Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
- Thread starter
-
- #41
Huo ndio utoto ninaosema tunao, sisi na viongozi wetu. Na Kenya hawajasema msiende kwao, wamesema msiingie kwao ikiwa mtapimwa mkaonekana mna Corona. Mnachokataa hapa ni kwamba hamtaki mpimwe kwa kuwa sisi hatuwapimi madereva wao. Sasa tusilazimishe utaratibu wetu uwe wao.Mkuu mbona hiyo ni simple logic, kama hutaki mi nifike kwako basi we usije kwangu
MONEY STOP NONSENSE
Na wewe uko Horohoro sivyo ndio maana unajua unachosema? Ila naona umesema nenda Horohoro, sio njoo!Ungefanya research kwanza kabla ya kuandika huu uzi ungekuwa umefanya la maana. Acha kudandia gari kwa mbele. Nenda horohoro ukaangalie hali ilivyo ujue undani wa hili swala.
Sent using Jamii Forums mobile app
wewe ujaelewa.hii ni vita ya kiuchumi kwa kusingizia corona.Hizi bifu na Kenya sasa naona kama ni utoto na nashangaa inafikia hata viongozi wetu wa ngazi ya mkoa wanahemuka na maamuzi bila kufikiria kumaliza mambo kidiplomasia. Hawa viongozi wanadhani wanamfurahisha Magufuli lakini ukweli ni kwamba wanamdhalilsha Magufuli na Tanzania kwa ujumla.
Ona kwamba tumekuwa na migogoro mipakani sio na Kenya tu, bali na Rwanda na Zambia pia. Hiyo ni dalili kwamba sisi ndio wenye tatizo. Ukiona kila siku wewe tu ndio unagombana na jirani zako, tatizo sio jirani, ni wewe!
Kwanza kabisa tuelewe kwamba nchi hizi jirani, japo sisi hatukuweka lockdown, wao waliweka. Sasa hatuwezi kuwalazimisha wasiwe na lockdown kwa Watanzania kwa kuwa sisi huku kwetu hakuna - huko ni kukosa si tu busara bali akili pia. Kwa mfano, Kenya wana lockdown kiasi kwamba hata kusafiri kati ya jimbo na jimbo, mfano, Nairobi na Mombasa, hairuhusiwi isipokuwa kwa vibali maalum.
Sasa sis tunachotaka kwa Wakenya au Rwanda au Zambia ni nini hasa? Tunataka madereva wetu wasipimwe wanapoingia kwenye hizo nchi? Au tunataka madereva wetu hata wakipimwa wakaonwa wana Corona waruhusiwe tu kuingia kwa kuwa kwetu hakuna lockdown?
Ona kwamba madereva wetu wanasema hawaviamini vipimo vya Kenya. Kenya watafanyaje vipimo vya udanganyifu kwa madereva ambao wanapeleka bidhaa kwao? Hiyo ni akili kweli kudhani mtu unaemplekea bidhaa kama chakula nk akukomoe kwa kukufanyia kipimo cha uongo? Tanzania tunataka tuamini vipimo vipi, maana hata vya kwetu tulisema vinasema mapapai yana Corona ni vipimo feki. Kama ni hivyo tupimwe madereva wetu mipakani basi ili wanapopimwa upande wa Kenya tuweze kubisha kisayansi kuwa upande wetu tumewapima wakaonekana negative.
Vitu vingine tusijifanye kuwa wajuaji na kukorofishana na jirani zetu pasipo sababu. Hatuwezi kuwalazimisha wasiwe na restrictions za Corona kwa kuwa sisi hatuna. Kama sisi hatuna restriction basi ni sawa madereva wao kuingia kwetu bila kupimwa, lakini hatuwezi kudai kuwa na madeeva wetu waingie kwao bila kupimwa! KUmbuka kwamba madereva wa Kenya wakitoka Tanzania wanaporudi kwao wanawekwa quarantine - sasa kama wanafanya hivyo kwa madereva Wakenya, kwa nini tuone sio sawa wakisema madereva wa Tanzania wawekwe quarantine?
Tupe sababu za kisayansi mmefanya nini hadi kufikia mkataa kuwa vipimo vya Kenya haviaminiki. Na haviaminiki kwa Watanzania pekee?
wewe ujaelewa.hii ni vita ya kiuchumi kwa kusingizia corona.
embu fatilia kwa kina utafahamu tu.
na unaona ni tanzania tu ni kwa sababu tanzania ni chem chem ya neema inanyeshea nchi zoote za jirani
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hilo halitakuwa suluhisho, litakuwa ni tatizo
Mkuu JF wakati fulani ilikuwa na watu kama wewe na ilifurahisha kujadili mada.Tulikwa hata na mawaziri tukaongea mambo ya msingi kwa nchi yetu. Kisha wakaingia wana JF yeboyebo mambo yakaharibika! Utagundua kuwa kuna wana JF wengine waliamua kujitoa kwa sababu ya huu uvamizi.Dah mkuu umeanzisha Uzi wa maana sana Ila majibu unayopata yanasikitisha...Yaani Watanzania wengi ni wapumbavu sana
Wanachofanya Kenya ndio kinachofanywa na na nchi karibia zote Duniani kwenye usafirishaji wa bidhaa kipindi hiki.. Tanzania tumeenda kinyume kabisa na dunia nzima, halafu tunawalaumu Wakenya
Sent using Jamii Forums mobile app
kwenye vita ndo panasuluhu.imma mmoja ashindwe asalimu amri au nguvu ziwe sawa mtengeneze mkataba wa amani ili yaishe.Mkuu hilo halitakuwa suluhisho, litakuwa ni tatizo
Bora shule zifunguliwe,kaa kimya kuficha upumbafu wako.Ndio tatizo letu - kila kitu tunaona ni game fulani Wakenya wanataka kutufunga bao la tobo! Ninachoona hapa sio game, ni ujinga tu tunafanya hatuna la maana!
Tumezoea kuwapiga makonzi wapinzania na sasa tunadhani kila mtu tuna uwezo wa kumpiga konzi.
Hii hali isiposuluhishwa haraka kwa njia za kidiplomasia, EAC ina hatari ya kuvunjika.. na kuja kuungana tena itachukua Muda sana.Hizi bifu na Kenya sasa naona kama ni utoto na nashangaa inafikia hata viongozi wetu wa ngazi ya mkoa wanahemuka na maamuzi bila kufikiria kumaliza mambo kidiplomasia. Hawa viongozi wanadhani wanamfurahisha Magufuli lakini ukweli ni kwamba wanamdhalilsha Magufuli na Tanzania kwa ujumla.
Ona kwamba tumekuwa na migogoro mipakani sio na Kenya tu, bali na Rwanda na Zambia pia. Hiyo ni dalili kwamba sisi ndio wenye tatizo. Ukiona kila siku wewe tu ndio unagombana na jirani zako, tatizo sio jirani, ni wewe!
Kwanza kabisa tuelewe kwamba nchi hizi jirani, japo sisi hatukuweka lockdown, wao waliweka. Sasa hatuwezi kuwalazimisha wasiwe na lockdown kwa Watanzania kwa kuwa sisi huku kwetu hakuna - huko ni kukosa si tu busara bali akili pia. Kwa mfano, Kenya wana lockdown kiasi kwamba hata kusafiri kati ya jimbo na jimbo, mfano, Nairobi na Mombasa, hairuhusiwi isipokuwa kwa vibali maalum.
Sasa sis tunachotaka kwa Wakenya au Rwanda au Zambia ni nini hasa? Tunataka madereva wetu wasipimwe wanapoingia kwenye hizo nchi? Au tunataka madereva wetu hata wakipimwa wakaonwa wana Corona waruhusiwe tu kuingia kwa kuwa kwetu hakuna lockdown?
Ona kwamba madereva wetu wanasema hawaviamini vipimo vya Kenya. Kenya watafanyaje vipimo vya udanganyifu kwa madereva ambao wanapeleka bidhaa kwao? Hiyo ni akili kweli kudhani mtu unaemplekea bidhaa kama chakula nk akukomoe kwa kukufanyia kipimo cha uongo? Tanzania tunataka tuamini vipimo vipi, maana hata vya kwetu tulisema vinasema mapapai yana Corona ni vipimo feki. Kama ni hivyo tupimwe madereva wetu mipakani basi ili wanapopimwa upande wa Kenya tuweze kubisha kisayansi kuwa upande wetu tumewapima wakaonekana negative.
Vitu vingine tusijifanye kuwa wajuaji na kukorofishana na jirani zetu pasipo sababu. Hatuwezi kuwalazimisha wasiwe na restrictions za Corona kwa kuwa sisi hatuna. Kama sisi hatuna restriction basi ni sawa madereva wao kuingia kwetu bila kupimwa, lakini hatuwezi kudai kuwa na madeeva wetu waingie kwao bila kupimwa!
KUmbuka kwamba madereva wa Kenya wakitoka Tanzania wanaporudi kwao wanawekwa quarantine - sasa kama wanafanya hivyo kwa madereva Wakenya, kwa nini tuone sio sawa wakisema madereva wa Tanzania wawekwe quarantine?
Ona pia thread hii:
Tunaweza kuona tuna msimamo imara suala la Corona lakini mwishoni gharama yake inaweza kuwa Tanzania kukosa heshima na kupoteza urafiki na nchi jirani
Ndio tatizo letu - kila kitu tunaona ni game fulani Wakenya wanataka kutufunga bao la tobo! Ninachoona hapa sio game, ni ujinga tu tunafanya hatuna la maana!
Tumezoea kuwapiga makonzi wapinzania na sasa tunadhani kila mtu tuna uwezo wa kumpiga konzi.
Uswiss wamepakana na Florida? Kwanza Florida ni nchi?Uswizi na florida wanatumia utaratibu upi ?
MONEY STOP NONSENSE
Aisee inasikikitisha sana, badala ya watu hawajadili hoja hata wakatae tu, Ila wanatukana..@moderator sijui nao vipMkuu JF wakati fulani ilikuwa na watu kama wewe na ilifurahisha kujadili mada.Tulikwa hata na mawaziri tukaongea mambo ya msingi kwa nchi yetu. Kisha wakaingia wana JF yeboyebo mambo yakaharibika! Utagundua kuwa kuna wana JF wengine waliamua kujitoa kwa sababu ya huu uvamizi.
MkuuTatizo nadhani linakuja hapa.
Nafunga mpaka upande mmoja, bila kuingia mezani na jirani ili kujua ni hatua gani tuchukue kwa pamoja kuweka mambo sawa.
Unaweza kuwa upo sawa kulinda wananchi wako, ila jirani nae anaweza kuja hoja yake.
Kwa hivyo ilipaswa wawasiliane kwanza wahusika.
Ukiacha kila mtu afanye kivyake ndio hii mikorogano tunayoshuhudia leo hii.
Si mliitwa kwenye kikao cha EAC Mkaingia mitiniTatizo nadhani linakuja hapa.