ninahisi ninatatizo mwilini plz nisaidieni

mjax

Senior Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
177
Reaction score
62
Mimi ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 26, ni muhitim wa chuo. Tatizo langu ni kwamba nikiongozana na mtu yeyote awe rafiki yangu au hata nikipishana na mtu ambaye hatufahamiani naye, kama hajashika pua basi atatema mate chini. Kiukweli hali hii inanikwaza sana, kwani hata kama nimetoka kuoga muda huo na nimejipulizia body spray bado nikitoka nitakumbana na hali hiyo. Natamani sana kuwauliza marafiki zangu nashindwa, na hiyo hali imeniathiri sana kisaikolojia kwan kwa sasa naogopa hata kujichanganya kwenye umati wa watu. Please naombeni sana ushauri wenu!!
 
Pole sana kaka.
Tafuta pesa uende Apolo. Si unakumbuka Mwakiyembe?? Nenda huko huko alikoenda maana naamini tatizo lako linahitaji wataalamu waliobobea. Anyway, cjui kwa hapa Tz.
 
Kama ni mwamini,nenda kafanyiwe maombi,halafu msikilize your innerman anasemaje,maana si wote wanaojiita manabii au wachungaji,au mapastor ni wako kwenye nguvu za mwanga wengine wako kwa nguvu za giza,Bwana Yesu akusaidie sana
 
Kama ni mwamini,nenda kafanyiwe maombi,halafu msikilize your innerman anasemaje,maana si wote wanaojiita manabii au wachungaji,au mapastor ni wako kwenye nguvu za mwanga wengine wako kwa nguvu za giza,Bwana Yesu akusaidie sana

...naounga mkono hoja,kama upo Dar nenda hapo kwa Rev. Katunzi chuo cha bandari anafanya maombezi kila jumapili kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni. Kwa mtazamo wangu wa haraka tatizo lako inaweza kuwa la kiroho zaidi,afterall hupungukiwi kitu ukipata tiba ya kiroho inayotibu matatizo yote ya ajabuajabu...
 
Pole sana ndgu yangu...kwa harakaharaka..hebu pima tumbo lako limekaaje kaka..

Matatizo mengi ya harufu mwilini husababishwa na mchafuko wa tumbo.cheki tumbo lako kama liko sawa halafu jitahidi kutumia maji, mdalasini,tangawizi mbichi na vitungu saumu kwa wingi.

changanya vitunguu saumu punje 4 na maziwa fresh moto kila siku asubhi na chai ya rangi yenye mdalasini+tangawizi mbichi vyote viwe kiasi na maji ya kunywa kwa muda wa siku 70 tu, then lete matokeo.

ila usiache kumshirikisha MUNGU kwenye hii dozi.
 
well said Gefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…