Ninajamba sana ifikapo asubuhi

Kama hupati maumivu unapojamba unachoogopa nini? Hebu endelea jamba utoe mihewa michafu mwilini
 
mwisho wangu kula ni saa kumi na mbili jioni na nakula tu matunda ila bado hali ni ile ile

Unajamba kwa sauti (rajabuuuu) au kimyakimya (yasufuuuu), kama ni kwa sauti basi watu wa kusini wanasemaga hakuna shida ila unagain (unanenepa), kilo zinaongezeka
 
nakula tu kawaida usiku .chakula kidogo au matunda inategemea. kujamba kunaanza kabla ya kupata haja kubwa.ninashtuliwa na vijambo maana vinakuwa vikubwa mno .nadhani nitakuwa najamba hata usingizini
Du pole..
Lakini kujamba si afya. Kuna wengine wanatafuta kujamba.
 
Kwa raha zako jamba kwani hujui unapunguza gesi tumboni. Pia mkeo akipika maharage aweke kitunguu swaumu kinasaidia sana kwa gesi.
 
Kwa raha zako jamba kwani hujui unapunguza gesi tumboni. Pia mkeo akipika maharage aweke kitunguu swaumu kinasaidia sana kwa gesi.
mtoto anateseka sana na sauti za kujamba.kitunguu swaumu nimejaribu ndo naharibu nakijamba kizimakizima harufu ya kitunguu swaumu mbaya sana
 
Nimewahi kufanya kazi na Mdenish flani naye alikuwa na tatizo kama lako.
Alikuwa anatumia vidonge fln km paracetamol, akisahau kutumia yaani siku nzima ving'ora, na wenzetu kuja.. sio aibu so alikuwa anangurumisha haswa tena mbele za watu. Watu wakicheka anashangaa. Vile vidongo alikuwa anatumia alikuwa anasema vinaondoa gesi tumboni.
 
mimi mchana sijambi kabisa
 
Naombeni msaada wa kitabibu nina tatizo la kujamba sana wakati wa kulala sanasana kipindi cha alfajiri.
sina shida yoyote ya tumbo ila asubuhi nakuwa nalipuka haswa.naombeni ushauri
1:Minyoo
2:Typhoid
3:Ulcers
Jaribu jutumia Andrews liver salt kwa kunywa asubuhi.
Lakini pia nenda kapime minyoo (kunywa dawa ni sawa lakini kuna dawa badhi haziangamizi minyoo aina zote) bora kupima ili ikiwezekana ijulikane kama ni minyoo ni ya aina gani.
Lakini pia isije kuwa mchanganyiko wa matunda unayokula ndio hutengeneza hiyo E=MC² tumboni mwako.
 
Naombeni msaada wa kitabibu nina tatizo la kujamba sana wakati wa kulala sanasana kipindi cha alfajiri.
sina shida yoyote ya tumbo ila asubuhi nakuwa nalipuka haswa.naombeni ushauri

Acha kula maharagwe
Kula mboga za majani kwa wingi
 
sawa nashukuru nitaenda kupima ila sina tatizo lolote la tumbo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…