lufulondama
Member
- Nov 13, 2019
- 95
- 194
Habari za asubuhi, wanajamiiforums.
Niko hapa kuomba msaada kwa haya yanayonisibu. Mimi ni kijana wa umri wa miaka30 kamili. Ni mwajiriwa serikalini. Niko hapa kuwataka msaada wa kimawazo kwa hali ninayopitia ambapo naona kama kuna kitu hakiko sawa kwangu.
Niliwahi kuishi kwenye ndoa kwa takribani miaka miwili ambapo hatma ya ndoa ilikua kufiwa kwa mwenza wangu hivyo nikabaki single. Hii imetokea last year 2019 March. Baada ya kukaa kwa takribani miezi 9, baada ya kukutwa na hili, niliamua kutafuta mwenza mwingine ambaye tungesongesha maisha ndipo nakutana na changamoto hizi.
Nilipata binti wa kijaluo toka ujaluoni ambaye ni mhitimu wa elimu ngazi ya degree ila hana ajira. Binti niliempata nimemkuta akiwa na mtoto mmoja wa miaka tisa. Kiufupi kabla sijapata uhakika wa tabia za binti vizuri nilijikuta naingia kwenye mtego baada ya binti huyu kupata ujauzito.
Licha ya kuwa sikujipanga ila nilifurahi sana kwani sijabahatika kupata mtoto na akaishi. (Marehemu mke wangu amefariki akiwa na kichanga changu pia). Sasa baada ya kuamua kulea ule ujauzito ambao mpka sasa tunategemea kupata kichanga next year January, nikajikuta napewa jukumu la kumlea yule mtoto niliemkuta kielimu (kulipia ada na mahitaji mengine).
Baada ya muda binti akaja kuishi kwangu nami nikaliafiki hilo ili tuzidi kufanya maisha nikiwa na imani kuwa nitamrasimisha soon tu baada ya kujifungua mtoto.
Leo ni wiki sasa kuna mambo yamejitokeza, binti aliniambia niwe na uharaka wa kumtolea mahali kabla Desemba. Baada ya kuambiwa kuhusu hilo niliamua kudodosa uhalisia wa kiasi cha pesa ambacho ningetakiwa kutoa kama mahari, nikawa nimejibiwa. Ila kuanzia juzi kuna kitu nimekinotice, kuanzia baba, mama, baba mkubwa na wengine wengi kila mmoja amekua akitaja kiasi cha pesa au kitu anachokihitaji ili kiwe nimekiambatanisha kwenye hio mahari, baada ya kupiga mahesabu naona kabisa inazidi 2m na hapo hapo majukumu mengine yananikabili. (Nauguza mama angu mzazi ambaye yuko hoi kitandani).
Baada ya kuliona hili binti haoneshwi kustushwa na taarifa ya kuuguliwa kwangu pengine tukasogeza mbele hii shughuli yeye anaishia kusema pole tu huku mengine yakiendelea(means hizo taratibu zake za kutaka mwisho wa mwezi huu niende kwao).
Kuna kitu nimegundua kuwa nisipokua makini jamii yangu itanishangaa endapo nitaenda kutoa mahali na wakati tuna mgonjwa akiwa hoi.
Nayoyafikiria kichwani mwangu ni haya, Nimekuwa mtu wa kupoteza muda wangu na pesa zangu kujaribu mahusiano ambayo yatakua yenye tija kwangu hivyo muda unaenda na sioni kupiga hatua za maendeleo yangu binafsi.
Nataka nichukue kiasi cha milioni 5 au 4 kisha nimkabidhi kwa maandishi mbele ya wanasheria kuwa ninampa kama msingi wake utaomsaidia baada ya kujifungua kufanya lolote ambalo, lakini pia kuandikisha kuwa nitalea ujauzito na mtoto baada ya kujifungua salama mpaka atakapofikia umri nimchukue niishi nae mwenyewe. Kiufupi naona nataka kupata mzigo mkubwa sana mbeleni nisipokua makini.
Naombeni msaada wenu wakuu ninahisi nimebugi kwa hili aisee nifanye nini kwa mazingira hayo.
UPDATE:Hakuna mwitikio chanya hata baada ya kuamua kumueleza binti kua tusitishe rasmi zoezi mpka bi mkubwa apone, naona ni full kununa tu