Ninahitaji mkopo wa machine hii:

Ninahitaji mkopo wa machine hii:

Fadhili Paulo

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2011
Posts
3,211
Reaction score
993
Habari Wakuu,

Ninahitaji kampuni au mtu anayeweza kunikopesha mashine hii hapa kwenye picha, nahitaji chombo chenyewe kama kilivyo na siyo pesa lakini sina dhamana. Nitalirejesha deni hili (katika fedha) baada ya miezi 6 na nipo tayari kulipia riba ikiwa itakuwepo
Power-Tiller.jpg
Aliyetayari kunisaidia nitashukuru, nipo dar kwa sasa ila nikiipata tu naelekea mbeya.

Shukrani
 
Wazo zuri kamanda, jaribu T.I.B huwa wanautaratibu wa kukopesa zana za kilimo kwa wakulima kwa utaratibu maalum.
 
Wazo zuri kamanda, jaribu T.I.B huwa wanautaratibu wa kukopesa zana za kilimo kwa wakulima kwa utaratibu maalum.
Ahsante mkuu, nitajaribu pia kwenda kupata utaratibu, kumbuka sina dhamana
 
Mkuu mi naomba nikuulize swali,,unaenda mbeya kulima nini? Mazao gani,yanachukua mda gani kukomaa'?maswali hayo ukijibu utawapa watu mwanga wa kukusaidia,na kiwango chako cha elimu.nijbu
 
-Unahitaji mkopo wa hii machine, je ni kiasi gani?
-Uta mconvince vipi mtu anayekukopesha kama utarudisha pesa bila kuwa na dhamana?
 
Kama una salary kwa maana ya ajira inaweza kuwa dhamana. Ongea na TIB kwanza uwasikilizie. Kila la kheri
 
-Unahitaji mkopo wa hii machine, je ni kiasi gani?
-Uta mconvince vipi mtu anayekukopesha kama utarudisha pesa bila kuwa na dhamana?

Mkuu nashukuru kwa muda wako;
1. Mkopeshaji ndiye atasema hiyo mashine ameambiwa ni bei gani dukani, natumaini haizidi mil 3 au 4.
2. Soma post # 5

karibu mkuu
 
Kama una salary kwa maana ya ajira inaweza kuwa dhamana. Ongea na TIB kwanza uwasikilizie. Kila la kheri

Mkuu, ni kweli nina salary lakini nafanya kazi na private company siyo serikalini na bado sina mkataba, pia ninavyojuwa wakopeshaji wengi wanapenda kuwakopesha wanaofanya kazi serikalini.

Thanks by the way
 
Mkuu mi naomba nikuulize swali,,unaenda mbeya kulima nini? Mazao gani,yanachukua mda gani kukomaa'?maswali hayo ukijibu utawapa watu mwanga wa kukusaidia,na kiwango chako cha elimu.nijbu

Mkuu, nashukuru kwa muda wako:
-Naenda kulima mazao mengi yakiwemo mpunga, mahindi, vitunguu, karoti, tangawizi na viungo mbalimbali (spices & herbs) vinavyotumika mahotelini n.k. Ndani ya miezi 3 mpaka sita nategemea kuanza kupata mavuno.
-Elimu yangu ni kidato cha sita pia nina diploma ya hotel management and tourism pia diploma ya ICT (na-design websites).

Karibu mkuu
 
mkuu, nashukuru kwa muda wako:
-naenda kulima mazao mengi yakiwemo mpunga, mahindi, vitunguu, karoti, tangawizi na viungo mbalimbali (spices & herbs) vinavyotumika mahotelini n.k. Ndani ya miezi 3 mpaka sita nategemea kuanza kupata mavuno.
-elimu yangu ni kidato cha sita pia nina diploma ya hotel management and tourism pia diploma ya ict (na-design websites).

Karibu mkuu
best of lucky
 
kiukweli hakuna mtu au benk itakayokukopesha bila dhamana,nenda kijijini kwenu tafuta ardhi ukishaipata nenda ofisi ya ardhi uombe hati ya kumiliki ardhi ya kimila,haichukui muda mrefu na haina gharama kubwa,kwa kutumia hiyo hati unaweza kukopeshwa power tilla au trekta za SUMMA JKT kwa kudhaminiwa na halmashauri yako mimi nimefanya hivyo na karibu nitafanikiwa.

kwa maelezo zaidi ni pm.
 
Nashukuru mkuu kwa muda na mawazo yako, kwa bank ni kweli haiwezekani lakini kwa mtu binafsi inawezekana, natumaini nitapata tu mtu wa kunisaidia hapa.
 
Unalo shamba? ni lako binafsi au la kukodi? una maji ya kumwagilia? au unategemea mvua? jibu kwanza then ntarudi
 
kurasa zina-load slow sana,
Shamba ninalo mwenyewe, kilimo ni cha umwagiliaji na mvua pia, wakati wa mvua tunategemea mvua lakini zinapokatika kuna mto mkubwa karibu haukauki miezi yote 12. Kama utahitaji kukodi mashamba zaidi kazi ni kwako mkuu kule kijijini kwetu ukiwa na laki 1 unaweza kukodi hata hekali 5 kwa ajili ya mahindi, ardhi nzuri na haihitaji mbolea.

Karibu mkuu @SABAYI
 
Back
Top Bottom