Nina wivu nashindwa hata kumeza mate!

Hahaha! Kesi ya mbuzi hakimu simba mwenye njaa ya siku nne?

where is ZD???? jeuri yako ya kuapproach ni wakati yeye hayupo tu akiwepo hapa unaufyata!!!

tumekutetea kakupunguzia kazi za nyumbani sasa unaleta jeuri si ndio eeeeh!!! endelea sasa uone vile ntanareti nikirudi home leo!!!
 
where is ZD???? jeuri yako ya kuapproach ni wakati yeye hayupo tu akiwepo hapa unaufyata!!!

tumekutetea kakupunguzia kazi za nyumbani sasa unaleta jeuri si ndio eeeeh!!! endelea sasa uone vile ntanareti nikirudi home leo!!!

Mwenzenu yuko matenite livu nyie mnachonga tu! Mmesahau alikuwa anatema mate hovyo majuzi kati hapa?
 
Nawashukuru wote kwa mawazo mazuri. Mniwie radhi sikuwa hewani wakati mnachangia. Kwa wale wanaouliza jinsia mimi ni She.

Nilitegemea kupata mawazo tofauti tofauti, sikuwa na aina ya ushauri nilioutegemea kutoka kwenu, vinginevyo kusingekuwa na haja ya kuomba ushauri! Once again, nawashukuru sana sana

Annina
 
tunashukuru pia Annina kwa hiyo utapunguza wivu au??😉
 
Matarajio yake yalikuwa nini? Apewe mbinu za kuongeza wivu siyo?

Asante Chrispin,
Nimegundua nina tatizo, natafuta namna ya kujikwamua sio kuongeza - ndio maana naomba ushauri wenu. Binaadamu tuna mapungufu yetu, mimi nina wivu, wengine uongo, wizi, uzinzi, uchawi, fitina, ubahili nk nk. kujitambua ni hatua kubwa kama wengine walivyoniambia, hatua inayofuata ni kujitahidi kubadilika, hakuna aliyemkamilifu.

Wivu kupitiliza ni tatizo na linaweza kupunguza mapenzi - lakini hii haimaanishi ndio kitu pekee kinachoweza kupunguza mapenzi, tabia nyingine pia zina uzito sawa, sio kweli kwamba wote wanoachana sababu pekee ni wivu. Nakubali mapungufu na najitahidi kupunguza ili angalau nifike kwenye kiwango kinachovumilika...

Asante sana,
Annina
 
tunashukuru pia Annina kwa hiyo utapunguza wivu au??😉
Apunguze au aongeze? Ongeza mwayego!

Mtu chake apendacho!
Hakina hila machoni,
Huridhika kuwa nacho,
Japo hakina thamani!
 
tunashukuru pia Annina kwa hiyo utapunguza wivu au??😉

FL1,
Nashukuru sana kwa mawazo yenu, nimejifunza mengi - nimeona kupitia jicho la tatu mwenzangu anajisikiaje ingawa halalamiki kwa sasa, lakini najua baadae atachoka ndio maana nachukua tahadhari na kuazimia kujirekebisha.

Nilikumiss sana hapa jamvini, naungana na wengine kukukaribisha tena na kukutakia mwaka mpya wenye mafanikio.

Asante sana,
Annina
 

hapa ushauri hauwezi kufanya kazi, wahi kwa mganga wa kienyeji kabla sichuesheni haijawa worst.
 

Asante sana Carmel,

Nimefikiri juu ya hili pia wakati najifanyia self asssessment with regard to mahusiano niliyonayo, ndio maana nikasema nahisi namnyima uhuru. Sio kwamba hana marafiki, anao na anawasiliana nao -sina tatizo na hilo. Shida ni pale nisipoambiwa sms imetoka kwa nani na niruhusiwe kuisoma... cha ajabu si mara zote nasoma hizo sms baada ya kuruhusiwa - huwa naridhika kwa kuambiwa na kupata ruhusa tu!

Annina
 
wewe annina nakushauri umsule tu hapo utakuwa na amani kabisa.kULE KWETU huwa tunasula ng'ombe wale wa kulima.unaambiwa Ng'ombe hata akiwa na sex drive kali akisulwa aka kuhasiwa kwisha kazi.
 
Achana na simu yake ila uwe unaichungulia kijanja mfano akienda kuoga hivi.Abiria chunga mzigo wako.Ila usimwonyeshe kuwa unamind saana mfano achana na kuuliza nani kamuandikia sms au kumpigia.wewe chunguza kiujanja asijue.Abiria chunga mzigo wako
 

Heeeh! Kumbe ubahili nao ni ugonjwa?....I am kidding!

Yote kwa yote sikuchangia tangu mwanzo lakini nimefurahishwa sana na ushauri uliotolewa kwa bibie. Na pia nimefurahishwa na kwa jinsi alivyokubali
mapungufu yake na kuahidi kuyafanyia kazi na kujirekebisha!

Jamvi naona liko vizuri katika suala zima la ushauri, burudani, vichekesho vya hapa na pale ili mradi yote heri tu wapwa na mabinamu!
 
We Annina inaonekana una matatizo kichwani humo kha! sasa mbona mtarimbo hujabadilisha? Mwenzio kaudownload mpaka amekuachia makombo wewe eti ukasusa kukaa kwenye kiti cha gari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…