Nimekutafuta sana kwenye maisha,pamoja na kusoma sana na kuwa na akili nyingi naishi maisha magumu mno Tena ya kudharaulika.nina familia na watoto but nikama wife ananidharau baada ya kujipatia.nina hisi muda wowote anaweza kubipiga tukio kwa maana kauli zake siziekewi elewi.nahisi ya kuwa nilishapoteza dira siku nyingi.kimsingi nimepata hasara kwenye mambo mengi ambayo nimejaribu kuwekeza,nimeajiriwa but nahisi hakuna chochote naweza kufanya plus madeni niliyo nayo .siwezi kufanya jambo lolote la kumuumiza mtu mwingine.huwa nalaumiwa sana kwa vitu ambavyo sijafanya au siku husika nalo ,kimsingi ninachangamoto nyingi mno,sijui nifanyeje jamani
Pole sana nachelea kuuliza kwamba kwenye familia uliyotoka ina wasomi wa level yako kwa kiasi gani ila ni seme tu kwamba haya mambo huwa ni maagano wakati mwingine.
Mimi sijali kama huwa unaamini mambo ya rohoni au hauamini ila nakusihi sana stick kwenye imani yako na ujiconnect na wale malaika waliobeba hatima yako.
Umesema ulikua vizuri kwenye biashara then ukapata hasara, natamani kujua maisha yako kabla ya kuoa yalikua vipi hasa kwenye upande huo wa uchumi, sisemi kuwa napata mashaka na mkeo kwamba pengine frequency zenu haziendani ila dunia iko na mengi ya kushangaza ambayo kwa jicho la kibinadamu ni ngumu kuyaona.
Kingine kufeli kwenye biashara ni kawaida sana kwa watanzania wengi coz huwa tunaingia kwenye hizi biashara bila kuwa na taarifa kamili, ni mara chache sana unamskia mtanzania akisema ako na mentor ambae amefanikiwa kwenye kitu ambacho yeye anakifanya ili aweze kumpa njia na moral ya kupush zaidi... wengi hatupendi kutoa pesa ili tupate pesa.
Umeajiriwa so unapokea mshahara na hapo hapo mkeo hakuelewi kwahiyo ni either mshahara haukidhi mahitaji au standard za maisha ambazo mliishi hapo awali zilikua za juu sana kuliko za sasa kwahiyo bado yuko na ile saikolojia ya maisha ya nyuma.
Kama ndivyo basi haukumchunguza vizuri huyo mwanamke kabla hujamuoa coz inaonekana aliolewa na wewe kisa pesa na kama sio basi jitahidi usiwe sana muwazi kwake kwa maana wanawake wanapenda kuwa na watu ambao wanajifeel safe wakiwa nao.
Namaanisha usipende sana kulalamika lalamika ugumu wa maisha kila ukiwa nae na pia usioneshe hali ya kukata tamaa hadi akuone huwezi tena coz hapo atajifeel hayuko safe na ataanza kujiongeza.
SALI SANA BRO, ACHANA NA NYUZI ZA WALE WANAOKUAMBIA MUNGU HAYUKO, MUNGU YUPO NA WEWE UWEPO WAKO HAPA DUNIANI SIO KULA KUNYWA NA KUFA ILA IKO HATIMA AMBAYO WAPASWA KUITIMIZA KWAHIYO INAWEZEKANA KOTE AMBAKO UNAPITA UNAPATA UGUMU COZ SIO SEHEMU SAHIHI KULINGANA NA HATIMA YAKO, OMBA MUNGU AKUONESHE HATIMA YAKO EITHER DIRECT AU AKUKUTANISHE NA WATU WA HATIMA YAKO ILI WAWEZE KUKUTOA HAPO ULIPO NA KUKUPELEKA KATIKA VIWANGO VINGINE.
LASTLY: Ugumu wa maisha kwa kila mtu ambae anatafuta pesa kihalali lazima akutane nao kwa namna fulani ila cha muhimu hakikisha wewe na mkeo mnaungana ili huo mshahara unaoupata msave kwaajiri ya kunyanyua uchumi wenu upya, wanawake wanakuaga na macho sana ya kibiashara hasa hizi business za kuanza mdogo mdogo ambazo sisi kwa sehemu kubwa huwa hatuziwazi mara nyingi.
Wewe ndio mbeba maono ya familia ila unae msaidizi ambae anapaswa kukushauri pale unapokwama.