Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Hizi bifu na Kenya sasa naona kama ni utoto na nashangaa inafikia hata viongozi wetu wa ngazi ya mkoa wanahemuka na maamuzi bila kufikiria kumaliza mambo kidiplomasia. Hawa viongozi wanadhani wanamfurahisha Magufuli lakini ukweli ni kwamba wanamdhalilsha Magufuli na Tanzania kwa ujumla.
Ona kwamba tumekuwa na migogoro mipakani sio na Kenya tu, bali na Rwanda na Zambia pia. Hiyo ni dalili kwamba sisi ndio wenye tatizo. Ukiona kila siku wewe tu ndio unagombana na jirani zako, tatizo sio jirani, ni wewe!
Kwanza kabisa tuelewe kwamba nchi hizi jirani, japo sisi hatukuweka lockdown, wao waliweka. Sasa hatuwezi kuwalazimisha wasiwe na lockdown kwa Watanzania kwa kuwa sisi huku kwetu hakuna - huko ni kukosa si tu busara bali akili pia. Kwa mfano, Kenya wana lockdown kiasi kwamba hata kusafiri kati ya jimbo na jimbo, mfano, Nairobi na Mombasa, hairuhusiwi isipokuwa kwa vibali maalum.
Sasa sis tunachotaka kwa Wakenya au Rwanda au Zambia ni nini hasa? Tunataka madereva wetu wasipimwe wanapoingia kwenye hizo nchi? Au tunataka madereva wetu hata wakipimwa wakaonwa wana Corona waruhusiwe tu kuingia kwa kuwa kwetu hakuna lockdown?
Ona kwamba madereva wetu wanasema hawaviamini vipimo vya Kenya. Kenya watafanyaje vipimo vya udanganyifu kwa madereva ambao wanapeleka bidhaa kwao? Hiyo ni akili kweli kudhani mtu unaemplekea bidhaa kama chakula nk akukomoe kwa kukufanyia kipimo cha uongo? Tanzania tunataka tuamini vipimo vipi, maana hata vya kwetu tulisema vinasema mapapai yana Corona ni vipimo feki. Kama ni hivyo tupimwe madereva wetu mipakani basi ili wanapopimwa upande wa Kenya tuweze kubisha kisayansi kuwa upande wetu tumewapima wakaonekana negative.
Vitu vingine tusijifanye kuwa wajuaji na kukorofishana na jirani zetu pasipo sababu. Hatuwezi kuwalazimisha wasiwe na restrictions za Corona kwa kuwa sisi hatuna. Kama sisi hatuna restriction basi ni sawa madereva wao kuingia kwetu bila kupimwa, lakini hatuwezi kudai kuwa na madeeva wetu waingie kwao bila kupimwa!
KUmbuka kwamba madereva wa Kenya wakitoka Tanzania wanaporudi kwao wanawekwa quarantine - sasa kama wanafanya hivyo kwa madereva Wakenya, kwa nini tuone sio sawa wakisema madereva wa Tanzania wawekwe quarantine?
Ona pia thread hii:
Tunaweza kuona tuna msimamo imara suala la Corona lakini mwishoni gharama yake inaweza kuwa Tanzania kukosa heshima na kupoteza urafiki na nchi jirani