Ninakosea wapi? Au biashara ni kipaji?

Ninakosea wapi? Au biashara ni kipaji?

Mtoa mada nakushauri Jambo moja.

Kwenye iyo biashara yako,
Ondoa uyo mfanyakazi.

Weka mkeo,
Kama ujaoa ,oa haraka ili ujipatie cheap labor kwa msimamizi mzuri kabisa wa biashara yako.

NB: ndugu nao sikuhizi Ni magumashi. Niulize kwanini

Mke ndio mtu pekee wakuweza kukusaidia, achilia ndugu hata watoto ni mazonge matupu.
 
Wachangiaji wanamtia sumu mbaya mleta mada kwa mfanayakazi wake, Ndio haohao hulalamikia wahindi wanalipa hela ndogo, lakini wao ni wanyonyaji kinoma ndani ya nasi zao.
 
Mil.3 kama bado unaitaka nikupe uniachie kama ilivyo halafu tutafutane ndani ya mwaka 1

utaona wapi ulikua unakosea,usiitamani ile mil.3 kama bado una nia umedhamiria Njoo PM

bado nakwambia usikate tamaa hiyo biashara iko vizuri mkuu bila kujali umewekeza kiasi gani

hata kama uliwekeza 10m na unapata faida hiyo 80k bado nasema hiyo biashara si yakuiacha asee

Narudia :
kama kweli bado ile nia yako ya kuiachia hiyo biashara unayo,karbu pm tuyajenge.
Bruh CONTROLA nifungulie pm kuna jambo nahitaji kuteta nawe kama hutojali,natanguliza shukrani,
 
Jaribu kuongeza huduma Mfano upigaji wa picha za pasport size, Kupiga picha za ukutani na kutengeneza flame za picha, utengenezaji wa kadi za harusi, utengenezaji wa business card.... nk. Pia jaribu kutembelea mashule na vituo vya afya ili uwe mzabuni wa vifaa vya ofisi

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Kama ukitoa kila kitu kuanzia mshahara/matumizi yote unabakiwa na faida ya 80,000 to 100,000

sikushauri uache hiyo biashara hata kidogo,wewe kilio chako ni faida ndogo ila si kwamba hupati kbsa

wenzako wanaliaga hawapati kabisa,80k usiichukulie poa kwa biashara, hebu jiulize biashara yako hiyo

ukiendaga fata mzigo wa 80k unachukua vitu kiasi gani?! assume huitumiii hiyo hela iache usiiguse kwa

miezi 10 tu Utakuta kibubu kina 800k hivi ukijikaza ndani ya 10month ukichukua ile 800k ukairudisha yote

kwenye hiyo biashara yako unahisi utakua na stationary ya ukubwa gani? Shida yenu watu mliozoea ajira

mnapenda mahela mengi mengi yanayokuja kwa mara moja kama mishahara yenu ilivyo, Biashara/ujasiriamali haupo hivyo.

Huku tunakusanya sh 200 tu sh 100 tu sh 50 tu sh 500 then total tunakuja ipata baada ya miezi kadhaa SO mkuu nikwambie tu kitu, Biashara yako iko vizuri sana komaa hapohapo Punguza matumizi yasio na lazima

graph yako ya income kwa mwezi itaongezeka,Kingine akili yako iruhusu kufanya kazi zaidi unapoona biashara inakupa income ndogo usifikirie kuiacha "utaacha biashara ngapi"?

jifunze kuweka akiba na kujiona kama huna biashara ongeza biashara nyingine na nyingine kupitia hicho kidogo unachokipata kwa mwezi "biashara za mitaji ya laki zipo kibao" zifanye.

kuwa na biashara nyingi ndogo ndogo unapofika mwisho wa mwezi ukikusanya kote Utajikutaa mfukoni una not less ya 3 to 4m (depends na vibiashara vyako) Acha kupasuka kichwa na biashara kubwa kubwa.

Umeingia ktk ujasiriamali Cheza namba zote cheza miguu yote Kuwa kiraka kama mcheza mpira anaetumia left n right...

Mwisho : Usifunge wala usiache hiyo biashara bali itumie kama sehemu ya kupatia mitaji ya vibiashara vyako vingine... Go ahead Champion...
Ni kweli kabisa ulichoongea kwa experience yangu ya biashara ni unakusanya kidogo kidogo watu wenye ajira hawawezi elewa hivi vitu na mtu lazima ufwatilie trend ya biashara unajua sometimes mtu unafungua biashara unaweka mtu akuletee pesa tu hiyo haipo lazima ujue trend ya biashara na numbers hapo utaweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa
 
Mie nakupongeza tu kwa mshahara mkubwa....wengine mishahara yao haitoshi kula ugali na matembele mwezi mzima!

Punguza matumizi ya kuendeshea biashara...anza na mshahara wa mfanyakazi....kodi ya nyumba nk

Pili jitahidi uwepo golini kila siku baada ya majukumu yako utajifunza mengi
 
Back
Top Bottom