Mimi ni kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 26, ni muhitim wa chuo. Tatizo langu ni kwamba nikiongozana na mtu yeyote awe rafiki yangu au hata nikipishana na mtu ambaye hatufahamiani naye, kama hajashika pua basi atatema mate chini. Kiukweli hali hii inanikwaza sana, kwani hata kama nimetoka kuoga muda huo na nimejipulizia body spray bado nikitoka nitakumbana na hali hiyo. Natamani sana kuwauliza marafiki zangu nashindwa, na hiyo hali imeniathiri sana kisaikolojia kwan kwa sasa naogopa hata kujichanganya kwenye umati wa watu. Please naombeni sana ushauri wenu!!