Tumetangaziwa kuwa siyo muda mrefu Daraja JPM (Kigongo - Busisi) karibuni litafunguliwa na Mhe. RaIs wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Daraja hili limejengwa kwa gharama kubwa takriban Tshs.680bn. Watumiaji wa vivuko kwa hivi sasa wanalipa (1) Mtu mmoja Tshs.400 (1) Pikipiki Tshs.1,000 (3) Gari ndogo Tshs.6,500 (4) Bus/Magari makubwa Tshs.40,000. Natumaini daraja litakapokamilika kila siku siyo chini magari 2000 yatapita kwenye daraja hilo. Ninashauri tulipe hata nusu ya hizo gharama ili tujifunze kuwa hapo mbeleni kutakuwa na miradi ya PPP. Fedha zitakazopatikana zitaelekezwa kwenye miradi mingine ili kukuza uchumi.
Tusizoe vya bure tuanze kulipa kama wananchi wanavyolipa wanapopita kwenye daraja la Kigamboni.
Tusizoe vya bure tuanze kulipa kama wananchi wanavyolipa wanapopita kwenye daraja la Kigamboni.