Nina wazo la kuanzisha kikundi cha vijana kwa ajili ya kulima na kufuga

Nina wazo la kuanzisha kikundi cha vijana kwa ajili ya kulima na kufuga

Unamawazo mazuri sana lkn ukweli ni kua kupata vijana ambao wanayo huo utayari ndio changamoto kubwa, vijana wenzetu wanapenda sana kukaa mjini, na kuwafatilia zaidi akina Mobeto na Diamond, na kubeti kwenye kilimo wanachukulia kama kazi ya wazee waliopitwa na wakati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za kutwa mwana jf mwenzangu?.
Leo nimefikiria jambo nikaona sio mbaya kama tukilijadili kwa pamoja. Tatizo la watu wengi ni kutokuwa na ujuzi katika jambo fulani hasa katika ukulima au ufugaji unakuta mtu anamtaji ila ni namna gani ataweza kuendesha swala zima la kilimo au ufugaji inakuwa ngumu kufikia muafaka.
KWA MTAZAMO WANGU.(kila mtu atakuwa na mtaji wake ila tutalima katika eneo moja ila kupeana uzoefu)
Tuunde kikundi ambacho baadae tutakisajili tutajadili ni kilimo gani tukiendeshe.
mfano tupo watu 7 na tumechagua kilimo cha mpunga tutatafuta eneo la heka 21 kila mtu pata heka 3. Safari itaanzia hapo tutalima hadi mavuno kwa pamoja itatusaidia kupata uzoefu zaidi na hata badae tunaweza kuchukua mikopo kwa ajili ya kilimo maana tiyari tutakuwa tumesha fahamiana.
Karibuni kwa mawazo.
nb: Hakuna mtu atakae shika pesa za mwenzake bali kufanya kila kitu kwa pamoja kama ni kulipia shamba basi tutamtafuta muhusika baada ya hpo tutalipia kwa pamoja kila mtu akiwa anaona..
Biashara za patnership huwa ni nzuri kimtazamo na hata kwenye kuanza miradi ila kimbembe huja pale pesa ikishapatikana. Ushenzi huanza pale mmoja akiona kwamba flani anapata sana au yeye ndio anajiona ama mchango zaidi kwenye upatikanaji wa pesa.
 
Biashara za patnership huwa ni nzuri kimtazamo na hata kwenye kuanza miradi ila kimbembe huja pale pesa ikishapatikana. Ushenzi huanza pale mmoja akiona kwamba flani anapata sana au yeye ndio anajiona ama mchango zaidi kwenye upatikanaji wa pesa.
Mkuu hilo ondoa wasiwasi ndio maana nasema kila mtu atakuwa na mtaji wake hakuna kumpa mtu pesa bali tutatafuta eneo tutalima kila mtu na eneo lake lengo ni kubadilishana uzoefu ili hata yule asie jua na alifunze karibu sana
Kilimo kwanza
 
Back
Top Bottom