Ninaachana na A-Level naenda D.I.T kusoma Diploma in Mining Engineering, Inalipa?

Ninaachana na A-Level naenda D.I.T kusoma Diploma in Mining Engineering, Inalipa?

Fibonacci

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2013
Posts
377
Reaction score
205
Mimi ni mhitimu wa kidato cha nne mwaka 2012. Katika matokeo yangu nimebahatika kupata Div One ya point 11...PHY-A, CHEM-A, MATH-A, BIO-C, Additional MATH-B....ningpenda kujua kati ya A level na DIT (technical education) ipi ni nzur zaidi, na kama DIT ni kuzuri zaidi, je Mining Engineering ina soko katika ajira (wahandisi hulipwa mshahara gani?)
Asenteni.
 
D.I.T elimu yao ni nzuri na itakufanya uweze kujitegemea au kujiajiri mwenyewe pale utapo hitaji kufanya ivyo na hii inatoka na mfumo uliopo pale. Kwa fani ambayo ni marketable ni Mechanical Eng, Electrical Eng pamoja na Civil Eng, Mining Eng kidogo ajira zake ngumu ngumu japo zinapatina.. Kuhusu maslahi itategemea kama umejiajiri au umeajiriwa wapi
 
Mimi ni mhitimu wa kidato cha nne mwaka 2012. Katika matokeo yangu nimebahatika kupata Div One ya point 11...PHY-A, CHEM-A, MATH-A, BIO-C, Additional MATH-B....ningpenda kujua kati ya A level na DIT (technical education) ipi ni nzur zaidi, na kama DIT ni kuzuri zaidi, je Mining Engineering ina soko katika ajira (wahandisi hulipwa mshahara gani?)
Asenteni.
diploma ni nzuri maana utasoma miaka miwili then kama ukipenda kusoma degree itakua poa pia....ukimaliza diploma utakua tofauti na wa form6 maana tayari utakua na ujuzi na hata degree haitokusumbua kivile....ila sijajua maswala ya loan(kama utahitaji) itakuaje??? na kusoma form6 kiasi flani ina kaugum tofauti na diploma....
 
Diploma of Engineer in Mining engineering ni miaka mitatu na hata Mech, Electr na Civil ni hivyo tu

Civil engineering ni nzuri zaidi kwani uwezekano wa kujiajiri na kuajiriwa ni mkubwa kotekote private sectors na serikalini
 
Diploma of Engineer in Mining engineering ni miaka mitatu na hata Mech, Electr na Civil ni hivyo tu
nimekwelewa mkuu....hatunaga diploma of engineer ila ni diploma of engineering in mining engineering!!!!
 
Yani nashangaa mnacomment kuhusu dit hlf hamjui et dipl miaka 2? unazan cbe pale? miaka mi3! mm nipo pale nachukua elect
 
Nenda MUST dogo kule ndo kuna elimu ya kufa mtu ukimaliza ajira pale pale
 
Uamuzi mzuri sana lakini one important warning.
Ili hiyo diploma iwe na mantiki kwako ni LAZIMA usome kwa bidii na kufaulu vizuri kiasi cha kuqualify for further studies.
Chuoni lifestyle ni tofauti na sekondari kwahiyo ukijisahau kidogo tu unaweza kuishia hapohapo kwenye diploma usipate degree.
Ukikaribia kumaliza diploma njoo hapa jukwaani tukupe ushauri how to move forward, kuna njia ukiifuata itakurahisishia sana mambo, ila maliza kwanza diploma.
Kila la heri.
 
Mdogo wangu 'there are so many ways to skin a cat' fuata moyo wako unataka nini alafu pia, hebu acha kwanza kufikiria ajira hebu kwanza fikiria masomo yaliyoko mbele yako, form 4 bado una safari ndefu sana, unaweza ukachagua hicho ukipendacho au unachoambiwa ni kizuri ukaja kuanguka kwenye masomo na usifike popote, soma kwanza, amini hakuna kozi mbaya mdogo wangu, soma na ufaulu kwa flying colours uone kama hutapata cha kufanya
 
Mbona kijana mnamdanganya na kumpotosha. Lazima awe na dira toka mwanzo. Enzi zetu za kusoma bila lengo eti tufaulu kwanza ndo tuone tutaenda wapi, zimepita. Huu ni wakati wa kuuliza huko mbele kukoje kama alivyouliza then kuangalia njia rahisi zaidi ya kukufikisha katika mafanikio.

Kijana mie nakushauri uachane na A-level maana utapoteza muda wako bure na nenda kasome hicho ukitakacho. Faulu vyema na ajira utapata
 
Sasa we nenda ukasome hiyo diploma yako alafu mwisho wa siku uishie kuwa mwana apolo pale mererani.
 
Utumishi kwa watanzania na sio mshahara! He unawaza mshahara leo, basi nimechoka
 
Mimi nafikiri akasome A' Level. Elimu ya diploma ni nzuri lakini unaweza kuishia kuwa technician usipate kwenda chuo kikuu ukasome na kuwa engineer. Lakini tii hisia zako. Chagua kile ukipendacho zaidi.
 
me pia natarajia kwenda d.i.t au m.u.s.t ninachokushaur nenda kasome tech coz kwa jinsi ulivyofanya katika matokeo yako ya o-level sidhan kama kufaul diploma kwenda degree itashindikana
 
mimi ni mhitimu wa kidato cha nne mwaka 2012. Katika matokeo yangu nimebahatika kupata div one ya point 11...phy-a, chem-a, math-a, bio-c, additional math-b....ningpenda kujua kati ya a level na dit (technical education) ipi ni nzur zaidi, na kama dit ni kuzuri zaidi, je mining engineering ina soko katika ajira (wahandisi hulipwa mshahara gani?)
asenteni.
si umeyashaachana na a level sasa soko la nini tena kilikufanya uachague huko ninin!
 
Nenda DIT mjukuu wangu! Ukifika msalimie Mzee Andimu kule jikoni. Ukimpa shikamoo zaidi na nyama utapata zaidi. Nyakati za jioni hadi usiku kule kiwanjani pembezoni mwa ukuta yalipo yale matenki ni kwa wale wajukuu zangu wanaopuliza ile mijani. Usisahau kujenga mahusiano mema na ma-warden ili upate meal card kwa bei chee.
Kila la Kheri Mjukuu wangu!
 
Acha kudanganya watu, shule gani umepata marks hizo? Marian na Kifungilo hawana A ya Physics. Feza sawa! Ulikuwa Feza?
 
Back
Top Bottom