Nina wasiwasi sana na kesi zilizohukumiwa na Werema akiwa judge

Nina wasiwasi sana na kesi zilizohukumiwa na Werema akiwa judge

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Wana JF, kuna ukweli kwamba unaweza ukawa msomi sana na bado ukawa huna uwezo wa kutumia kisomo chako katika kuamua mambo. Kwa kifupi, mtu aliyesoma sana mambo ya utawala haina maana ndiye atakuwa mtawala au meneja bora sana kuliko wengine.

Kwa mantiki hii, nina wasiwasi sana na kesi zilizosimamiwa na Werema akiwa judge. Kwa kifupi namwona Werema kama mtu ambaye was probably one of the most incapable judges to have ever been appointed hapa Tanzania.

Ningependa sana kujua hukumu zake, na kesi ngapi alizohukumu zilikatiwa rufaa na rufaa hizo kufanikiwa. Wapi naweza kupata taarifa kama hizi?
 
Kuwa msomi hakuondoi tabia za asili za binadamu kama kusahau, kughadhabika, kusinzia n.k na kuwa tabia hizo haina maana kwamba elimu yako haina maana. Kilichotokea Bungeni kwa AG na KAFULILA ni havihusiani kabisa na taaluma zao, ni tabia za asili za mwanadamu kama kukasirika n,k. Kudharau taaluma ya mtu kwa sababu tu ya kutamka neno fulani inaonesha ni jinsi gani tulivyo weupe kwenye vichwa vyetu.
 
Hii mada haina mashiko. Ni swa na kusema mtu akilewa pombe hawezi kurudia hali yake pombe ikiisha. AG kukasirika na kutoa maneno makali Kwa KAFULILA sidhani kama ndiyo tafsiri ya kila jambo analolifanya.
 
Sasa naomba kukwambia kwamba kusoma ni pamoja na kuwa mstaarabu na kuweza kujua baya na zuri. Sasa tofauti ya msomi na ambae ni mbumbumbu itaonekana wakati gani?
 
Wanasheria waliosoma vema ni makini sana katika maongezi yao. Huyu bwana hilo limemshinfa kabisa. Nilianza kumdharau pale alipotoa kauli mbovu na akaja kuomba radhi tena bungeni. Katika hali ya kawaida watu wenye akili tuliona kama ni tatizo
 
Kuwa msomi hakuondoi tabia za asili za binadamu kama kusahau, kughadhabika, kusinzia n.k na kuwa tabia hizo haina maana kwamba elimu yako haina maana. Kilichotokea Bungeni kwa AG na KAFULILA ni havihusiani kabisa na taaluma zao, ni tabia za asili za mwanadamu kama kukasirika n,k. Kudharau taaluma ya mtu kwa sababu tu ya kutamka neno fulani inaonesha ni jinsi gani tulivyo weupe kwenye vichwa vyetu.

kusoma ni kustaarabika. kustaarabika ni pamoja na kucontrol emotions. kama judge, AG, lawyer, baba, mme na taja sifa zake zote anadanganya na anapobanwa aseme ukwel anatishia kupiga, kuua au kudhuru tena mbele ya chombo cha kutunga sheria nae akiwa mshauri mkuu hapo LAZIMA watu tuhoji taaluma yake.

wewe boya unakuja na utetezi wa kijinga kabisa. hivi hujui wanasheria hufundishwa ethics, hujui kama part ya kozi yao hujigunza logic? huna cha kucomment kaa kimya au cheza na wanao nyumban. idiot
 
Inafika pahala unweza kukufuru kuwa huu uongozi wote sijui umetokea wapi.
 
kuwa msomi hakuondoi tabia za asili za binadamu kama kusahau, kughadhabika, kusinzia n.k na kuwa tabia hizo haina maana kwamba elimu yako haina maana. Kilichotokea bungeni kwa ag na kafulila ni havihusiani kabisa na taaluma zao, ni tabia za asili za mwanadamu kama kukasirika n,k. Kudharau taaluma ya mtu kwa sababu tu ya kutamka neno fulani inaonesha ni jinsi gani tulivyo weupe kwenye vichwa vyetu.

mbona una chemka mapema?
Hujui kuwa tabia nini?.
Kwakusema haviusiani na elimu.kazi mi nakataa kwani tabia ndio inakuongoza kwenye kila kitu.tabia ni mfumo wa moja kwa moja wa maamuzi.
 
hii mada haina mashiko. Ni swa na kusema mtu akilewa pombe hawezi kurudia hali yake pombe ikiisha. Ag kukasirika na kutoa maneno makali kwa kafulila sidhani kama ndiyo tafsiri ya kila jambo analolifanya.

chukua mfano:
Mzee mtemba akilewa ana lia na kuji garagaza chini.

Jeni aki bughudhiwa hua ana susa kula

na wewe ukiambiwa ukweli una tukana matusi tena hapo habaki mzazi.

Fred na usomi wake wote havumilii matus we ukitaka kujua hasira zake ziko wapi mtukane.

Maana ya mf hii ni usemi huu!

Tabia ni sawa na ngozi ya mwili huwezi kuivua!!!
 
Hii mada haina mashiko. Ni swa na kusema mtu akilewa pombe hawezi kurudia hali yake pombe ikiisha. AG kukasirika na kutoa maneno makali Kwa KAFULILA sidhani kama ndiyo tafsiri ya kila jambo analolifanya.
Huwezi kukasirika kwa jambo lisilikuhusu.Hiyo issue inamhusu ndio maana anatapika
 
Wanasheria waliosoma vema ni makini sana katika maongezi yao. Huyu bwana hilo limemshinfa kabisa. Nilianza kumdharau pale alipotoa kauli mbovu na akaja kuomba radhi tena bungeni. Katika hali ya kawaida watu wenye akili tuliona kama ni tatizo
 
Werema ni mzigo kwa kweli.. Hana hekima wala Busara za kiuongozi..sijui hata JK alimwonaje hadi akamteua..mara nyingi namwona kama ni mtu asiyekuwa serious kakitka kutetea taifa letu..
 
Mimi mgeni maeneo haya, ngoja nisome some kwanza najua nitaelimika tuu :A S 109:
 
kwahiyo ulitaka aendelee kutukana na kuacha kuomba radhi! kweli hata kama lugha sielewi lakini picha naiona! wewe ni mweupe huko upstairs
 
mwanyika na werema wamepiga hela gani tena? hebu tupe data za kutosha. au ndio fununu kama kawaida ya JF
 
alichokosea nini hasa! maana unamwita mwenzako idiot kama wewe ndio perfect being. unaonyesha jinsi ulivyo mwepesi kwenye akili zako kwa kumtukana mtu kwa kutoa mawazo yake. huna tofauti na mtawala wa kiimla. jibu hoja kwa hoja na sio kutukana watu. halafu kuna kitu umesahau, hebu tupe takwimu za werema kutukana na kubishana kwa maneno makali akiwa bungeni.
 
Hii mada haina mashiko. Ni swa na kusema mtu akilewa pombe hawezi kurudia hali yake pombe ikiisha. AG kukasirika na kutoa maneno makali Kwa KAFULILA sidhani kama ndiyo tafsiri ya kila jambo analolifanya.

Mkuu sijatumia tukio moja la Kafulila kunifanya niwe na wasiwasi na busara za Werema katika nyanja ya sheria. Ni mfululizo wa matukio, kutia ndani uwezo wake wa kutafsiri sheria na na kauli anazotoa hadharani unaonifanya niwe na wasiwasi sana na hukumu zake kama judge.

Kama unampenda Werema ni juu yako, usilete hisia zako binafsi kwa Werema kwenye huu mjadala.
 
Naona wewe ndio Werema mwenyewe umekuja kivingine. Sasa naomba kukwambia kwamba kusoma ni pamoja na kuwa mstaarabu na kuweza kujua baya na zuri. Sasa tofauti ya msomi na ambae ni mbumbumbu itaonekana wakati gani?

Tofauti itaonekana wakati wa kupokea mishahara..!
 
Back
Top Bottom