Ninachoendelea kujifunza kwenye sakata la Ajibu

Airmanula

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
3,527
Reaction score
5,762
Nikisoma habari za huyu bwana mdogo naishia kucheka tu.

Mfano ukichukulia mchezaji Samata, nawaza samata angekua na demand kubwa na kujiona yeye ni staa sidhani kama angekua hapo alipo, wakati anaenda Tp Mazembe aliona ni njia pekee ya yeye kufika mbali kimataifa na kwenda ulaya, kwahio kitu muhimu katika maisha ni kujishusha na kukubali kile ambacho kwa wakati huo unakipata ama utaenda kukipata kwa malengo ya kwamba one day thamani yako itazidi kukua na itaonekana tu.

Tp mazembe ni klabu kubwa na ina program na mipango madhubuti, sasa nashangaa sana mtu ambaye anatoka tanzania kwenye timu tena iliyo kwenye matatizo makubwa kwa sasa, anashindwa kukubaliana masharti binafsi. Hapo hakuna lingine ninaloliona zaidi ya vitu viwili, kwanza selfish na kujiona wewe ni mkubwa sana hata zaidi ya Tresor Mputu, ina mana kweli Tp Mazembe klabu kubwa inashindwa kukubaliana masharti binafsi na mchezaji? Nasema hapana, shida kubwa iko kwa mchezaji, kujiona staa na ku demand vitu vikubwa ambavyo kama ungekua loyal vingekuja tu huko mbele mana mikataba hua inaboreshwa. Hapa ndipo tunapoona umuhimu wa wachezaji kua na MANAGERS.

Kingine ni usimba na uyanga, mchezaji anaona wenzie wnaakula shushu na yeye anaona ni haki yake naye awepo hapo, wakati anaondoka vilisemwa vijembe vingi sana mpaka ikafikia hatua akifunga anavua shati anaenda kuwaonesha mashabiki wa simba jezi namba kumi..
Sasa leo hii anaona kule kutamu, mbinu zinasukwa ili arudi, alikua wapi wakati simba tuna struggle kujitoa wakati huo tunaitwa simba wa matopeni,/michangani?? Binafsi ningekua Aussems nisingemsajili kabisa. Nawapongeza pia Tp Mazembe kwa kubwaga manyanga, tp mazembe wako bize na hawana muda wa kuchoshana wako straight na mambo yao hawapindishi pindishi. Na simba mkimsajili huyu mtu ntashangaa sana. Mara mia okwi abaki.
 
Ukisikia akili za kuazima ndio hizo za huyo jamaa

Think about kitu ambacho angeenda ku achieve kule ...aisee

Sishangai kumuona samata premier league ya uingereza next time soon
Ila ukute wakala ndo analamba nyingi jamaa kaona bora wakose wote
 
Mkuu ipo hivi, Ajibu alikuwa ana tamaa ya hela akasign mkataba wa awali na Simba na hela alishachukua, hiyo ilikuwa kwa Siri, TP Mazembe na kina Zahera hawakujua, ilipokuja suala ya mkataba na Mazembe Ajibu akawaeleza waongee na Simba, ndipo simba wakasema wanataka Mil 220 mezani kumwachia, ndo mazembe wakasusa dili
Ukisikia akili za kuazima ndio hizo za huyo jamaa

Think about kitu ambacho angeenda ku achieve kule ...aisee

Sishangai kumuona samata premier league ya uingereza next time soon
 
Hapa usiwasingizie mazembe
Huyu dogo fundi ajibu ni kipenzi cha mo
Kama zengwe limetengenezwa na simba
Moo kafika dau kubwa kamshawishi dogo
Ikabidi aachane na mazembe kwa kisingizio
Cha kushindwa kukubaliana maslahi binafsi na mazembe. na Mimi sioni ajabu hata alivyokaa
Kama ni level sasa ivi simba inakimbilia kuwa leval ya timu kubwa kama mazembe

Na ndomana sasa hivi mchezaji atayetakwa
Na simba ni ngumu kuchomoa awe wa ndani ama wa nje.

Mimi namkaribisha kabisa kwa mikono miwili. cc Shadeeya
 
Simba inakimbilia level za mazembe,okaay
 
mpira bongo umekua.. mazembe wakugombania mchezaj na timu za bongo!!
 
Unaona sasa... Na simba why wanasumbuka na huyu mtu
 
Ndio hicho ambacho nakisisitiza..namchukia jamaa kinyama ...nikikumbuka tunaitwa simba ya matopeni
Kati ya watu naochukia warudi simba ni Ajibu, aliondoka kwa madharau Sana wakati tukiwa kwenye hali ngumu
 
Ndio hicho ambacho nakisisitiza..namchukia jamaa kinyama ...nikikumbuka tunaitwa simba ya matopeni
Ajib hajaikimbia Simba Simba hawakua nampango nae maana ndio mwaka Simba tulifanya usajiri mkubwa....kessy ndio kaondoka kwa nyodo
 
Simba inakimbilia level za mazembe,okaay
Tumekuwa wakubwa sasa;
Mechi za mchangani tumeachia wengine

Tunao uwezo wa kuchukua mchezaji yeyote yule tokea timu yeyote ile kubwa Africa; sembuse huyu dogo; tumefuka dau kubwa kuliko mazembe, migomba akajisemea bora abaki kwenyerere hapa hapa
 
TP Mazembe wana Ndege wana uwanja imeshinda makombe Africa,huwezi kusema Simba iko level ya Mazembe
 
TP Mazembe wana Ndege wana uwanja imeshinda makombe Africa,huwezi kusema Simba iko level ya Mazembe
Nimesema simba inakimbilia level; alafu icho kigezo chako sijui cha makombe nk. Ni historia tu izo mkuu hata ac millan ni timu kubwa iliyofanikiwa kubeba makombe mengi nyuma ya Madrid lakini kwa sasa hivi sio timu bora ni timu yenye jina kubwa ila kwa sasa hivi huwezi waweka meza mmoja hata na totnham kwa ubora.
 
Kwenye hili Ajib atakua yupo sahihi...maana kibongo bongo mchezaji akiwa huru uwa anasajiriwa na anapewa fedha za usajiri binafsi Jambo ili ni tofauti na ulaya labda na nchi zengine znazojiendesha kiprofesheno Sasa itakua Mazembe walikubaliana nae mshahara tuu na hawakuwa tayari kutoa hela ya usajiri Sasa Simba itakua imetoa hela kwa mchezaji na maslahi binafsi wamemalizana
 
Ndugu yangu Simba haijawahi kuchukua kombe lolote Africa na wala haina miundombnu na thamani kama hao jamaa
 
Tumekuwa wakubwa sasa;
Mechi za mchangani tumeachia wengine

Tunao uwezo wa kuchukua mchezaji yeyote yule tokea timu yeyote ile kubwa Africa; sembuse huyu dogo; tumefuka dau kubwa kuliko mazembe, migomba akajisemea bora abaki kwenyerere hapa hapa
Kusema kweli mmekua ila level za mazembe mkuu,mbali sana,
Hivi mnaweza kugombania mchezaji mmoja na Tp alaf aje kwenu agome kwenda kwa mazembe,bado sana ila atleast mna uelekeo mzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…