USIJARIBU IKIWA UNA MALENGO YA KUENDELEA NA MASOMO (KUPATA DEGREE)
Binafsi nilichukua uamuzi kama unaotaka wewe kuchukua mwaka 1999, japokuwa sikupata marks nzuri za kunifanya kupata nafasi ya kidato cha 5 kwa shule za serikali (wakati huo) mzazi wangu alikuwa tayari kunipeleka private school (kwa wakati huo zilikuwa chache), lakini nilikataa. Nilijiunga DIT (wakati huo inaitwa Dar Tech na kuchukua kozi ya Mech. Eng.); Utakapomaliza ili kuingia university itahitajika upata alama nzuri zaidi (ambapo sio rahisi), vile vile utahitajika kufanya kazi kwa miaka 2 kwanza kabla ya ku-apply chuo kikuuu (labda kama kuna mabadiliko), utakapoomba mkopo (wanapewa kipaumbele form 6) kwa sababu wewe tayari una ujuzi.
Usiwe na haraka, wengi wanapomaliza kidato cha 4 hutamani kufanya jambo ili aanze kutengeneza pesa.
Kuhusu marketing ya kile unachotaka kusoma.....!, soma au kuchukua kozi ambayo unaipenda (utakuwa tayari kujifunza zaidi) na sio kulingana na watu wanvyolipwa; inaweza kuwa leo na soko zuri katika ajira, lakini baada ya miaka 3 mambo yakawa tofauti na hii ilitokea katika miaka fulani IT ilikuwa inalipa sana na kila mmoja akakimbilia kusoma IT; leo hii usijaribu...........!!!