Ninachokiona kuna baadhi ya viongozi wanataka kulifanya suala la maandamano ni la Wakristo dhidi ya serikali na dini yao

Ninachokiona kuna baadhi ya viongozi wanataka kulifanya suala la maandamano ni la Wakristo dhidi ya serikali na dini yao

kulagha nenga

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2026
Posts
690
Reaction score
1,375
Kuna Kila jitihada zina fanyika kuyafanya maandamano yaliyotangazwa na wanaharakati yaonekani ni ya wakristo kuipinga serikali inayoongozwa na muislamu.

Mimi siungi mkono maandamano hayo, kwasababu maandamano lazima yafuate taratibu na ajenda inayoeleweka hasa katika kipindi hiki Taifa likiwa kwenye mkwamo . Sasa hivi tujikite kutafuta muafaka na sio kuchochea mifarakano

Chakusikitisha Kuna baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu wanatoa matamko na kauli zinazotia wasiwasi kanakwamba wao ni sehemu ya jeshi la polisi au serikali.

Yaani wameunda vikundi vya vijana kuzuia maandamano. Je vijana hao ni wa dini gani? Kwani serikali imeshindwa kufanya kazi yake?

Pili maswala yote yanayo husu demkrasia na haki za binadamu yaonekani ni ya wakristo, kwao ni chokochoko dhidi ya kiongozi wa nchi ambaye ni muislamu jambo ambalo si sahihi na upotoshi wa maksudi

Ushauri wangu kwa serikali hata kama kuna baadhi ya wanasiasa wananufaika na aina hii ya siasa LAKINI tujue hilo ni bomu litalipuka tu. .Serikali itoke hadharani kulikemea

Mwisho niseme hili jambo kadiri linavyoendelea ndivyo linafanya nchi wafadhili waone tuna matazizo ya kidini dhidi ya dini nyingine,. Sisi ni ndugu moja tamaa za viongozi wa kisiasa zisitumike kutugawa
Mungu ibarika Tanganyika ibariki Tanzania
 
Mashehe ubwabwa ndo wanaibua mijadala ya kidini,
Wananchi wanataka katiba, utawala Bora na uwajibika ila utawasikia mashehe ubwabwa wameleta uhuni wa agenda za udini
 
Hao mashaikh hawana elimu, ndio tatizo lao, wanaleta taharuki za kidini kana kwamba wakristo ndio washadidiaji wa hayo maandamano yasiyofahamika kwa wananchi wengi
 
Tumempa shilole aiongoze Tanzania unategemea nini?
Hao masheikh sio wa kulaumiwa Bali huyo ambaye yupo ikulu ndiyo ameratibu haya yote..... watanzania najua wamejifunza kuwa siku nyingine hawatathubutu kumpa mzanzibar nchi
 
Tumempa shilole aiongoze Tanzania unategemea nini?
Hao masheikh sio wa kulaumiwa Bali huyo ambaye yupo ikulu ndiyo ameratibu haya yote..... watanzania najua wamejifunza kuwa siku nyingine hawatathubutu kumpa mzanzibar nchi
Kuna wakatoliki walienda kuimba "Mwambaaa ni Yesuuu"! Mmesahau?
Haya tote yanaratibiwa na yeye ndo maana mikanganyiko haiishi.
 
Back
Top Bottom