Kama ukitoa kila kitu kuanzia mshahara/matumizi yote unabakiwa na faida ya 80,000 to 100,000
sikushauri uache hiyo biashara hata kidogo,wewe kilio chako ni faida ndogo ila si kwamba hupati kbsa
wenzako wanaliaga hawapati kabisa,80k usiichukulie poa kwa biashara, hebu jiulize biashara yako hiyo
ukiendaga fata mzigo wa 80k unachukua vitu kiasi gani?! assume huitumiii hiyo hela iache usiiguse kwa
miezi 10 tu Utakuta kibubu kina 800k hivi ukijikaza ndani ya 10month ukichukua ile 800k ukairudisha yote
kwenye hiyo biashara yako unahisi utakua na stationary ya ukubwa gani? Shida yenu watu mliozoea ajira
mnapenda mahela mengi mengi yanayokuja kwa mara moja kama mishahara yenu ilivyo, Biashara/ujasiriamali haupo hivyo.
Huku tunakusanya sh 200 tu sh 100 tu sh 50 tu sh 500 then total tunakuja ipata baada ya miezi kadhaa SO mkuu nikwambie tu kitu, Biashara yako iko vizuri sana komaa hapohapo Punguza matumizi yasio na lazima
graph yako ya income kwa mwezi itaongezeka,Kingine akili yako iruhusu kufanya kazi zaidi unapoona biashara inakupa income ndogo usifikirie kuiacha "utaacha biashara ngapi"?
jifunze kuweka akiba na kujiona kama huna biashara ongeza biashara nyingine na nyingine kupitia hicho kidogo unachokipata kwa mwezi "biashara za mitaji ya laki zipo kibao" zifanye.
kuwa na biashara nyingi ndogo ndogo unapofika mwisho wa mwezi ukikusanya kote Utajikutaa mfukoni una not less ya 3 to 4m (depends na vibiashara vyako) Acha kupasuka kichwa na biashara kubwa kubwa.
Umeingia ktk ujasiriamali Cheza namba zote cheza miguu yote Kuwa kiraka kama mcheza mpira anaetumia left n right...
Mwisho : Usifunge wala usiache hiyo biashara bali itumie kama sehemu ya kupatia mitaji ya vibiashara vyako vingine... Go ahead Champion...