Ulikua unanyanyuka kiholela kwenda mahali bila kumpa taarifa baba?? Au ndo kisa mna fedha mnakuwa hamjali???
Sad.
 
Hakutoka hata DSM huenda alisogezwa maeneo ya Bagamoyo tu. Hizo story za Dodoma hazi tally. La kama alifika Dom basi walienda na private ila aliishia Dom.

Hivyo kudai tiketi itakuwa gomvi kubwa na sababu ni ile ile,,, "Ina maana huniamini au?" kama huyo mke asipotumia hii point katika kubisha kwake uniite mi mbwa nimekaa zangu juu ya bed now.

Mkuu atanieleza leo ata makofi atakula asipoangalia mi ujinga staki kasha nitibua yaan now simuelew kabsa kiongoz
 
Back
Top Bottom