Ninachoona, ligi yetu ndiyo imezikwa rasmi kuanzia jana

Mbona mwaka 2021 haikuzikwa??
Huenda kulikuwa na viongozi wenye hekima kiasi fulani.
Ila kwa hili la sasa,huu moto waliouanzisha wanachochea ili waone nini kitatokea.

TFF wako njia panda.
Serikali kuhusika kuhujumu timu kwa ajili ya timu nyingine ni kitu cha ajabu sana.
Meneja wa uwanja ni serikali, polisi waliotumika kuzuia basi la Simba ni serikali,mabaunsa waliohusika ni mamluki wa yanga.Mpira umekuwa kama siasa za cuf na ccm Zanzibar,chadema na ccm bara.Uhuni unaanza kuzigubika hata fani zinazowasahaulisha watu shida zao.
Udhaifu wa viongozi kwenye hizi club umekuwa tatizo kubwa jingine.

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Jamaa ameandika madini sana.Kiufupi itafikia hatua hakuna mtu atapenda kuangalia mechi za ligi ya Bongo kwa kuwa utakuwa ni upuuzi tu,ndio maana ligi ya Italy ishu ya upangaji matokeo hadi leo ligi yao haina mvuto tena.Watu wanashindwa kujiuliza kwanini EPL miaka na miaka ina mvuto ...Ki ukweli Yanga na TFF wanaharibi ligi hii.Yaani mechi za Yanga zikichezwa kila mtu anaenda na matokeo uwanjani unajua kabisa Yanga anashinda.Angalia mechi za Simba zinavyokuwa ngumu hasa hizi za Ndani,Yaani Simba anapata ushindani wa kweli.Hiki kitu kinatesa hadi timu ya Azam ambao nao wanawekeza Fedha nyingi kujenga timu..
Ki ukweli kama haya hayatopigiwa kelele watu wataacha kuangalia hata TV ,itakuwa hasara kwa Azam tv na thamani ya ligi yetu itashuka.Tukemee hili la Yanga kupanga matokeo,halina Afya kabisa.
 
Shida sio simba vs yanga sheria ni dhaifu,and waliopo madarakani hawana meno
 

Yanga amemfunga simba mechi 4 mfululizo..

Je simba na yeye huwa anapanga matokeo kwa kumruhusu yanga amfunge kila siku ?
 
Mtoa mada hauna ulijualo,endelea kukaa apo kwa shemeji yako.
Simba na Yanga itaendelea kuepo,Gsm ataendelea kuepo.
Hauchangii hata sh mia kuchangiaa maendeleo ya timu yoyote,hata kadi ya uanachama wa timu yoyote huna..
Kazi kubwabwaja tu.
 
Yanga amemfunga simba mechi 4 mfululizo..

Je simba na yeye huwa anapanga matokeo kwa kumruhusu yanga amfunge kila siku ?
Matokeo ya 5-1 unajua uhalisia wake?? Kwanini Manula hadi leo hachezi? Kwanini Simba waliuza wachezaji wote wenye majina? Unajua nini kilitokea siku moja kabla ya Mechi?
Angalia mechi za Simba vs Yanga mnasema makosa ya waamuzi kununuliwa yanvyoigharimu Simba.
 
Siasa hizi. Hahaha. Ngoja niendelee kusoma.
 
Wanasema wamesajili vizuri sana ndo sababu ya matokeo bora na mwaka jana walifika fainali shirikisho sababu ya kusajili vizuri. Hapo vipi?
 
Wewe unapiga domo na kuzunguka zunguka bila hoja ya msingi,,ungetamka wazi kwamba Simba aikuwa na hoja yoyote ya kikanuni Wala kisheria za soka kugomea mechi,,na bodi ya ligi aikuwa na hoja yoyote ya maana kuahirisha mechi,,kwa maana iyo mnajua kwamba yanga awezi kuendeshwa na wajinga wachache kwa manufaa binafsi ya mapenzi yao kwenye hivi vilabu kwa kutoa maamuzi ya ovyo kuahirisha mechi,,yanga atocheza mechi nyingine yoyote ya derby ndio imetoka iyo
 
GSM amefanikiwa sana kwa msaada wa mabilioni yanayochepushwa kutoka serikalini, kutengeneza ufalme wa yanga nje ya uwanja,
Haya maneno ya hatari kwako.
Tuhuma nzito ambazo ukidaiwa uthibitishe utashindwa.
JF siyo kichaka cha kuchafua watu au taasisi mbalimbali.
Maxence Melo , Paw , Active , Moderator angalieni hilo kulinda taswira ya JF na kuepuka migogoro ya kisheria.
JF isiwe sehemu ya kuumiza watu kwa mambo yanayo zuilika kama haya. Mumdai ushahidi huyu mdau mjivue lawama.
 
Haya maneno ya hatari kwako.
Tuhuma nzito ambazo ukidaiwa uthibitishe utashindwa.
JF siyo kichaka cha kuchafua watu au taasisi mbalimbali.
Nilichojifunza JF ni kuwa ukiona mtu anaandika humu mambo kama haya uwezekano ni kuwa ana imune ya kimtaa ndo maana kuna watu humu hawana woga wa kutoa tuhuma, ukiiga na huna hiyo imune id baada ya muda inakuwa idle, unaikimbia wewe mwenyewe.
 
Shida ya simba wakiifunga wydad halaffu wakibattle na al ahly halafu wakaongoza kundi kwao ni mafanikio makubwa wakat overall performance timu inaishia robo..ni uzuni kabisa kwa watu wanaojua mpira
 
Juzi mzee Dewji kapigilia msumari kuwa ni Wajinga😆 wasamehe tu
 
Wanasema wamesajili vizuri sana ndo sababu ya matokeo bora na mwaka jana walifika fainali shirikisho sababu ya kusajili vizuri. Hapo vipi?
Yanga Kufika fainali caf sio kigezo cha ubora .
Robo fainali anacheza na Marumo gallants timu ipo mkiani mwa ligi ya South Africa
Nusu fainali anacheza na rivers United timu dhaifu kuliko, Alafu anajisifu amecheza fainali ya cafcc??

Hii ni aibu.
 
Yanga Kufika fainali caf sio kigezo cha ubora .
Robo fainali anacheza na Marumo gallants timu ipo mkiani mwa ligi ya South Africa
Nusu fainali anacheza na rivers United timu dhaifu kuliko, Alafu anajisifu amecheza fainali ya cafcc??

Hii ni aibu.

kama walikuwa dhaifu walifikaje nusu fainali ?

mbabe wako tp mazembe na yeye alipigwa nje ndani sasa sijui na yeye alipanga matokeo
 
Kweli simba imejaa mambumbumbu, hivi aliyezuia pitch feeling ya simba ni nani? Next time ukitaka kuleta hoja tafuta facts kwanza.
 
Mtapoa tu na maisha yataendelea kama kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…