Nina wazo hili wadau

Nina wazo hili wadau

KIATUE

Member
Joined
Dec 17, 2012
Posts
13
Reaction score
0
Nina wazo la kuwekeza katika cho kimoja hapa tanzania ambapo katika chuo hicho watu wengi hufuliwa nguo zao na wadada waliopo hapo chuoni sasa mimi nataka niwaajiri wafuaji hao ambapo nitaka kununua washing mashine ambayo nitaifunga katika site hiyo .
swali langu sasa napenda kama kuna mtu mwenye uzoeffu na mambo haya au anayejua bei za washing mashine mie nina milion moja nannusu ni hayo tu wakuu
 
Zile maxhine bhana zinauzwa kati ya laki 3-5, pia kuwa makini pindi ununuapo, kwani waweza uziwa mbovu.Isitoshe hao wanachuo ulishawataarifu kuwa unampango wa kuwapelekea mashine za kufulia nguo?,pia wanapenda nguo zao zifuliwe kwa njia ya mashine?
 
Ukinunua mashine maana yake una-replace human labour, kama walikua wafuaji watano bas atahitajika mmoja tu wa kusimamia zoezi.. Issue ya ajira kwa hao wamama haipo hapo.
Tatizo jingine ni cost za umeme na kiasi cha fedha ambacho madent wapo tayari kulipa.
Fanya research kwanza
 
poa mkuu ila umeme upo fresh coz hospitali inalipa flat rate na hapa hakunaga limit ya matumiz ya umeme
 
Nina wazo la kuwekeza katika cho kimoja hapa tanzania ambapo katika chuo hicho watu wengi hufuliwa nguo zao na wadada waliopo hapo chuoni sasa mimi nataka niwaajiri wafuaji hao ambapo nitaka kununua washing mashine ambayo nitaifunga katika site hiyo .
swali langu sasa napenda kama kuna mtu mwenye uzoeffu na mambo haya au anayejua bei za washing mashine mie nina milion moja nannusu ni hayo tu wakuu
Hiyo mashine itafanya pia kazi za ziada ambazo wadada hao wanazifanya?
 
Bila shaka unaongelea chuo cha Mzumbe wewe, kwa uzoefu wangu, biashara kama hiyo ilishaanzishwa pale ikafeli so kama unataka kuifanya acha nkupe changamoto utazokumbana nazo;
1. Wale wadada wanafanya delivery service, wanakuja kuchukua nguo chafu chumbani na wakishafua wanakuletea mpaka chumbani so ukitaka kuweza ushindani itabidi na wewe utoe hiyo huduma.
2. LAZIMA utapata resistance kutoka kwa hao wadada maana ukumbuke unawanyang'anya ajira
3. Nguo zikifuliwa zinahitaji kuanikwa, uandae eneo la kutosha kufanya Hilo
4. Running costs kama umeme na maji inhawa hizi sidhani kama zitakusumbua

Sina nia Ya kukukatisha tamaa lakini bila kufatilia hayo biashara itakua ngumu, otherwise kama ni pale Mzumbe soko la biashara yako ni kubwa sana ukijitangaza vizuri lazima utawin tu!
 
Back
Top Bottom