safuher
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 11,837
- 17,412
Baada ya salamu naomba kushare nanyi jambo hili ambalo nimekuwa nikilitafakari kwa siku nyingi sana.
Kuhusu mambo ya kilimwengu hasa haya mambo ya sayansi na technolojia.tukiangalia namna tunavyopata picha katika tv kupitia ving'amuzi mbalimbali na sauti na watu tukawaona live pale kwenye screen, naamini fika kuna kanuni za kilimwengu ambazo zinaongoza haya mambo bado hatujazijua vizuri
Ni jambo kubwa sana kuona tukio la kigoma live ukiwa pale gongo la mboto ukiangalia television.lakini leo tunaona na ni kweli.
Tunaongea na mtu akiwa mbali kabisa kupitia simu na bado tunasikiana,hili linafikirisha sana hawa waliogundua walitumia fika akili zao
Kinachonifanya nione kuwa kuna kanuni za asili zinaendesha haya mambo ni kwa sababu zifuataza.
1.Wote tumekuja duniani tumekuta kanuni zipo tayari tokea hapo zamani tulichofanya ni kutumia hizo kanuni na sio kuzianzisha.
Mfano kanuni ya third law of motion hii ilikuepo tangu na tangu hata kabla ya isaack hajazaliwa,kazaliwa kaikuta kabisa hii kanuni akaanza kufanya mambo yake kupitia hii kanuni.
Na kanuniz zingine nyingi sana.
Mfano mzuri ni kanuni ya kusafirisha mawimbi ya sauti kutoka kwenye simu yangu kuja kwenye simu yako ukiwa mbali.
Ninaamini kuna kanuni ya asili ambayo hao waliotengeneza simu wameikutawao wakaunda vifaa tu na kuacha kanuni za asili zifanye kazi yake.
Siamini kama wao ndo wanasafirisha hizo sauti kutoka kwa mtu kwemda kwa mtu,bali kanuni za asili ndo zinafanya mambo hayo.
Hata katika mambo mbalimbali ya kusafirisha picha kutoka kigoma live kuja dar tukaona kwemye tv naamini kuna kanuni za asili zinazoongoza haya mambo.
Ninaamini kanuni hizo sio kwamba zimejificha,zipo ila tunaweza kuzipata kupitia matendo yetu ya kawaida ya kila siku tukatumia kanuni hizo kufanya matendo makubwa zaidi.
Mfano mimi naamini kuwa mtoto analijua jina lake kwa sababu ya kuitwa mara nyingi jina hilo na watu wakimuangalia yeye,kupitia kanini hiyo ya marudio ya sauti mtoto anajua kuwa hapa anaitwaax yeye na hilo ndio jina lake.
Hivyo kupitia kanuni hii ya asili ya marudio,mtoto mdogo ukimuita jina lake mara 1000 kwa siku kwa muda wa mwaka mmoja.
Na mtoto mwingine kwa siku ukamuita jina lake mara 1 kwa siku kwa muda wa mwaka,basi huyo wa mara 1000 atajua mapeema kuwa hilo ni jina lake na huyu wa mara 1 atachelewa kujua jina lake.
Hii ina maana ya kuwa kutumia kanuni hii ya asili ya marudio tunaweza kumpa jina paka,au mbwa au hata panya unaemfuga kwa kurudiarudia kumuita jina hilo.
Sio kwamba wanaowapa majina wanyama kuwa wao wamesababisha na wanauwezo hapana,bali walitumia kanuni ya asili ya marudio ambayo wameikuta duniani kufanya mambo yao ambayo yanategemea kanuni hizo.
Je, una mawazo yeyote juu ya hili suala ?
Karibu