Sioni namna Simba itakavyokubali tena kuendelea kunyanyaswa ili yanga wapate ubingwa.
Yanga hawawezi kucheza mpira kihalali ni lazima watumie mbinu nyingi za hovyo kwa msaada wa vyombo vyote vikiwemo vya serikali. Simba wamekataa kuwa wanyonge maana wanataka mpira uchezwe sio figisu nje ya uwanja na kupitia waamuzi.
Kutokana na msimamo wa Simba kugomea mechi,yanga nao hawakubali tena kupangiwa siku nyingine kwa vile watalazimika kuwekeza tena nje ya uwanja kabla ya mechi nyingine.
Kutokana na mvutano huu,na aina ya viongozi waliopo yanga na Simba ni kama wote hawana akili ya kufikiria vizuri matokeo ya maamuzi yao.
Hivyo, ninaona ni wazi hizi timu kuna uwezekano wa kususa kucheza ligi ama kuendeleza mapambano dhidi ya mamlaka za soka.
Ninachokiona mbele, umefika mwisho wa ubora wa ligi, na sijui kama utakuja kurudi tena kwenye ubora wake hivi karibuni.
GSM amefanikiwa sana kwa msaada wa mabilioni yanayochepushwa kutoka serikalini, kutengeneza ufalme wa yanga nje ya uwanja, na kuua soka la ushindani ndani ya uwanja, na kuufanya mchezo wa soka kama maigizo ambayo tunajua mwisho wa picha utakuwaje.
Sisi wengine tungependa mamlaka wawe wakali hasa kwenye kanuni, bila kujali nani amekosea. Kosa la kuizua timu kufanya mazoezi kabla ya mechi liwe na adhabu kali sio faini milioni moja.
Makosa yanayoashiria ushirikina kama kupita geti lisiloruhusiwa yawe na adhabu kali sio faini ya milioni moja iwe hata milioni 300.
Sent from my Infinix X626 using
JamiiForums mobile app