Bila shaka unaongelea chuo cha Mzumbe wewe, kwa uzoefu wangu, biashara kama hiyo ilishaanzishwa pale ikafeli so kama unataka kuifanya acha nkupe changamoto utazokumbana nazo;
1. Wale wadada wanafanya delivery service, wanakuja kuchukua nguo chafu chumbani na wakishafua wanakuletea mpaka chumbani so ukitaka kuweza ushindani itabidi na wewe utoe hiyo huduma.
2. LAZIMA utapata resistance kutoka kwa hao wadada maana ukumbuke unawanyang'anya ajira
3. Nguo zikifuliwa zinahitaji kuanikwa, uandae eneo la kutosha kufanya Hilo
4. Running costs kama umeme na maji inhawa hizi sidhani kama zitakusumbua
Sina nia Ya kukukatisha tamaa lakini bila kufatilia hayo biashara itakua ngumu, otherwise kama ni pale Mzumbe soko la biashara yako ni kubwa sana ukijitangaza vizuri lazima utawin tu!