Ninaachana na A-Level naenda D.I.T kusoma Diploma in Mining Engineering, Inalipa?

Ninaachana na A-Level naenda D.I.T kusoma Diploma in Mining Engineering, Inalipa?

Tujadili hoja acha kutaka kunifahamu kiundani ndio maana natumia fake id kuwakwepa wachimvi kama wewe. Nikikuambia mwaka niliomaliza DIT itakusaidia nini wewe ndugu yangu Asprin ?
Ulivyoniita mchimvi kwangu mie nliona inatosha na sikustahili tena kuwa ndugu yako. Au wapenda undungu na wachimvi?

Ustaarabu hauuzwi gengeni, says me.
 
USIJARIBU IKIWA UNA MALENGO YA KUENDELEA NA MASOMO (KUPATA DEGREE)

Binafsi nilichukua uamuzi kama unaotaka wewe kuchukua mwaka 1999, japokuwa sikupata marks nzuri za kunifanya kupata nafasi ya kidato cha 5 kwa shule za serikali (wakati huo) mzazi wangu alikuwa tayari kunipeleka private school (kwa wakati huo zilikuwa chache), lakini nilikataa. Nilijiunga DIT (wakati huo inaitwa Dar Tech na kuchukua kozi ya Mech. Eng.); Utakapomaliza ili kuingia university itahitajika upata alama nzuri zaidi (ambapo sio rahisi), vile vile utahitajika kufanya kazi kwa miaka 2 kwanza kabla ya ku-apply chuo kikuuu (labda kama kuna mabadiliko), utakapoomba mkopo (wanapewa kipaumbele form 6) kwa sababu wewe tayari una ujuzi.

Usiwe na haraka, wengi wanapomaliza kidato cha 4 hutamani kufanya jambo ili aanze kutengeneza pesa.

Kuhusu marketing ya kile unachotaka kusoma.....!, soma au kuchukua kozi ambayo unaipenda (utakuwa tayari kujifunza zaidi) na sio kulingana na watu wanvyolipwa; inaweza kuwa leo na soko zuri katika ajira, lakini baada ya miaka 3 mambo yakawa tofauti na hii ilitokea katika miaka fulani IT ilikuwa inalipa sana na kila mmoja akakimbilia kusoma IT; leo hii usijaribu...........!!!
Nikisoma hizo bold nauona upotoshaji mkubwa. Mwanzaoni nilifikiri labda ulisoma miaka ya zamani sana ambapo hayo mambo kweli yalikuwepo. Lakini kama ni mwaka 1999, utakuwa unaleta upotoshaji mkubwa sana, hasa hapo kwenye red bold.

Ukweli halisi ni kinyume na hayo uliyoyasema, usimkatishe dogo tamaa.
 
Kama hizo ndiyo pasi zako kweli, basi nakushauri uangalie mbele zaidi. Reach for the stars. Kama ni mambo ya kiufundi au uhandisi, lenga kuwa juu ya wote. Uwe mtaalamu. Nenda A-level utakuwa na uwanja mpana zaidi. Utaweza kusoma uhandisi. Fikiria kwenda hata kunako vyuo na program za mining kama Zambia au nchi nyingine. Ukiishia hapo ukaitafuta diploma tuu unaweza kuwa na njia ndefu zaidi. Usiwe na haraka sana.
 
Back
Top Bottom